chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,376
- 24,928
IGP Sirro amewaita makamanda wa polisi wa mikoa yote kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kikao maalumu ambacho kitafanyika kesho kuanzia saa moja na nusu asubuhi.
“Nimewaita makamanda wote wa mikoa waje Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza nao…siwezi kusema nini tutauzungumza maana hayo ni mambo yetu ya ndani,” alisema IGP Sirro.
Kwa mara ya kwanza IGP Sirro amewaagiza makamanda wapande magari kwa kanda, badala ya kila kamanda kutumia gari lake ili kubana matumizi.
“Kwa mara kwanza afande IGP ameagiza makamanda waje kwa kupitia kutokana na ukaribu wa mikoa au kanda ili kupunguza gharama za matumizi ya mafuta na na malipo ya maderava (allowance),” alisema ofisa mmoja wa jeshi hilo.
Chanzo: Muungwana Blog