IGP Sirro huyu Trafiki wako mwenye Mbwembwe Kawe, Lugalo na Mbezi Beach anapokea Rushwa bila Aibu huku akijiamini kabisa

Muache trafik wetu,tumempenda wenyewe,rushwa atoe mwingine kuumia uumie wewe,hiyo ni roho ya kasopata ,kasojidai ,kasozenga,umejuaje kuwa ni rushwa,kwanza rushwa za barabarani sisi wenyewe tunachangia,mtu mgari TZA bado uko nao road tu,mgari mbovumbovu,washkaji Wana wafanyia fear nyie mnamind,
 
Huwa kanakuwa njia panda ya Kawe pale Maringo na kuna muda huwa anakuwa njia panda ya Kawe pale Lugalo na wakati mwingine anakuwa Mbezi Beach Tangi Bovu.

Ni Trafiki ambaye mara kwa mara nimeona Watu wakimsifia kwa Kufanya Mbwembwe zake huku akiongoza Magari na nadhani huenda hili ndilo linamfanya hata akichukua Rushwa asijulikane na asijadiliwe Mitandaoni.

Leo kwa macho yangu mida ya 9 Kasorobo huyu Trafiki ila mwenye Mbwembwe jirani kabisa na ilipo Benki ya NBC Tangi Bovu akiwa anakagua Gari ya Dada Mmoja hivi iliyogongana na nyingine aliisimamisha Gari aina ya Canter ( Kenta ) iliyobeba Mbao kisha akawahi kwa Dereva na akapewa Tsh 5,000/= ambayo aliikunja Kiustadi na kuitumbukiza Mfukoni na kuendelea na Maisha.

Huku nikidhani kuwa huenda Tukio hilo la Kipumbavu na Kinyume na Maadili ya Kipolisi niliona peke yangu kumbe hata baadhi ya Madereva Bodaboda baadhi Jirani waliona na Kunishangaa huku wakisema kuwa Mimi ni Mgeni wa huyo Trafiki kwani Wao wameshamzoea na kwamba kwa Siku akikosakosa mno Pesa kuanzia Asubuhi hadi Jioni hakosi kati ya Tsh 50,0000/= hadi 75,000/=

Najua Maisha sasa ni Magumu hivyo kuna muda Mtu anaamua Kujiongeza kwa namna namna ila basi Staha itumike pamoja na Umakini.

Yaani kwa namna alivyoichukua ile Pesa ( Rushwa ) kiukweli imeonyesha kuwa haogopi, anajiamini na anaidharau ile Uniform yake na hata Jeshi la Polisi.

Mwisho IGP ikikupendeza kwa nia njema tu muonye huyu Kijana wako ( Trafiki ) aachane mno na tabia yake ya Kupenda tu Kutongoza hovyo Wanawake ambao huwa anasimamisha Gari zao ama Kuzikagua au kwa Makosa kweli ya barabarani.

Mdhibitini upesi sana asipende Rushwa.

Hakuna asiyepokea rushwa, umbea tu unakusumbua
 
Hii nchi raha saana yaani uovu unajengewa nyumba yaani...what a hell...mijitu imeshakuwa addicted na maisha ya hovyohovyo. Hivi Kila kosa lznmtu atoe helaa mengine si onyo au kalipio yaani mtu akikosea tuu azame mfukoni.....aisee
Ila ikipewa jina kama lile la solidality tax tunaona sawa tuu siyo ovyo ovyo?
 
Huyo wakati mwingine madereva wanampaga th sababu hata akikukamata na kosa ukiongea anakusamehe bila kudai kitu.
Anakula faida ya kuishi vizuri na madereva/watu
 
Acha wivu mzee si tunamtunza kwa mbwembwe zake sio rushwa hyoo bwege weewee!!=
 
Uzuri wa mambo haya ni kuwa watoaji wenyewe wanafurahia kuzitoa kuliko kulipa faini ya 30k,😂😂😂😂😂😂😀
 
Traffic wengi wamekaa kishari shari kuoteana ndo mana hatuwapendi ila Ashirafu hanaga noma yule jamaa, asubuhi baada ya foleni wanakaaga pale mbezi shule baada ya zebra, kama nnayo hata me huwa nasimama nampa la 5 au 10 akabrashi viatu. Kazi iendelee!!
 
50,000-75,000/= ni pesa kidogo sana.
Kuna wenzake wanazungushiana 100k kila siku na wako 7. Means kila siku mmoja wao anachukua 700k. Kwa mzunguko wa siku 7. Unaonaje hii? Its look beautiful eeh!!😂😂😂😂
 
Nimeshangaa na Kusikitika mno Ndugu yaani nimeleta Taarifa hii ili Dhambi hii imalizwe kwani ina madhara makubwa matokeo yake naambiwa nina Wivu nae, Chuki nae na Askari Mwenzake hivyo niko hapa Kumuharibia.

Acheni tu Watanzania tudharaulike sana.
Watanzania hawawezekani kokote kule duniani, Rushwa badala ya kuichukua wameshazoea na kuiona kawaida!
 
50,000-75,000/= ni pesa kidogo sana.
Kuna wenzake wanazungushiana 100k kila siku na wako 7. Means kila siku mmoja wao anachukua 700k. Kwa mzunguko wa siku 7. Unaonaje hii? Its look beautiful eeh!!
Iko hiviiii hata yule mkuu wao anaingiza zaidi ya 10Mil per day so tukae tutulie, tusifanywe tutoe yalipo vifuani.
 
Kabla hawajaanza na yule traffic waende pale Mbeya Central na waanze na RPC mpaka chini ni uozooo mtupu. Huyo traffic awe wa mwisho kabisaaaaaa.
 
Kuna ile mbinu yao ya kulizunguka gari,madereva wa gari za abiria wanajua,kondakta humfuata traffic huko na kupachika hela kwenye pachi pachi za bodi ya gari,dereva anaruhusiwa kuondoka,konda nae anaondoka huku nyuma noti znachomolewa kwenye bodi
 
Huyu trafiki anapendwa na madereva wengi sana kwa zile mbwembwe zake wengine husimama tu kumuangalia..na kufurahi ma kumtunza..hakuna cha rushwa wala mini acheni uongo
 
Huwa kanakuwa njia panda ya Kawe pale Maringo na kuna muda huwa anakuwa njia panda ya Kawe pale Lugalo na wakati mwingine anakuwa Mbezi Beach Tangi Bovu.

Ni Trafiki ambaye mara kwa mara nimeona Watu wakimsifia kwa Kufanya Mbwembwe zake huku akiongoza Magari na nadhani huenda hili ndilo linamfanya hata akichukua Rushwa asijulikane na asijadiliwe Mitandaoni.

Leo kwa macho yangu mida ya 9 Kasorobo huyu Trafiki ila mwenye Mbwembwe jirani kabisa na ilipo Benki ya NBC Tangi Bovu akiwa anakagua Gari ya Dada Mmoja hivi iliyogongana na nyingine aliisimamisha Gari aina ya Canter ( Kenta ) iliyobeba Mbao kisha akawahi kwa Dereva na akapewa Tsh 5,000/= ambayo aliikunja Kiustadi na kuitumbukiza Mfukoni na kuendelea na Maisha.

Huku nikidhani kuwa huenda Tukio hilo la Kipumbavu na Kinyume na Maadili ya Kipolisi niliona peke yangu kumbe hata baadhi ya Madereva Bodaboda baadhi Jirani waliona na Kunishangaa huku wakisema kuwa Mimi ni Mgeni wa huyo Trafiki kwani Wao wameshamzoea na kwamba kwa Siku akikosakosa mno Pesa kuanzia Asubuhi hadi Jioni hakosi kati ya Tsh 50,0000/= hadi 75,000/=

Najua Maisha sasa ni Magumu hivyo kuna muda Mtu anaamua Kujiongeza kwa namna namna ila basi Staha itumike pamoja na Umakini.

Yaani kwa namna alivyoichukua ile Pesa ( Rushwa ) kiukweli imeonyesha kuwa haogopi, anajiamini na anaidharau ile Uniform yake na hata Jeshi la Polisi.

Mwisho IGP ikikupendeza kwa nia njema tu muonye huyu Kijana wako ( Trafiki ) aachane mno na tabia yake ya Kupenda tu Kutongoza hovyo Wanawake ambao huwa anasimamisha Gari zao ama Kuzikagua au kwa Makosa kweli ya barabarani.

Mdhibitini upesi sana asipende Rushwa.
Umeongea la moyoni mwishoni kabisa la kutongoza mkeo. Hiyo ya rushwa kila sekta yenye mahitaji ya wengi ipo
 
Back
Top Bottom