figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Mkoa wa Simiyu unahitaji mtu mzoefu na mwenye kusikiliza na Utii.
Sijui kuhusu Rushwa, ila Chatanda analaumiwa kuwa na kiburi, dharau na Majivuno. Hapokei simu ya Ofisi, anampa msaidizi wake.. Halafu msaidizi anakupa sababu. Jaribu kumpigia simu ya Ofisi then Jitambulishe kama Nyanzila ili ujue nisemacho. Bila kushirikiana na Wananchi, kazi ya Polisi utaiona ngumu.
Alipokuwa Pwani ajali ziliongezeka, akapelekwa Mtwara ajali zikaongezeka, akapelekwa Tanga ajali zikaongezeka, kapelekwa Simiyu Ajali zikaongezeka.
Pili hana mahusiano Mazuri na Club za Waandish wa habari hasa wa Simiyu, hawapi Ushirikiano.
Kwa ajali iliyoua watu 14, anatakiwa ashushwe cheo kwa Uzembe. Kaaibisha Jeshi la Polisi hadi linaanza kulaumiwa kwa kutozuia Ajali.
Tunaomba Umrudishe Dodoma apangiwe majukumu mengine.
Au akuandikie barua ya kukiri kwamba atabadilika na kuanza kushirikiana na Wananchi wa Simiyu wakiwemo Waandishi wa habari.
Mimi huwa nakubari utendaji wa IGP sababu ni Msikivu hadi nikampendekeza awe namba moja Tanzania kwenye Jeshi la Polisi.
Zaidi soma;
Thread 'Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) , ana hofu ya Mungu' Ili Nchi iwe na amani, Simon Sirro awe Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) , ana hofu ya Mungu