IGP Sirro amshukuru Rais Samia kwa kuwapatia tsh 1.4 bilioni za ujenzi wa madarasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
50,860
2,000
IGP Simon Sirro amemshukuru Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kiasi cha tsh 1.4 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.

IGP Sirro amesema kwa sasa ujenzi unasuasua kidogo baada ya fedha hizo kuingizwa katika akaunti ya Amana wakati wa kufunga mwaka wa fedha na ameahidi kulifuatilia swala hilo Hazina.

=====

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI (CPF) AKAGUA MIRADI YA UJENZI YA JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM.

Dar e salaam 9 Novemba 2021
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (Chief of Police Force) IGP Simon Nyakoro Sirro tarehe 08/11/2021 amefanya ukaguzi katika miradi ya ujenzi wa Madarasa na mabweni katika chuo cha Maofisa wa Polisi Dar es salaam (DPA).

Afande CPF amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyolisaidia Jeshi la Polisi, ambapo alitoa kiasi cha Tsh 1.4 bilioni kuwezesha ujenzi wa madarasa na mabweni katika chuo cha maofisa wa Polisi Dar es salaam kilichopo Kurasini.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameridhishwa na maendeleo ya Ujenzi huo, lakini amebaini kuwepo kwa changamoto ya kukwama kwa fedha kutoka hazina kutokana na kubadilika kwa mwaka wa fedha wa serikali ambapo fedha za mradi zilihamishiwa katika akaunti ya amana ambayo ilikuwa imefungwa.

Kwa upande wake Mhandisi wa Jeshi la Polisi ACP Fadhil Ishekazoba amesema walishaanza ufuatiliaji ili waweze kupatiwa fedha hizo.

Aidha afande CPF amemuhakikishia mkuu wa chuo cha maofisa wa polisi Dar es salaam SACP Lazaro Mambosasa kuwa atashughulikia changamoto zote haraka iwekezananyo ili mradi huo ukamilike kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini amekagua ujenzi wa Kituo cha Polisi wilaya ya Kigamboni eneo la Gezaulole ambapo ujezi wake umefikia asilimia 30, na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami katika hospitali kuu ya polisi kilwa road ambapo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.

Imetolewa na;
Dawati la Habari Kanda Maalum ya Polisi Dar es salaam Dar es salaam.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,334
2,000
Madarasa ya kusomea PGO au ya amemshukuru ujenzi wa madarasa ya shule hizi za kawaida?
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,546

Tuombe Mungu hayo madarasa yazalishe Polisi wenye weledi na wanaotenda haki, Mungu aepushe kupelekwa wale watakaotumika kuangamiza nchi na kubambikiza kesi au meno ya tembo.
Watakaosoma ndani ya hayo madarasa wajitambue wao ni raia na uraiani watarudi kama raia. Wasipate laana za wake wanaostaafu wakawa makorokoroni huku mitaani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom