beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Heshima yako Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ndugu Simon Sirro.
Hongera sana kwa kuteuliwa kwenye nafasi hiyo ya juu. Hakika ulistahili na ndiyo maana taifa zima liiridhika kabisa na maamuzi ya Rais Magufuli kukupa wadhifa huo mkubwa.
Nimesikiliza kwa umakini mkutano wako na waandishi wa habari asubuhi ya leo. Pamoja na mambo mengine uliyozungumza, nimekusikia very well ukitangaza vita na wahalifu wanaoendeleza mauaji ya viongozi na raia ktk maeneo mbalimbali kama Kibiti, Vikindu, Rufiji huko Mkoani Pwani.
Ulinisisimua, nikasisimka. Na kwa rekodi yako ya utumishi, inaonyesha pasi na shaka kwamba umekuwa very successful kwenye operations karibia zote ambazo umewahi kuzisimamia, hivyo hili la Pwani sina shaka nawe hata tone.
Nina haraka kidogo, unaonaje tukizitumia hizi mbio za Mwenge zinazoendelea (kwa sasa zipo Dar) zikatumika KUMULIKA WAHALIFU waliojifcha huko Pwani na kutuulia ndugu zetu!?
Naamini ni fursa nzuri sasa kupeleka Ombi Maalumu kwa wanaohusika wakupatie kibali cha kuukimbiza huu Mwenge maeneo hayo ili uweze kuwaangaza washenzi hawa wanaotishia amani ya nchi.
Ukifanyia kazi wazo hili na ukafanikiwa, kwenye ile milioni 10 nipe 5 tu, kisha 5 iliyobaki
iwe ni kodi yangu kutokana na pato hilo (PAYE).
Nasubiri.