IGP Sirro: Sisi tunataka Lissu ndie afungue kesi, hatuwezi kufanya uchunguzi mpaka arudi

"Sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, atueleze ilikuwaje, nini kimemtokea, mazingira gani, na yule dereva wake tumemtafuta imekuwa shida. Yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao, lakini jinai haifi."- IGP Simon Sirro

HT: ITV
Duh...ama kweli, kwa hizi kauli inabidi tufunge na kuiombea nchi yetu. Kauli hizi si kiashiria kizuri kwa mustakabali wa nchi, kama siyo mtu kairoga serikali basi serikali imepigwa laana.
Kwa hiyo wale ndugu zetu walioshambuliwa kule mpakani na Msumbiji inabidi wao ndiyo wafungue kesi vinginevyo serikali haina cha kufanya katika shauri lao?
Hivi Sirro yupo kwenye utambuzi na utashi wake kweli?
Nini maana ya kulinda raia na mali zao?
Kwani Lissu kadhurumiwa hadi wamsubiri aje kufungua madai? Kwani kinachotakiwa ni uchunguzi kufanyika au kesi kufunguliwa?
Okay labda tukubali kuwa wanamsubiri, je watakubali aje kufanya uchunguzi kwa kutumia wapelelezi binafsi au kwa kutumia wapelelezi wa nje ya nchi?
 
"Sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, atueleze ilikuwaje, nini kimemtokea, mazingira gani, na yule dereva wake tumemtafuta imekuwa shida. Yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao, lakini jinai haifi."- IGP Simon Sirro

HT: ITV
Seriously!!!???
Kweli jinai mshtaki ni aliyejeruhiwa au serikali?? Serikali imemtelekeza au ndiyo mtuhumiwa. Ok Lissu njoo na wanasheria wale wa kimataifa mlio saini mkataba tumegundua majambazi ni Govt.
 
Kwan yule RPC wa mwanza ilikuwaje? Mbona watuhumiwa walipatikana wote?
"Sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, atueleze ilikuwaje, nini kimemtokea, mazingira gani, na yule dereva wake tumemtafuta imekuwa shida. Yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao, lakini jinai haifi."- IGP Simon Sirro

HT: ITV
 
"Sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, atueleze ilikuwaje, nini kimemtokea, mazingira gani, na yule dereva wake tumemtafuta imekuwa shida. Yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao, lakini jinai haifi."- IGP Simon Sirro

HT: ITV
Siro unatudanganya kwenye makosa ya jinai. Serikali ndo inashitaki,
Siro umejitoa akili ili kulinda kibarua
 
Sasa kama mpaka leo wameshindwa kumbaini muhusika basi waruhusu vyombo vya nje vichunguze mana tukio linaonekana lipo beyond na capacity zao hafu hio polisi kumejaa uvundo tu huwezi kusema watu kupotea haijaanza leo ina maaana kwa vile nyuma iliwahi kutokea basi leo tunaipa uhalali? Nini kimemfanya aje afanye iyo press ya kujiuma uma ivo
 
Hawezi kufungua Kesi kwa kuwa labda ndo mhusika mkuu wa plot yote, hivyo ni kama kujishitaki na ndo maana hawezi kurudi wala kumrudisha dereva.

Ila swali ni nani analipipia gharama za Tundu Lisu na familia yake Ulaya pamoja na dereva labda pia na Familia yake?

Chadema its time to cut him off, let him fall!
 
Back
Top Bottom