IGP Sirro anasema hawezi kumkamata Askofu Gwajima mpaka apate barua. Je, hivi ndivyo anafanya kwa makundi yote?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Hayupo ambaye hajavishuhudia vimbwanga vya askofu Gwajima kuhusiana na Corona na Chanjo zake.

Hadharani tuhuma za Gwajima kumhusu mheshimiwa Rais na wasaidizi wake zimesikika.



Haya yakiendelea ni kweli kuna Watanzania wasio na hatia wanaendelea kuwekwa hatarini kuhusiana na ugonjwa huu.

Sirro anasema hawezi kumkamata Gwajima kwamba yeye hayo anayasikia mitandaoni tu. Kwamba yeye hadi apate makaratasi rasmi na ajiridhishe kama kuna jinai imetendeka.

Hivi ndivyo Sirro anavyofanya kazi kwa makundi yote? Au ndiyo ile sote hatuko sawa mbele ya sheria?

Kwa msimamo wa Sirro na Dkt. Gwajima, mafahali wawili hawa, pana japo mmoja ambaye basi hafai kabisa.

Itapendeza basi mtu akiwajibika au kuwajibishwa japo kwa kadhia hii.
 
Sirro ana dharau sana, mi naona tatizo linaanzia kule juu, bora katiba ibadilishwe Rais akifia madarakani nchi irud kwenye uchaguzi

Mtu anatuhumu Viongozi wamepewa hongo kuingiza chanjo means alikua anamaanisha Rais Samia bado ameachwa?

kipindi kile mtu yyte alikua hata akikohoa tu kuhusu JPM anakamatwa, Idris alicheka tu picha ya JPM akakamatwa

lakini Gwajima analiambia kanisa viongozi walioruhusu chanjo akili zao zimeenda kikizo halafu IGP anaongea nini sasa,

mi naona sasa kama vya chanjo tuachane navyo kwanzia leo maana ni kama vile hata Rais hatuna
 
Hayupo ambaye hajavishuhudia vimbwanga vya askofu Gwajima kuhusiana na Corona na Chanjo zake.

Hadharani tuhuma za Gwajima kumhusu mheshimiwa Rais na wasaidizi wake zimesikika...
Askofu Gwajima hana kosa lolote
 
Sirro anadharau sana, mi naona tatizo linaanzia kule juu, bora katiba ibadilishwe Rais akifia madarakani nchi irud kwenye uchaguzi

Mtu anatuhumu Viongozi wamepewa hongo kuingiza chanjo means alikua anamaanisha Rais Samia bado ameachwa?..
Nina mashaka hata Hili la kumkamata Mbowe pengine Kuna kakikundi kanataka kumfitinisha Samia na Wananchi na Sirro huenda akawa anakatumikia hako kakikundi
 
Sirro anadharau sana, mi naona tatizo linaanzia kule juu, bora katiba ibadilishwe Rais akifia madarakani nchi irud kwenye uchaguzi
Tumeshudia watu wakisukumwa ndani na wakuu wa mikoa, mawaziri, ma DC nk papo kwa papo kwenye mikutano ya hadhara.

Mikutano ya wah. Mwanri, Jaffo, Ummy, Majaliwa, Awesu, Katambi, nk ni mifano mizuri ambapo watu wamekamatwa kinyume na utaratibu anaouongelea Sirro leo.

Sirro ni tatizo.

Sirro must go!
 
Askofu Gwajima hana kosa lolote

Makosa ya Askofu Gwajima ni wazi:

1. Hadharani amewatuhumu Rais na wasaidizi wake kwa rushwa.
2. Hadharani amehamasisha watu dhidi ya serikali.
3. Kwenye #2 hapo amekuwa akitumia maneno ya dharau, kejeli, kuudhi, dhidi ya Mh. Rais na serikali.

Haya yote ni makosa kisheria kwani kwa kila moja upo ushahidi wa watu walikwisha kukamatwa, kushitakiwa na hata kuhukumiwa.
 
Askofu Gwajima hana kosa lolote
Askofu ana kosa kutoa tuhuma hadharani ambayo ingefaa angeithibitisha...Tusitete uovu...Kwenye chanjo hana kosa kwakua ni opinion yake na kama wale wanaoi promote wanaruhusiwa wenye doubts kwanini wasipewe haki ya kuuliza?
 
Hayupo ambaye hajavishuhudia vimbwanga vya askofu Gwajima kuhusiana na Corona na Chanjo zake.

Hadharani tuhuma za Gwajima kumhusu mheshimiwa Rais na wasaidizi wake zimesikika...
Huu ni ushahidi mwingine kuwa Sukuma Gang inalitumia jeshi la Polisi kumhujumu Rais Samia
 
Hata wakimfukuza CCM,Gwaji has nothing to lose!

Ana pesa na platform hata kabla ya huo ubunge na ataendelea kuongea anachokiamini tena ndiyo atakuwa maarufu zaidi.

Hongera kwa IGP kwa kuukataa huu upuuzi wa majukwaani,taasis zote huwa zinatoa majibu hayo hayo ya Sirro kuhusu matamko ya wanasiasa majukwaani.
 
4) Kuzua taharuki kwa raia.
5) Kuhamasisha raia kukaidi na kuipinga serikali.
Ya tano ni siyokweli hiyo ya nne ni sawa ila pia ni contextual. Tuwe reasonable ili turudishe trust ya raia kwa serikali yao ambayo kusema ukweli imegeuka haraka mno na kwa muda mfupi kiasi ambacho ilitakiwa ijue imewa confuse raia wake; inaweza ikawa hawakua na jinsi basi watu wapewe benefits of doubt
 
Hayupo ambaye hajavishuhudia vimbwanga vya askofu Gwajima kuhusiana na Corona na Chanjo zake.

Hadharani tuhuma za Gwajima kumhusu mheshimiwa Rais na wasaidizi wake zimesikika...
Sirro has rushed to dismiss dr Gwajima sentence mno

this is dangerous

mama Ana maamuzi ya kufanya
 
Hahahah dunia hadaa walimwengu shujaa leo chadema ndio wanaanda mashtaka dhidi ya Gwajima.
brazaj Corona lazima ipote na wewe
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Similar Discussions

Back
Top Bottom