IGP Sirro ni mjanja, nafikiri kesi ya Sabaya unaleta matokeo chanya kwa wenye Mamlaka

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,880
Herehoa!

Kesi inayomkabili Sebaya vyovyote itakavyoisha, iwe Kwa kushinda Kwake au kushindwa kwake lakini imetoa funzo kubwa Kwa wenye mamlaka hasa Wale wanaopewa Amri na kuifuata.

Katika maelezo ya Sebaya, alisema kuwa mambo aliyokuwa anayafanya alikuwa akiagizwa na wakubwa wake. Hata hivyo utaratibu wa kazi za Serikalini unafahamika kuwa kazi yoyote ya kiofisi inapaswa iende Kwa maandishi.
Sasa Sebaya anakazi mbili, mosi kuthibitisha kuwa alikuwa akiagizwa na wakubwa wake, na pili, kujitetetea yeye Kama yeye mbali na HAO wakubwa waliomtuma.

IGP Siro baada ya kupokea Oda kutoka Kwa Waziri Gwajima kuwa wamtie nguvuni Askofu Gwajima ili ajibu na athibitishe madai yake. IGP Siro ameuona mtego huo, ndio maana akasema anasubiri Barua Rasmi itakayotoa maelekezo ya kumkamata huyo mtuhumiwa.

Hata hivyo maelezo ya IGP Siro sio tuu anahitaji Barua lakini ndani ya hiyo barua iwe na maelezo yanayojiyosheleza ya kumkamata Askofu Gwajima.

Hii inatuambia nini?
Hii inatoa funzo Kwa watu wengine kuwa, Mkubwa akikutuma hasa ishu za kikazi ni vizuri utaratibu ufuatwe, mambo ya kufanya kazi kienyeji huko mbeleni likitokea lakutokea unashangaa jumba bovu linakuangukia wewe pekeako.

Wanaosema, kuwa kwa nini IGP Siro Raundi hii kwenye sakata la Gwajima na Shemeji yake ndio kataka Barua Rasmi, na sio baadhi ya vipindi vilivyopita hasa kuwakamata wapinzani. Jibu kinaweza kuwa, kila siku watu wanajifunza. Kuna kujifunza Kwa njia rahisi na kujifunza Kwa njia ngumu.
Kuna kujifunza wewe mwenyewe na kujifunza kupitia wengine.

Wito: kila Mmoja afuate taratibu za kazi yake. Haki, upendo na sheria zifuatwe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
 
Bado hiyo haitoshi kututhibitishia hakuna ubaguzi katika utekelezaji wa majukumu ya polis has a linapokuja jambo linalohusu wanaotofautiana na sirikali katika mtazamo wa kisiasa, au wapinzani tena zaidi Chadema.
 
Umeandika makusudi Sebaya badala ya Sabaya au umekosea tu kwa bahati mbaya
 
Bado hiyo haitoshi kututhibitishia hakuna ubaguzi katika utekelezaji wa majukumu ya polis has a linapokuja jambo linalohusu wanaotofautiana na sirikali katika mtazamo wa kisiasa, au wapinzani tena zaidi Chadema.
Sirro mnafiki. Siku zote anatekeleza hata bila kuambiwa just by hisia tu kwamna Rais hapendi Chadema basi anatuvaa.
 
Mbona alishaharibu sana siku zilizopita, kama ameshtuka leo basi amechelewa, Sirro akili humrudia akifanya kazi za CCM, lakini akitumwa kukamata upinzani hasa CHADEMA akili zake hufyatuka kabisa.
 
Hakuna kitu hapo kwanza huyo IGP wenu kajidhalilisdha sana , wengine wakipewa tu matamko hata ya kwenye facebook wanawakamata usiku wa manane kwa kuvunja milango ya hoteli, wengine mpaka barua za maelekezo yaani katika vilaza wanaojitia aibu nchi hii ni huyo sirro, he is inept
 
Mamlaka Iliokuwa inamtuma Sabaya sijui hata kama ungekua wewe ungohoji zaidi ya utekelezaji kuifurahisha cuz ilikua ni katili.
 
Mamlaka Iliokuwa inamtuma Sabaya sijui hata kama ungekua wewe ungohoji zaidi ya utekelezaji kuifurahisha cuz ilikua ni katili.

Unahoji Kama unajiamini, lakini Kwa maslahi binafsi na familia huwezi ukahoji.

Mtu aache Kula posho na Mshahara mnono kisa Kanuni na taratibu
 
Bado hiyo haitoshi kututhibitishia hakuna ubaguzi katika utekelezaji wa majukumu ya polis has a linapokuja jambo linalohusu wanaotofautiana na sirikali katika mtazamo wa kisiasa, au wapinzani tena zaidi Chadema.

Atakuambia ameajiriwa na serikali ya CCM Bwashee
 
Herehoa!

Kesi inayomkabili Sebaya vyovyote itakavyoisha, iwe Kwa kushinda Kwake au kushindwa kwake lakini imetoa funzo kubwa Kwa wenye mamlaka hasa Wale wanaopewa Amri na kuifuata.

Iyee, iyeee, iyeeee! Mpaka iki. Mira uu mrisha na mroti wa kukuendia akagurwa na vakarungu nire thari. Eneitanga aa magonji akwe eagurie mitwi yavo iti amghenje kutonga ha ava vakarungu. Wekiongeja na uu chasaka eguriwe kiidimika moshi ufuke handu.

Magonji auu mghenji eidima agharuke nguto na angi hangi eho uko hauu mlala mbaha wa ithanga ili. Ni huvodu mira herehoahoa mbaghia ya mathetha thinaivona handu mira ithibereshwe.
 
Back
Top Bottom