IGP Sirro, kukiri hadharani kuwa polisi hutumia nguvu za ziada ni sababu tosha ya kuondolewa nafasi yako

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
1,329
2,000
Kama mkuu wa polisi anakiri hadharani kuwa jeshi analolisimamia linatumia nguvu ya ziada basi ni wazi kuwa jeshi analosimamia huwa linafanya kazi kinyume cha sheria.

Ni nguvu gani ya ziada inayotumika? Kupiga watu walio mahabusu ya polisi? Kutesa mahabusu wa polisi?

Hii ni kinyume na katiba ya JMT na sheria amabyo inataka mahakama ndio kiwe chombo cha kutoa haki.

Pia ni kinyume na sheria ya ushahidi kifungu cha 27.

Huu ndio wakati wa Igp Sirro kupisha ofisi ya UIGP
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Mimi si mbaguzi na pia nachukia ubaguzi, ila kwa hakika zipo jamii kwa asili ukatili ni asili, tangungazi ya familia, Hadi wapatapo majukumu ya kitaifa, pekee kinachoweza kulisaidia taifa ni vetting yenye weledi, nasisitiza, sii ule weledi wa kitanzania, kwenye weledi tulisha feli, na haipo dalili ya kufufuka katika eneo hili, Kubwa ni kumwomba Mungu aturejeshee weledi wa viwango vya ulimwengu uliostaarabika. Weledi huo, ufanye kazi katika kufuata sheria na Katiba, utawala bora, democrasia ya kweli, chaguzi huru na hata weledi katika kutoa huduma za msingi kwenye jamii.
 
Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
18,686
2,000
Hueleweki kamanda!!!!!

Mara ushahidi

Mara kupiga mahabusu

Mara kutesa walio mahabusu

Kwan yeye kasema, wanatumia nguvu katika mazingira yapi?? Sikasema Kwenye kukamata na akatolea mfano. Ukiwa na bunduki, basi nawao watatumia bunduki.

Ni Tanzania tu ndo mnataka Majambazi, magaidi, wauaji ,wakamatwe kwa Kubembelezwa.
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,575
2,000
Hueleweki kamanda!!!!!

Mara ushahidi

Mara kupiga mahabusu

Mara kutesa walio mahabusu

Kwan yeye kasema ,wanatumia nguvu katika mazingira yapi?? Sikasema Kwenye kukamata na akatolea mfano... Ukiwa na bunduki, basi nawao watatumia bunduki .Ni Tanzania tu ndo mnataka Majambazi, magaidi, wauaji ,wakamatwe kwa Kubembelezwa.
Tanzania hatuna magaidi,wapo wanaoonewa.Kwani nyie mnasemaje?
 
Full Blood Picture

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
671
1,000
Kama mkuu wa polisi anakiri hadharani kuwa jeshi analolisimamia linatumia nguvu ya ziada basi ni wazi kuwa jeshi analosimamia huwa linafanya kazi kinyume cha sheria.

Ni nguvu gani ya ziada inayotumika? Kupiga watu walio mahabusu ya polisi? Kutesa mahabusu wa polisi?

Hii ni kinyume na katiba ya JMT na sheria amabyo inataka mahakama ndio kiwe chombo cha kutoa haki.

Pia ni kinyume na sheria ya ushahidi kifungu cha 27.

Huu ndio wakati wa Igp Sirro kupisha ofisi ya UIGP
Ndo ulichotumwa leo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom