Haya ni maoni yako mkuu....sisi tunasubiri uamuzi wa mahakama
sote tunasubiria mahakama itende haki.
maana watanzania wapenda amani kamwe hatuko tayari kuona mtu yeyote au kikundi cha watu kwa uchu wake/wao na tamaa ya kutafuta madaraka anahatarisha Amani yetu.
 
sote tunasubiria mahakama itende haki.
maana watanzania wapenda amani kamwe hatuko tayari kuona mtu yeyote au kikundi cha watu kwa uchu wake/wao na tamaa ya kutafuta madaraka anahatarisha Amani yetu.
Mbona umeshamuhukumu?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
IGP alieleza wazi tangu mwanzo kuwa Mbowe si malaika na kwamba ushahidi upo wa kutosha juu ya ushiriki wake kwenye ugaidi.

Tunayoyaona na kusikia mahakamani yanathibitisha ukweli kuwa kila binadamu ana siri kubwa moyoni mwake. Kamwe usisema fulani siyo au fulani hawezi kufanya hili wala lile. Yaliyo moyoni mwake ni giza tororo na ni siri yake.

Ushahidi unaotolewa kila kukicha kuthibitisha jinsi Mbowe alivyoshiriki kwenye njama za kufanya ugaidi zinatuacha midomo wazi. Ni aibu kwa waliofikiri Mbowe ni malaika. Muhimu ni kuiacha mchakato wa mahakama uendelee hadi mwisho na mbivu zitajulikana. Kwa ushahidi tunaoona, hatutashangaa tukisikia mtu anakula miaka 30 jela.
 
Wewe unasema ushahidi unaotolewa mahakamani, kuwa unadhihirisha ushiriki wa Mbowe kwenye ugaidi?

Hivi unafikiri atatiwa hatiani kwa ushahidi huo wa michongo wa huyo Askari wako Urio?

Ngoja uone atakavyopigwa maswali na Kibatala, ndiyo utaona huyo shahidi wako atavyoumbuka huyo Urio wako na ushahidi wake wa uongo!
 
Elimu Elimu Elimu Elimu.Siwezi kukulaumu kwakuwa Elimu yako mpaka leo imeshindwa kukukomboa.

Luteni Urio kathibitisha mwenyewe tena pasipo shaka kwamba hakuna ugaidi na kesi yenyewe imejengwa katika misingi ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom