IGP Sirro huyu Trafiki wako mwenye Mbwembwe Kawe, Lugalo na Mbezi Beach anapokea Rushwa bila Aibu huku akijiamini kabisa

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,753
2,000
Huwa kanakuwa njia panda ya Kawe pale Maringo na kuna muda huwa anakuwa njia panda ya Kawe pale Lugalo na wakati mwingine anakuwa Mbezi Beach Tangi Bovu.

Ni Trafiki ambaye mara kwa mara nimeona Watu wakimsifia kwa Kufanya Mbwembwe zake huku akiongoza Magari na nadhani huenda hili ndilo linamfanya hata akichukua Rushwa asijulikane na asijadiliwe Mitandaoni.

Leo kwa macho yangu mida ya 9 Kasorobo huyu Trafiki ila mwenye Mbwembwe jirani kabisa na ilipo Benki ya NBC Tangi Bovu akiwa anakagua Gari ya Dada Mmoja hivi iliyogongana na nyingine aliisimamisha Gari aina ya Canter ( Kenta ) iliyobeba Mbao kisha akawahi kwa Dereva na akapewa Tsh 5,000/= ambayo aliikunja Kiustadi na kuitumbukiza Mfukoni na kuendelea na Maisha.

Huku nikidhani kuwa huenda Tukio hilo la Kipumbavu na Kinyume na Maadili ya Kipolisi niliona peke yangu kumbe hata baadhi ya Madereva Bodaboda baadhi Jirani waliona na Kunishangaa huku wakisema kuwa Mimi ni Mgeni wa huyo Trafiki kwani Wao wameshamzoea na kwamba kwa Siku akikosakosa mno Pesa kuanzia Asubuhi hadi Jioni hakosi kati ya Tsh 50,0000/= hadi 75,000/=

Najua Maisha sasa ni Magumu hivyo kuna muda Mtu anaamua Kujiongeza kwa namna namna ila basi Staha itumike pamoja na Umakini.

Yaani kwa namna alivyoichukua ile Pesa ( Rushwa ) kiukweli imeonyesha kuwa haogopi, anajiamini na anaidharau ile Uniform yake na hata Jeshi la Polisi.

Mwisho IGP ikikupendeza kwa nia njema tu muonye huyu Kijana wako ( Trafiki ) aachane mno na tabia yake ya Kupenda tu Kutongoza hovyo Wanawake ambao huwa anasimamisha Gari zao ama Kuzikagua au kwa Makosa kweli ya barabarani.

Mdhibitini upesi sana asipende Rushwa.
 

4IR

JF-Expert Member
Apr 21, 2014
1,000
2,000
Muda wote huo unamchora tu? Hata kavideo au audio hamna. Umepoteza muda wako. Anyway, tutajie Askari wasiopokea rushwa huko barabarani, seems unawajua wote Dsm hii.
 

kasanga70

Senior Member
Oct 19, 2015
178
500
Hii nchi raha saana yaani uovu unajengewa nyumba yaani...what a hell...mijitu imeshakuwa addicted na maisha ya hovyohovyo. Hivi Kila kosa lznmtu atoe helaa mengine si onyo au kalipio yaani mtu akikosea tuu azame mfukoni.....aisee
 

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
2,656
2,000
Huyo traffic hachukuwi rushwa ni watu wanampenda sana kwa mbwembwe zake kwa hiyo kila mmoja anaamua kumpa chochote. Kwani huyo uliyemuona anampa pesa uliona amekamatwa kuwa gari lake bovu au kafanya makosa hapana wananchi wanapita na njia zao wanaamumua kumpa
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,597
2,000
Isije kuwa wewe ndo mwenye mke aliyetinduliwa na Emolo, maana si kwa kusaga kunguni huku......anyway, hiyo ya kubrashia viatu ilishapewa baraka na mamlaka ya juu, ingawaje walimu nao wangeruhusiwa kuchukua ya maziwa kwa ajili ya vumbi la chaki, halikadhalika wahudumu wa afya wachukue ya gloves na maafisa mifugo walambe ya kukagulia nyama. Kilichonishangaza ni bodaboda kufuatilia mahesabu ya mlungula anaolamba Emolo kwamba ni 50 hadi 75 kwa siku, sijui hiyo chobingo ya kusoma milungula wanakuwa wanaifanyia wapi....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom