IGP Sirro, toeni elimu kwa askari wa usalama barabarani; wanatuchelewesha kazini

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
549
785
Wanabodi leo mara ya pili nimepatwa na shida ndiyo nikajua kuna tatizo.

Nineamka saa 11 niwahi ofisini trafiki amekamata daladala yetu kisa dereva hakusimama kwenye zebra. Toka saa 12 hadi sasa hivi saa 1:30 tumekalishwa hapa wanamsubiria tajiri wa gari, vitu havieleweki kabisa.

Nashindwa kuelewa kwanini trafiki asichukue hatua kwa dereva kama ni kosa akaandikiwa faini akatuwahisha abiria au wao ndiyo wanaamini wana haki peke yao, gari ni Heicher limebeba abiria wengi kweli watu wamesimama wanawachosha bila sababu.

Inahitajika elimu kwa matrafiki wa dar juu ya namna bora ya kusimamia haya mambo namna hii hatutafika kwakweli.
 
Mkuu siungeshuka ukapanda daladala nyingine na nauli ni 400? unapoteza muda sababu ya 400 kweli? trafic ni watu wa hovyo sn
 
Mkuu siungeshuka ukapanda daladala nyingine na nauli ni 400? unapoteza muda sababu ya 400 kweli? trafic ni watu wa hovyo sn
Sasa mkuu hili ndo suluhisho la kudumu kweli?

Mtoa mada anataka suluhisho la kudumu kwa askari wote sasa ukisema ashuke apande basi jingine si itaendelea kuwa ndo tabia?

Halafu mia nne waiona ndogo watu wana bajeti zao na ukute ni kila siku lazima apande daladala.
 
Mkuu hiyo ni ajali kazini kama ajali zingine, je gari ikiharibika utasubiri mpaka itengenezwe ndiyo uende kazini? lazima uwe na pesa ya dharura kidogo.
 
Hapo askari yupo sahihi kabisa, maana dereva amekiuka sheria.

Cha msingi shukeni mpande gari nyingine uyo muhuni akawekwe lockup, washaua sana ndugu zetu katika zebra hao madereva wavuta bange unaowatetea.
 
Sasa mkuu hili ndo suluhisho la kudumu kweli?

Mtoa mada anataka suluhisho la kudumu kwa askari wote sasa ukisema ashuke apande basi jingine si itaendelea kuwa ndo tabia?

Halafu mia nne waiona ndogo watu wana bajeti zao na ukute ni kila siku lazima apande daladala.
Hapo askari Hana kosa kwakweli, madereva wa daladala wengi hawana akili sawasawa
 
... tumsome "mzalendo" anayeomba kuungwa mkono na watanzania na ujumbe wake murua ... "piga risasi"

Magufuli baba lao, Makonda baba lao...
CCM baba lao, Wapinzani piga risasi
Tuna polisi, tuna jeshi...wamekwishaaa!
 
We mpaka leo hujui matatizo ya trafic barabarabani?
madereva wa daladala ni wendawazimu karibia wote,
Week iliyopita Kuna mmoja ameangusha gari mtaroni kisa walikuwa wanakimbizana kuwai abiria kituoni,

Hawa kamanda Awadh haji ndio alikuwa anaweza kudili nao
 
We mpaka leo hujui matatizo ya trafic barabarabani?
Kelele zinasaidia mwenye Mamlaka kuamka!! Nakumbuka 2016 Makonda alitoa agizo polisi wa usalama barabarani waongezwe Mara kumi zaidi!! Hadi polisi wa kulinda RAIA na Mali zao wakakosekana!! Sasa ni Muda muafaka kuwarudisha kwenye majukumu ya awali kupunguza usumbufu barabarani, Polisi watatu wanalinda taa nyekundu kukamata anaye jisahau!?
 
Mkuu hiyo ni ajali kazini kama ajali zingine, je gari ikiharibika utasubiri mpaka itengenezwe ndiyo uende kazini? lazima uwe na pesa ya dharura kidogo.
Kwa kawaida gari ikiharibika kondakta anarudisha nauli na kwahiyo haiathiri bajeti ya abiria. Kero ni utendaji wa trafiki kama anavyolalamika mtoa mada.
 
Back
Top Bottom