IGP Sirro: Majambazi hawana uwezo, wangekuwa wanaona silaha na mafunzo mlionayo wasingethubutu

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka Askari wa Jeshi hilo kutimiza wajibu wao ili kuweza kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu pamoja na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani vinavyojitokeza kwenye jamii.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya medani za kivita katika kambi ya Kambapori iliyopo West Kilimanjaro, wilayani Siha ambapo Askari wa kozi ya cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi ambayo mafunzo yake yanahitimishwa leo Oktoba 8, 2021.

"Wahalifu wanafanya kazi kama timu ili kuwashinda ni lazima tufanye kazi yetu kama timu, na mimi nimetimiza wajibu wangu, kilichobaki ninyi mtimize wajibu wenu, uwezo mnao, majambazi wanachukua silaha na kunyang'anya watanzania huwa nawaambia uwezo hawana, wangekuwa wanaona silaha na mafunzo mliyonayo wasingethubutu,”amesema IGP.

IGP%20SIRRO%20WEB.jpg

Hamza mmoja aliwakalisha wanne tena hakujikinga wala kujificha iliwachukua saa nzima kumuangisha. Halafu siku ya Tuzo wanapewa askari 16, hadi unajiuliza hawa 16 walijificha na kulala nyuma ya fenci wanamkosaje jitu kubwa kama goliati tena linatembea kweupee, Msichezee hela zetu kwa hayo mafunzo hewa.:mad::mad::mad::mad:.

NB: Ukisikia polisi waua majambazi baada ya kurushiana risasi jua ni vibaka au walimuotea au wamepandikizia silaha

Turudi Tabora fisi mmoja alikoswa na risasi 49 hadi kuuawa wakiulizwa wanadai alikuwa anakwepa risasi:D:D:D:D
 
Wanachojua askari wa Tanzania ni ku act wako smarter ila ukiongea nae dakika 5 unajua chenga
 
Hamza mmoja aliwakalisha wanne tena hakujikinga wala kujificha iliwachukua saa nzima kumuangisha. Halafu siku ya Tuzo wanapewa askari 16, hadi unajiuliza hawa 16 walijificha na kulala nyuma ya fenci wanamkosaje jitu kubwa kama goliati tena linatembea kweupee, Msichezee hela zetu kwa hayo mafunzo hewa.:mad::mad::mad::mad:.

NB: Ukisikia polisi waua majambazi baada ya kurushiana risasi jua ni vibaka au walimuotea au wamepandikizia silaha

Turudi Tabora fisi mmoja alikoswa na risasi 49 hadi kuuawa wakiulizwa wanadai alikuwa anakwepa risasi:D:D:D:D
Kwamba hata Mimi nawashinda🤣🤣🤣
 
nyie ndo mtasababisha polisi wakitudaka waanze kukagua kwanza cm zetu wakikuta app ya jf kipigo kiongezeke maana tunaandika maneno ya kuwadharau sana
 
Back
Top Bottom