IGP Sirro huyu Trafiki wako mwenye Mbwembwe Kawe, Lugalo na Mbezi Beach anapokea Rushwa bila Aibu huku akijiamini kabisa

Kwa jinsi anavyokubalika na watu huyo jamaa hata watu huamua kumpa hela ya ku-brash viatu kwa kiroho safi tu hata bila kuomba mtu.

Kuwa naye karibu jifunze kutoka kwake na wewe upate kibari kwa wale unaofanya nao kazi.

Inawezekana trafiki ukafanya kazi zako vizuri bila kuchukiwa na wananchi.
 
Trafik wa miji mikubwa ni hatari sana. Kuna wengine wapo maeneo ya Buigiri Chamwino Dodoma wananyodo sana. Kuna siku nilikutana nao Buigiri sokoni kuna local Mgahawa wamakaja Trafiki watatu wakawa na gari Wish nyeusi. Wanajinasibu kbs kama wao pesa za barabarani ni mali zao. Kama tungekuwa na uweledi ndani ya jeshi la Polisi. Hawa trafiki wote wangepelekwa FFU na wale FFU waje kuwa matrafiki. Hawa trafiki wanaUKWASI wa kutisha sana.
 
Kwa mtoa post uandishi wako unatia mashaka nadhani kuna jambo behind the scene
Kwa kifupi rushwa ipo ila kwa hili hujaliweka kuingia masikioni mwa watu vizuri
Kifupi hujaeleweka!
 
We ulitegemea asichukue rushwa kwa hela gani anayopata? Kwa marupurupu yapi mtu apende kushinda juani masaa 12+
Vumbi lake, jua lake, upepo wake, risk za ajali alaf asichukue elfu tano tano? Hata wewe ungechukua kwanza sio hela nyingi anajikimu tu.

Huko bungeni tunaibiwa kiasi gani kwa kutumia usanii wa kisheria? Kwenye mataasisi ya umma tunaibiwa kiasi gani kwa kisingizio cha stahiki za viongozi, manunuzi ya umma n.k

Acha tu apate hizo elfu tano tano maana polisi hawana extra duty, hakuna hela ya mazingira magumu achana na zile laki tatu tatu sijui chakula na blah blah gani.

Ile laki tatu anaisotea mwezi mzima wakati hela hiyo hiyo Gwajiboy anaipata kwa kikao kimoja tena akiwa kivulini, anapiga porojo tu, tena kwenye AC saafi kabisa
 
Mleta mada nadhani ni mgeni wa Traffic police, hakuna Traffic ambaye hachukui rushwa nchii. Uzuri naongea with evidence, kila kona ya nchi ni wala rushwa.

Ajali hizi za kila week hapa nilipo ni matokeo ya rushwa, mkikaribia walippo askari mnapakiwa kwa boda then akifika anampa traffic buku tano anaendelea na safari.

Asubuhi hio Morogoro road mabasi yote I mean yote ndio wanasimamishwa njiani wanawapa askari kati ya 5000-10,000 kwa over speeding au wrong overtaking..... Hii ni kati ya Mbezi na Chalinze.

Kwa huko Dar zile Kirikuu au Canter za mizigo zinaitwa "wali nyama" na askari maana wale ukifika unatoa buku mbili unaendelea na ukaguzi fake.

Juzi jirani na hapa kijijini kwa Bibi Mzaa Babu yangu imetokea ajali ya USO kwa USO kati ya Probox na L/cruiser ya Taasisi kisa tu, kuna lorry liliharibika kwenye corner kwa siku mbili bila Traffic kusimamia liondoshwe au kuwekwe tahadhari hadi pale probox ilipokua inapita eneo hilo kuvaana USO kwa USO na Cruiser. Traffic wakajitokeza na kuwaambia jamaa wa lorry waweke tahadhari.

Nimeshawahi kuwarekodi wakichukua rushwa.....nikafuta nikasema basi WACHA TUFE KWA UJINGA WETU.

KWAHIO kumtaja huyo Dogo ni sawa na tone mvua kwenye bahari

IMG_20210804_123339_391.jpg


IMG_20210804_123218_526.jpg


IMG_20210804_123300_513.jpg
 
Ngoja tukupe taarifa Huyo Mwamba Sharif ana Mashabiki wake kutokana na style yake ya ufanyaji kazi hivyo watu huwa wana mpa tuu fedha hizo buku tano ,buku kumi kawaida sana.
Anaitwa Dogo Ashirafu, nishamPa pesa tu bila kuombwa miaka ile 2017-2018 akiwa Bamaga kabla sijahamia huku Mkoani
 
Kwa sisi madereva wakongwe kitambo hicho hapa mjini,umenikumbushs kulikuwa na traffic
Alikuwa mkuda naye anaitwa "kimti"
Alikuwa anapenda sana kukaa pale magomeno
Mataa ,alisumbua sana enzi zake ila alikuja letewa zengwe alipotezwa kabisa alitupwa
Mkoano huko akapoteaa😂

Ova
 
Siyo kila Rushwa ina madhara, zingine zinafaida, hapo dereva angepigwa fine la 30 lakini Askari kamuonea huruma na kumpaa worning kwa buku tano,hata ningekua Mimi ningekubali kutoa la tano kuliko kutoa la 30 na Uchumi huu!!
Rushwa zote zina madhara, hii kauli ya kuwa sio kila rushwa ina madhara ndizo zinazopelekea kukua kwa tatizo! Tunakoelekea tunalibomoa taifa. Narudia tena "RUSHWA ZOTE ZINA MADHARA"
Kununua haki yako kuna madhara!!
 
Back
Top Bottom