Moshi. Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amewataka viongozi wakuu wa vyama vya upinzani nchini, kuwasilisha malalamiko yanayohusu hujuma wanazodai kufanyiwa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali kabla au wakati wa mikutano yao ya ndani ili aweze kuyashughulikia.
“Kama kuna chama ambacho kinaona hakitendewi haki na Jeshi la Polisi, basi tuandikiwe malalamiko hayo ili tuweze kufuatilia kwa nini hiyo wilaya imeshindwa kutoa haki, waniandikie barua, nasisitiza sijawahi kupokea malalamiko yoyote ya barua kuhusiana na suala hilo (vikwazo vya polisi),” alisema Sirro.
Kauli hiyo imekuja siku chache tu baada ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kulitaka Jeshi la Polisi kutotumia nguvu kushughulikia migogoro ya kisiasa nchini.
Akiwa mkoani Manyara, Dk Bashiru alisema “tukianza kutumia mabavu katika kutatua migogoro yetu ni dalili za kushindwa kuongoza nchi, hakuna sababu wakati wananchi wanatii sheria bila shuruti.”