IGP SIRRO, siyo kila jambo la chumbani lastahili kuletwa sebleni

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,430
37,645
Kipindi Fulani nikiwa naishi Tabata nilikuwa na rafiki yangu tumeshibana kwelikweli. Rafiki huyu alikuwa na mtoto wa kiume umri miaka 3/4 hivi lakini machachari kweli.

Mtoto huyu alikuwa na Tabia ambayo kama mwanangu angekuwa nayo siku moja ningeenda jela kwa kosa la kujeruhi mtoto. Ukifika mgeni baada ya makaribisho na salam salaam mtoto ataelekea chumbani kwa Baba yake, huko atabeba chochote anachoweza kubeba cha Wazi au cha Siri ili aje amuoneshe mgeni fahari za Baba. Atakaa na hicho kitu hata kama ni chupi mpaka umwambie basi Rudisha nimeona.

Tabia ya mtoto wà rafiki yangu ndo ninayoiona kwa IGP SIRRO. Bwana huyu amewaambukiza Hadi watoto wake (RPCs) kutoa hadharani matendo ya ovyo ya Askari wake ambayo mengine hayapaswi kufika kwa Umma toka taasisi ya kijeshi.

Mfano, kulikuwa na haja gani kuwaanika hadharani Askari waliomuua Hamza? Ni faida gani kama ipo Jeshi la Polisi limepata kwa kuwataja kwa majina na kuwaonesha sura hadharani Askari waliotekeleza mauajj yale ambayo maelekezo ya chamzo chake bado yanaelea?

Jana yeye mwenyewe kajivua nguo kwa kututajia aibu yàke ya Polisi kufukuza magendo ya elfu 30. Siungi mkono utendaji mbovu wa baadhi ya Askari Polisi, na kosa zaidi Askari kuvuka mpaka WA nchi yako bila kibali cha mamlaka husika. Lakini Nani àlijua kwamba pikipiki Ile imebeba mzigo wa 30elfu kabla ya kuufungua?

Au Askari siku hizi wanatembea na Scanner kujua kilichomo ndani ya kiroba na kupotezea? Miongoni mwa sifa za Askari ni kuwa suspicious Muda wote na hii huwafanya wakamate silaha hatari au madawa hatari ya kulevya, lakini wakifanya hivyo wakafanikiwa hawalaumiwi kwa kiherehere.

Ifike mahali Sirro na makamanda wako mchambue Mambo ya kutoa hadharani, mengine mbaki nayo maana yanawavua nguo. Si kwamba Magereza na Uhamiaji hakuna madudu, na si kwamba hawana Maafisa habari, wanao lakini wanachambua pumba na mchele na kuacha chumbani visivyohtajika sebleni. Wewe Askari akigombana na mkewe tayari RPC anaitisha Press conference, hivi Walimu hawagombani ni wake zào?
 
Pale ni mahafalini....

Alitoa rai kwa wahitimu kama walivyotoa rai wengine kwa ajili ya kuwaasa.

Ulitaka awaambie kwa KUWANONG'ONOZA?!! Khaaa 😳😳😳

IGP Sirro hajakosea.
 
Back
Top Bottom