IGP Sirro: Nilikimbiwa na mchumba mwanasheria kisa Ukurya wangu

DAT BOY SU

Member
Nov 15, 2017
29
30
IGP Saimon Sirro amesema kwamba yeye aliwahi kukimbiwa na msichana aliyekuwa akimpenda kwa dhati ambaye alikuwa Mwanasheria, anaendelea kwa kusema mwanamke huyo ambaye ni mwanasheria alimkimbia kisa tu yeye Sirro ni Mkurya na story alizowahi kuzisikia huyo mwanamke ni kuwa Wakurya wanapiga wake zao, so na alihofia kupigwa endapo kama angemkubalia.

My take: Yule mwanamke sijui kwa sasa anajisikiaje kuona kuwa mwanaume aliyemtosa ni IGP wa leo. Na yeye usikute bado hajaolewa au ameolewa na mtu wa kawaida tu.

=======

Serengeti. Ukiachwa na umpendaye tena bila kupewa sababu inauma sana. Lakini ni jambo la kawaida katika maisha ya mwanadamu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro hayupo mbali na ukweli huo.Anakumbuka alivyoachwa na mchumba msomi kimyakimya baada ya kumtambulisha kwao.

Sirro mzaliwa wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara anasimulia jinsi alivyoachwa na mchumba wake waliyekutana chuo kikuu na kukubaliana kuoana kisha akamfikisha nyumbani kwao kumtambulisha.

Anasema baada ya kumtambulisha nyumbani mchumba huyo alitokomea kimyakimya bila kumwambia. Hata hivyo anasema alibaini kuwa sababu kubwa ni sifa mbaya za ukatili wa wanaume wa Mara ndizo zilizomkimbiza.

Akieleza kwa hisia taarifa hiyo wakati wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Dawati la Kijinsia na Watoto cha Mugumu, Wilaya ya Serengeti kilichojengwa na UNFPA , Sirro alisema vitendo vya ukatili vinafanya watu wasioe. “Watu wanaogopa, mimi niliachwa na mchumba msomi wa sheria kimyakimya hili si jambo jema,”alisema.

Alisema wanaume wa mkoa huo kuendekeza mfumo dume inayokinzana na mabadiliko ya kiulimwengu inasababisha madhara makubwa kwa wanawake, watoto na makundi mengine.

Alisema suala la mahari kubwa kwa mkoa huo linachangia ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike, akidai mzazi hafanyi kazi badala yake anategemea kuoza binti apate utajiri wa ng’ombe.

Alisema kwa sasa wana ofisi za dawati 420 kwa nchi nzima kwenye vituo vya daraja A,B,C hivyo askari wanatakiwa kushughulikia makossa hayo kwa usiri mkubwa ili mhanga wa ukatili asionekane ananyanyasika tena.

Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Marwa Ryoba alisema pamoja na mikakati mingi ya maendeleo mkoa wa Mara wanarudishwa nyuma na ukatili wa kijinsia.

“Mwanaume unampiga mke na kumkata kwa panga, unamkata mke wako masikio hii ni tabia ya ajabu kama amekushinda mrudishe kwao, tunatakiwa kubadilika maana huu ni ukatili wa ajabu,” alisema.

Naye Rhobi Samwel, mkurugenzi wa Shirika la Matumaini kwa watoto wa kike alisema ukatili unawafanya watoto wa kike kukimbia kwao hali ambayo haitakiwi kuvumiliwa na kuomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.

Chanzo: Mwananchi
 
atasema yote yaliyo jificha
 
ni yeye tu alikataliwa..wanaume wa kikurya ndo tumekua lulu mjini saiv.
 
Siro bana,,,jf walimpiganiaga sana huyu siro awe igp,hivi kisharudisha shukrani kweli?
 
Back
Top Bottom