IGP Sirro: Ikicheza Simba/Yanga na Polisi Tanzania, shabikia Polisi Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema, amejisikia vibaya Yanga Sc walivyoifunga timu ya Usalama kwenye mchezo wa hivi karibuni

Amesema Jeshi la Polisi ndio wanaolinda usalama wa nchi sio Yanga Sc, hivyo ikitokea Usalama wamecheza na timu yoyote raia inapaswa washabikie Polisi kwa kuwa ndio wanaolinda usalama

Ameyasema hayo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Arusha akiwaelezea hali ya usalama kwa Moka wa Arusha kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu

Aidha amewataka vijana kutojihusisha na shughuli za uvunjifu wa amani siku ya Uchaguzi Mkuu kwa kuwa Jeshi la Polisi limejiandaa vizuri

 
Sasa sisi raia tunaanzaje kuwashangilia polisi.

Yeye atoe agizo kila timu yao inapocheza polisi wote wawe wanaenda huko.

Sisi raia tutashangilia timu zenu za kiraia.
 
1603626795902.png
 
..kwa mara ya kwanza nimemsikia IGP Sirro akitamka neno HAKI.

..Hongera sana kwa IGP Sirro.
 
Hakuna kijana wa kujihusisha na uvunjifu wa amani .mbona mnatusumbua sana kuhusu uvunjifu wa amani.? Hakuna kijana anaeipenda Tanzania halafu akaleta fujo, nyie ndio mtatusababishia huo uvunjifu uwapo mtamlazimisha ambae hajashinda kuwa mshindi.
 
Back
Top Bottom