IGP Sirro: Kwa yeyote aliyepotelewa na ndugu anatakiwa kufika kwa DCI, miili iliyookotwa haijatambulika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Mtwara.
Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro amesema wameunda timu ya wataalamu kuchunguza miili iliyookotwa na sampuli kutoka miili hiyo zimechukuliwa.

Amesema iwapo kuna watu ambao ndugu zao wamepotea ni vyema wakafika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya vipimo na kufanyika upelelezi.

“Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu, haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi tumeunda timu ya wataalamu ya kupeleleza kuhusu miili hii, wamechukua majimaji kutoka mwilini,” amesema.

IGP Sirro amesema, “Kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike makao makuu ya Polisi upande wa DCI tuweze kufanya uchunguzi kuona kama ni ndugu yake.”

Amesema miili hiyo haijabainika kuwa ni ya watu wa Taifa gani.

“Tatizo letu Watanzania ni kwamba moja kwa moja wanaanza kuhisi, sijui kwa nini tunakuwa tunaishi kwa hisia na hii hisia hisia si nzuri, tuseme kitu tukiwa na uhakika. Ikitokea jambo utasema ni Sirro, utasema ni nani, hii si nzuri na niwaambie tumwogope Mungu pia,” amesema IGP Sirro.


mwananchi
 
Hivi mfano mnapokuwa mnakataza maandamano, huwa ni hisia au vichocheo vyenu vya mwili ndio vinakuwa vinafanya kazi?
 
Tatizo ukishakaa na BASHITE meza moja tu lazima na ww uwe hamnazo
 
ku
Wakija mtawaeleza walikufaje na nani aliwauwa? Kwani mmemaliza uchunguzi??!
kujkujitokeza kwa mtu aliyepotelewa na ndugu ni sehem Ya uchunguzi, vipimo vya kinasaba vikifanyika ndiyo conclusive
 
ku
Wakija mtawaeleza walikufaje na nani aliwauwa? Kwani mmemaliza uchunguzi??!
kujkujitokeza kwa mtu aliyepotelewa na ndugu ni sehem Ya uchunguzi, vipimo vya kinasaba vikifanyika ndiyo conclusive
 
Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu, haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi tumeunda timu ya wataalamu ya kupelelezakuhusu miili hii, wamechukuamajimaji kutoka mwilini,”

Hivi kwa nini sasa; wakati bahari hii ilikuwepo siku zote?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom