beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kesho akiwashauri warudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao.
Ameeleza kuwa, baadhi ya viongozi wamekuwa wakihamasisha wapiga kura walinde kura, kitendo ambacho amesema ni dalili ya kufanya fujo.
Amesema kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanaolinda kura ni Mawakala ambao kila Chama imepeleka.
Amesema, "Kuna Vyama vinajiona vimeshashindwa kwahiyo malengo na nia iliyopo ni kufanya fujo. Niwaombe sana Viongozi wa Siasa, wakati huu si wakati wa kufanya fujo"
Kuhusu Zanzibar, Sirro amesema karibu watu 42 wamekamatwa Pemba kwa madai ya kuwashambulia Polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana
Ameeleza kuwa, mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo na hatarajii kuwe na vifo vyovyote, akisisitiza wasingependa Uchaguzi ambao unasababisha maisha ya watu kupotea