IGP Sirro: Gari lililomteka Mo Dewji ni la nchi jirani. Kwa sasa hatuhitaji msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nje. Tuviamini vyombo vyetu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Nimewaita ili kuzungumzia matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza ndani ya Tanzania ili muweze kuwahabarisha watanzania.

Kwa ujumla hali ya nchi yetu ni shwari ukiacha yale matukio machache yanayojitokeza. Ushwari huu unatokana na zile oparesheni tunazofanya mara kwa mara. Nawashukuru Raia wanaotupa habari na kuweza kuwadhibiti waharifu. Takwimu zinaonesha kuwa matukio yamepungua.Ukilinganisha na Januari mpaka Oktoba mwaka jana, Hii yote ni kutokana na ushirikiano tunaopata kutoka kwa Raia wema.

Oparesheni ambazo tumefanya kuanzia Machi mpaka tulipofikia

Wizi wa Magari - Tumekuwa tukifanya opesheni nchi nzima, kuanzia Machi mpaka oktoba tumeweza kukamata magari 42. Haya magari nimesema yakusanywe yote mikoani na kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya utambuzi. Nichukue nafasi hii kuwaalika walioibiwa magari kuja Dar kwa ajili ya utambuzi.

Ujambazi - Kwa hali ya sasa ujambazi Tanzania umepungua. Tulikuwa na oparesheni ya kukusanya silaha kwa wakati na tumeweza kukusanya silaha 190. Tumekamata AK47 - 10, Shortgun - 23, bastola 14, risasi takribani Risasi 235 za aina mbalimbali - Hii yote ni kwasababu ya operesheni tunazofanya na ushirikiano tunaopata kutoka kwa raia.

Usalama wa Raia - Wenyeviti washiriki katika ulinzi wa raia. Zoezi la vikundi vya ulinzi shirikishi ni la msingi na lazima tushirikane kuhakikisha mitaa yetu inakuwa shwari.

Waharifu kukimbilia nchi jirani - Miezi ya nyuma kulikuwa na shida Kibiti, Ikwiri Lindi na kuelekea Mtwara.Tuliweza kuwadhibiti na wengine walikufa katika mapambano na wale waliosalia wanakimbilia Msumbiji. Wasifikiri kwamba kukimbilia Msumbiji watakuwa salama,tuna ushirikiano mzuri sana na Msumbiji na mipaka yetu ipo salama.


Kutekwa Mo Dewji
Kwa hilo tukio, eneo la tukio kuna CCTV Camera, baada ya tukio tuliokota risasi mbili za Pistol, tulienda kufanya uchunguzi kwenye maabara zetu za Polisi, Forensic. Tuliweza kulitambua gari. Tumefuatilia CCTV Camera na tulibaini kwamba baada ya gari kutoka Colosseum liliingia kwenye barabara ya Ally Hassan Mwinyi kuelekea 'round about' ya kwenda Kawe , tunafuatilia kama walienda Silver au Kawe.

Kikubwa tumepata taarifa kuwa gari limetokea nchi jirani. Tumefualia mpakani na tumebaini kweli gari kama hili lilipita mpakani tarehe 1 September 2018. Tumewasiliana na Interpol na nchi jirani ili tuweze kubaini gari linamilikiwa na nani.Tumepata details za kutosha, nani mwenye gari nchi anayotoka imefahamika, watu wetu wa Interpol wanafanyia kazi

Tusidharau vitisho, mtu unapoona unatishiwa na mtu yeyote, tupe taarifa, ili tuweze kufanyia kazi mapema. Na pia wale wenye uwezo kifedha ni vyema wakawa na silaha na wasaidizi wenye silaha, kwa sababu fedha walizonazo kila mtu anazitaka. Mo anamiliki silaha lakini siku hiyo hakuwa na silaha, ana dereva lakini siku hiyo aliendesha gari mwenyewe.Kuna vitu unaweza viachia sababu ukijua nchi yetu ni shwari halafu watu wabaya wakachukua hiyo nafasi

Kingine tupeane taarifa za ukweli, kuna watu wanapotosha kwa kutoa taarifa za uongo polisi, wanasema Mo yuko huku.. ukienda unatumia askari,magari na mbwa lakini ukifika hukuti kitu, mtu huyu tumemweka ndani.

Picha za gari nitawapa muweze kuzisambaza, gari lenyewe ni aina ya Toyota Surf yenye namba ya usajili AGX 404 MC

Hatuwezi kusema kama Mo yupo hai au la kwa sababu sisi sio watekaji. Na kufahamu sababu ya kutekwa kwa mfanyabishara huyo, hadi hapo tutakapompata yeye na watekaji.

Tunashirikiana vizuri na 'Interpol' bado hatujaona haja ya kuomba msaada wa Vyombo vya uchunguzi kutoka nje, kama tutaona kuna ulazima sisi tutamshauri Amiri Jeshi Mkuu, lakini mpaka sasa bado tuna imani na Vyombo vyetu vya ndani. Hili ndilo gari lililomteka Mo.

Mtakumbuka jeshi hili hili ndo limemaliza ujambazi sugu na mauaji ya kibiti mimi najua majeshi ya wengine naomba watanzania mtuamini sisi tupo vizuri na tutamaliza jambo hili.

Nataka niseme anayeharibu Amani ya nchi tutamgonga kwelikweli haiwezekani leo siku ya nane jambo moja linatuumiza tupeni taarifa"

Kuhusu utekaji mwingine IGP amesema > Kuna watu wengine huondoka majumbani mwao na kwenda shamba, au wanakwenda nchi nyingine wanaoa huko, lakini huku mnabaki mkisema ametekwa. Sasa unajiuliza kuna silaha au nguvu ilitumika? mtu amemuaga hadi mkewe, huyo ametekwa?
CCTV-camera-ya-Sirro.jpg
 
Karibu!
Up dated:
Kamanda Sirro amesema bado wanafuatilia picha za cctv na maendeleo ni mazuri. Namba za gari zimeshafahamika na gari hilo limetokea nchi ya jirani.
Interpol inafuatilia pia kubaini uelekeo wa gari.
Imebainika gari laina hiyo lilionekana likiingia nchini pale mpakani likitokea nchi jirani.
Kamanda Sirro amesema kwa sasa wanashirikiana kwa karibu na Interpol na kama itatokea ulazima wa kuomba msaada nje wataomba kibali kwa amiri jeshi mkuu. Hata hivyo Sirro amewahakikishia wananchi kuwa jeshi letu ni imara na linaimudu hii changamoto na ametolea mfano vurugu za Kibitji na jeshi limezizima bila msaada wa nje.
 
Ujambazi umepungua - Tumekusanya silaha 190, katika silaha AK47 - 10, Shortgun -Risasi 235 - Hii yote ni kwasababu ya operesheni tunazofanya na ushirikiano tunaopata kutoka kwa rais
Kwenye ujambazi si kweli nasikia kigoma huko haswa kibondo hili tatizo lipo kwenye kiwango cha juu, watu wanavamia mchana kweupe na join join halafu wanaibia hadi watu wa pikipiki na wanakua na silaha za moto.
 
Kwa ujumla hali ya nchi yetu ni shwari ukiacha yale matukio machache yanayojitokeza. Nawashukuru Raia wanaotupa habari na kuweza kuwadhibiti waharifu. Takwimu zinaonesha kuwa matukio yamepungua. Hii yote ni kutokana na ushirikiano tunaopata kutoka kwa Raia wema.

Wizi wa Magari -

Ujambazi - Kwa hali ya sasa ujambazi umepungua. Tumekusanya silaha 190, katika silaha AK47 - 10, Shortgun -Risasi 235 - Hii yote ni kwasababu ya operesheni tunazofanya na ushirikiano tunaopata kutoka kwa raia.

Usalama wa Raia - Wenyeviti washiriki katika ulinzi wa raia. Zoezi la vikundi vya ulinzi shirikishi ni la msingi sana mitaani.

Watu kukimbilia nchi jirani - Kuna waharifu walikuwa wanafanya uharifu Kibiti.Tuliweza kuwadhibiti na wengine walikufa katika mapambano na wale waliosalia wanakimbilia Msumbiji. Wasifikiri kwamba kukimbilia Msumbiji watakuwa salama,tuna ushirikiano mzuri sana na Msumbiji na mipaka yetu ipo salama.

Tukio la kutekwa Mo Dewji; Kwa hilo tukio kuna CCTV Camera, baada ya tukio tuliokota risasi mbili za pistol, tulienda kufanya uchunguzi kwenye maabara zetu za forencic. Gari tumelitambua, tumefuatilia cctv camera Ally Hassan Mwinyi kuelekea kawe, tunafuatilia kama walienda Silver au Kawe.

Kikubwa tumepata taarifa gari limetokea nchi jirani. Tumefualia kmpakani na tumebaini kwenli gari kama hili lilipita mpakani tarehe 1 september 2018. Tumewasiliana na Interpol na nchi jirani ili tuweze kubaini gari linamilikiwa na nani.

Nawaomba wenye uwezo wawe wanachukua tahadhari kwa kujilinda. Mo anamiliki silaha lakini siku hiyo hakuwa na silaha.

Kingine tupeane taarifa za ukweli, kuna watu wanapotosha kwa kutoa taarifa za uongo polisi, wanasema Mo yuko huku.. ukienda unatumia askari,magari na mbwa lakini ukifika hukuti kitu, mtu huyu tumemweka ndani.

Picha za gari nitawapa muweze kuzisambaza, gari lenyewe ni aina ya Toyota Surf.
Mbona ametoa maelezo ya kawaida sana. Haya ngoja tusubiri tuone kitakachofuata.
 
Inasikitisha sana IGP Kuwasumbua Waandishi wa habari kwa press ya Kipuuzi kama hiyo.....Iweje IGP mzima hajui muda upi ni sahihi kwa Kuitisha press? Anaitisha press na kuanza kuleta mipasho badala ya kutuletea taarifa za kupatikana kwa MO au hatua madhubuti iwapo bado hajapatikana!.
 
Back
Top Bottom