Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,217
ALIYEJISAIDIA HAJA NDOGO JUU YA KICHWA CHANGU NIKIWA GEREZANI”
Nelson Mandela: “Baada ya kutawazwa kuwa rais niliwaomba Baadhi ya walinzi wangu wa karibu kutembelea mgahawa fulani mjini ili kupata chakula cha mchana.
Tulifika kwenye mgahawa huo baada ya matembezi mafupi na kuagiza chakula”.
“Punde muhudumu akaleta tulivyoagiza, na nikaona mbele yangu yuko mtu mwingine anasubiri alichoagiza. Nikamtuma moja ya mlinzi wangu amuagize mtu yule ajumuike nasi tupate wote chakula cha mchana”.
“Mtu yule bila kusita alifika kwenye meza yangu na chakula chake. Lakini hakuwa na hali nzuri kabisa, kwani mikono yake ilikuwa inatetemeka vibaya sana, alishindwa kunitazama usoni hadi chakula kilipoisha na akaondoka zake”.
Moja wa ya mlinzi akamwambia mandela baada ya mtu yule kuondoka: “Inaonekana mtu yule alikuwa mgonjwa sana, kwani hakuishiwa kutetemeka muda wote amekaa hapa”.
Mandela akajibu: “Hapana, hakuwa mgonjwa hata kidogo”.
“Mtu yule alikuwa bwana jela katika gereza nililokuwa nimefungwa. Katika nyakati ambazo niliteswa kwa kupigwa na kila aina ya kadhia, niliomba msaada wa maji pale nilipopata kiu kikali sana, mtu yule bila huruma alifika na alinikojolea kichwani mwangu”.
“Hofu yake yote ile ni kuona mimi nimekuwa rais wa Afrika ya Kusini, kwamba naweza kumfanya chochote kwa sababu mimi ni Rais. Ila siwezi kumfanya kitu chochote kwa sababu hiyo mimi sio tabia yangu”
“Mara nyingi hulka za kulipiza visasi zinavunja sana mataifa, ila hulka ya uvumilivu na kusamehe, ina jenga umoja na utaifa”.
- NELSON MANDELA.
MY TAKE;
Mnavyo mtendea Freeman Mbowe sasa ipo siku mtajikuta mnatetemeka mbele yake kwa kudhani atawalipa kwa uovu wenu. Nani ajuaye kwamba Freeman hawezi siku moja kuinuliwa na muumba kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi?
OLE WENU WATAWALA WAOVU