View attachment 1877322
IGP Simon Sirro leo Agosti 2, 2021 akizungumza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe


IGP Simon Sirro leo Agost 2,2021 amefanya mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza mbalimbali kuhusu kukamatwa na Mwenyekiti wa Chadema pamoja na vuguvugu la kutaka kufanya maandamano. Akiwa katika mkutano huo SIrro alisema yafuatayo:

“CHADEMA wanaona Mwenyekiti wao (Mbowe) ameonewa na wanasema hawezi kuwa hivyo wanamuona ni Malaika hawezi kufanya kosa”

“Kabla ya Uchaguzi nilisema kuna Watu wamepanga kuhakikisha Uchaguzi haufanyiki, nilisema kuna baadhi ya Watu wamepanga kulipua visima vya mafuta na kufanya mauaji ya Viongozi na nilisema tutawakamata kabla hawajafanya hivyo”

“Tuliwakamata kabla, hayo ya Mwenyekiti wao (Mbowe) sitaki kuzungumzia sana lipo Mahakama ila wajue yeye ni Binadamu kama Binadamu wengine na anaweza kufanya kosa tumempeleka Mahakamani tuache Mahakama itimize wajibu wake”

“Kama kweli ni mkweli Mwenyekiti wao (Mbowe) na anamuamini Mungu waende wamuulize habari hiyo, kuna mambo unaweza kuyafanya kwamba ni siri lakini ndio mana Vyombo vya Habari vipo, niwaombe Watanzania wenzangu usilolijua ni kama usiku wa giza usiingie kwenye mtego ambao hujui aliyeutega ana jambo gani”

“Waende wamuulize huyo Mtu tuliyempeleka Mahakamani (Mbowe) kwamba hili jambo unalijua na kama ni ukweli ana Dini yake na anamjua Yesu Kristo aende aaambiwe, tunamuonea kwa lipi ?, tupate nini?, tuna ushahidi wa kutosha tuache Mahakama iamue, kafanya Yes hakufanya Yes lakini habari ya kikundi cha Watu kusema tunataka kuandamana wewe ni nani Bro!? hiyo nafasi hauna”

Awaonya Wanaotaka kuandamana
“Niwaombe Watanzania tuache wale Watu wachache ambao wanataka kupambana na Serikali wapambane nayo labda wana sababu zake lakini Mtu wenye hekima na busara anielewe, lakini kikubwa kama wameandaa kwenda Canada au Marekani wajiandae ila hatuwezi kuruhusu Watu wachache wavuruge Nchi kwasababu wamekosa madaraka”

“Habari ya kusema mnataka kuandamana mnavunja sheria na ukivunja sheria usilaumu Jeshi, ukivunja sheria umeingia kwenye uhalifu, Sirro hatokuacha na Polisi hawatokuacha na ndio maana wanafanya siasa kwa sababu amani na utulivu upo, Sisi hatufanyi Siasa”

“Niwaombe Watanzania ambao wameambiwa mkusanyike kutoka Mara kutoka wapi sijui na muelewe Mahakamana ni kituo nyeti ni kama Kituo cha Polisi ukitaka kuvamia utakung’utwa kwa mujibu wa sheria sababu umetaka sasa kama kuna Mtu maisha yamemshinda aje ila asije kulalamika, hii kesi iko Mahakamani tuiachie Mahakama iamue”
Watu walimdharau sana Mama.., sasa kuna wakati sauti ya mamlaka inatakiwa isikike na asiwepo mwenye kufanya fyoko..!
 
Yaani mbona unakuwa biased Sana mkuu. Unadhani ni wangapi wanaosota mahabusu ama wanasingiziwa kesi wakafungwa.
Mbona huwaongelei ama unaona binadamu ni mmoja tu jamani hapa tz.
Usikute hata Kuna ndugu ,rafiki wako wa karibu anasota Ila hujamuongelea Ila huyu .inaonekana labda Kuna kitu alikuwa anakufanya Ila umemisi saivi
CCM hamuwezi kujenga hoja, bali mnajenga matumbo tu.
Wajinga nyie.
 
Hizi kauli zilikuja maalum ili kuwaandaa watu kisaikllojia Mbowe aonekane ana hatia tayari, haya maneno ya Sirro hayakuwa bahati mbaya, alishapangwa.
 
Sirro ufahamu kuwa sisi kama watu wenye akili zetu:

1. Tunajua kuwa mwenyekiti Mbowe mmembambikizia kesi
2. Tuko kwenye nafasi za kujua mnambambikizia kesi
3. Tunajua ni haki yetu kuja mahakamani...
Hao mamilion wa kuwekwa gerezani mko wapi Hadi leo?
Nyumbu hovyo kabisa.
 
Hao mamilion wa kuwekwa gerezani mko wapi Hadi leo?
Nyumbu hovyo kabisa.

Kwani mwisho wa safari ulishafika? Au ratiba zetu unazo wewe? Yaonekana una maumivu makali sana:

IMG_20210829_032751_977.jpg


Unadhani jaji Mutungi na miito yake kumuasa Sirro ni kwa sababu hatusomi tulipofika?

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Kwamba unakereka mno kwa sababu:

1. Tunajua kuwa mwenyekiti Mbowe mmembambikizia kesi
2. Tuko kwenye nafasi za kujua mnambambikizia kesi
3. Tunajua ni haki yetu kuja mahakamani
4. Tunakutaka ujue tutakuwapo mahakamani wala usitutishe
5. Tunakutaka umwogope Mungu wako kwani kushuhudia uongo huku ukilitaja jina lake bure, Mola anakataza
6. Tunakutaka uwashauri wenzio mtafute magereza zaidi ya kutuweka katika mamilioni yetu
7. Tunakutaka uziheshimu haki zetu

8. Tunakutaka uheshimu katiba

Jiandae kuteseka zaidi kwa sonona.

Tulizana mburula wewe mnufaika wa udhulumati wa haki, usawa na uhuru wa watu ambao siku zake zinahesabika. Si mbaya mkijua tuko njiani wala hatuko mbali.

Ukiukwaji Katiba, Tanzania tunafeli Wapi?

Apumzike kwa amani Brigedia Chefe Ali.

Habari ndiyo hiyo.
 
Tumeona mambo yalivyo, kwani Mahakama imetoa amri ya kwenda kubadilishwa kwa hati ya mashitaka. Kama hati imeonekana ina ubatili, jiulize huo ushahidi utakuaje?
 
Serikali ya CCM ilishamfutia dhamana na akakaa gerezani akiwa na Matiko zaidi ya siku 100 kama kibaka anayeweza kutoroka.
Wakamhukumu na wezake jela au faini ya mamilioni ya shilingi na jela wakakimbilia kumnyoa kipara kufurahisha roho zao.
Wakamvurugia biashara zake na mashamba wakang'oa huku wakifunga bank accounts zake.

Sasa wamekuja na kubwa kuliko kuwa ni gaidi na ana fadhili ugaidi kwa shilingi laki sita au dola za kimarekani $230.
Uonevu wote huu wanaomtendea Mbowe ni kwa sababu gani hasa?

Jee ni kwa vile wafuasi wake ni wapole au yeye ndio mpole?

Maana nina hakika Mbowe akikasirika na kuonyesha hasira, wafuasi wake wanaweza kubadili mwelekeo wa siasa zetu na kuchukua mrengo mwingine kabisa.

Hali hii mpaka lini?

HAPPY BIRTHDAY KAMANDA FREEMAN

20210914_124914.jpg
chadema_in_blood-___CTokkpzrVUV___-.jpg
 
Wanabadilishana tu aina ya uonevu
  • kipindi Cha JK , walimpiga na kumpa kesi
  • Kipindi Cha jiwe, wakambomolea club yake
  • kipindi Cha hangaya, wanampa kesi ya ugaidi
Siku akija kuwa raisi, ni lazima kisasi kilipwe. Kuanzia waliohusika enzi za Jk, jiwe hadi huyu hangaya
 
Umasikini ni tatizo, nchi ingekuwa tajiri tusingeona yote haya, ukiwa masikini unaona kila mtu anakuroga kumbe ni ujuha wako mwenyewe.
 
Huu usemi wa kwamba ukimkimbiza sana Mjusi anageuka kuwa nyoka kama ni kweli....basi kuna kitu kitatokea si mbali sana...
 
Anaisumbua sana Seri_kali, wacha akae ndani kwnza tupumue pumue lah !! Corona yumo, Katiba mpya yumo aisee hapana. wacha tumuweke stoo kwa muda kidogo.
 
Na yeye ajifunze aache kujifanya mbabe, alimuona Mama ni dhaifu kama ambavyo alimuona JK akaanza chokochoko kama kawaida yake
 
Huyu jamaa nisichompenda ni kufuata umagharibi sana. Alipendekeza nchi iwekwe lockdown kipindi cha jiwe, alipendekeza chanjo ya lazima kwa wananchi wote kipindi cha Chief Hangaya.
 
Back
Top Bottom