IGP Sirro, toeni elimu kwa askari wa usalama barabarani; wanatuchelewesha kazini

Kelele zinasaidia mwenye Mamlaka kuamka!! Nakumbuka 2016 Makonda alitoa agizo polisi wa usalama barabarani waongezwe Mara kumi zaidi!! Hadi polisi wa kulinda RAIA na Mali zao wakakosekana!! Sasa ni Muda muafaka kuwarudisha kwenye majukumu ya awali kupunguza usumbufu barabarani, Polisi watatu wanalinda taa nyekundu kukamata anaye jisahau!?
Kila mtu anajua kuwa trafic ni tatizo kubwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa
 
Kila mtu anajua kuwa trafic ni tatizo kubwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa
Piga kelele, kuna mwenye hekima atasikia, kwa dar Afande Mambosasa alishiriki kuwaongeza na Makonda
 
Wanabodi leo mara ya pili nimepatwa na shida ndiyo nikajua kuna tatizo.

Nineamka saa 11 niwahi ofisini trafiki amekamata daladala yetu kisa dereva hakusimama kwenye zebra. Toka saa 12 hadi sasa hivi saa 1:30 tumekalishwa hapa wanamsubiria tajiri wa gari, vitu havieleweki kabisa.

Nashindwa kuelewa kwanini trafiki asichukue hatua kwa dereva kama ni kosa akaandikiwa faini akatuwahisha abiria au wao ndiyo wanaamini wana haki peke yao, gari ni Heicher limebeba abiria wengi kweli watu wamesimama wanawachosha bila sababu.

Inahitajika elimu kwa matrafiki wa dar juu ya namna bora ya kusimamia haya mambo namna hii hatutafika kwakweli.
Saa moja na nusu?! Kwanini usidai nauli upande lingine?
 
Sasa mkuu hili ndo suluhisho la kudumu kweli?

Mtoa mada anataka suluhisho la kudumu kwa askari wote sasa ukisema ashuke apande basi jingine si itaendelea kuwa ndo tabia?

Halafu mia nne waiona ndogo watu wana bajeti zao na ukute ni kila siku lazima apande daladala.
Sio kwamba asilete malalamiko, hapana, alete lakini wakati huo akiwa ameshaoanda gari lingine
 
Hapo askari yupo sahihi kabisa, maana dereva amekiuka sheria.

Cha msingi shukeni mpande gari nyingine uyo muhuni akawekwe lockup, washaua sana ndugu zetu katika zebra hao madereva wavuta bange unaowatetea.
Hawatetei kama ni faini aandikiwe ili awahishe abiria kama ni kufukishwa kutuo cha polisi then mahakamani afikishwe haraka ilikusave muda sio mnakaa lisaaa wakati mnawahi kazini ni ujinga.
 
Echer imejaa vizuri angalau ina watu mia au zaidi trafic mmoja tu au wawili wanawapotezea mda kizembe tu alafu hamna la kufanya bado tuna safari ndefu sana nchi hii
Hilo halikuhitaji kulisema hapa au kuwatafuta wakubwa ni palepale anawajibishwa huyo mshamba
 
Kuna siku tulimpa kichapo traffic kwasababu ya issue kama hii. Yani tumepanda coaster tunawahi Moshi jamaa kasimamisha gari halafu akaondoka yupo busy kusimamisha mengine hataki kuzungumza na dereva.

Uzuri machalii wa Meru walikuwa wengi kwenye gari wakaona isiwe kesi tukashuka tukamtia jamaa nakoz halafu tukaamsha popo kwa kupanda gari jingine. Sijui kama ule msala uliwaacha salama wale jamaa wa ile coaster.
 
Back
Top Bottom