IGP Sirro amkubali RPC Shanna, apandisha hadhi kituo cha Polisi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP ,Simon Sirro ,amempongeza kamanda wa polisi Mkoani Arusha,(RPC)Jonathan Shanna kwa kudhibiti matukio ya uhalifu ambayo kwa kiasi kikubwa yamepungua mkoani hapa.

Aidha IGP Sirro amemwagiza RPC Shanna kushughulikia kero ya Mauaji ya wanawake katika kata ya Olasiti na Muriet ,ambapo wananchi walimweleza mkuu huyo wa polisi juu ya kero hiyo wakati akizungumza nao katika zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kwa nyumba sita za kisasa za polisi zinazojengwa na wadau wa jeshi hilo katika eneo la feed force ,kwa Morombo jijini Arusha.

Sirro kabla ya kuwahutubia wananchi hao ,aliruhusu maswali kwa wananchi ,ndipo mwànanchi mmoja mkazi wa eneo hilo alipotoa kero hiyo na kuungwa mkono na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alisema kuwa wanawake wapatao nane waliuawa na watu wasiojulikana akiwemo mke wa aliyekuwa diwani wa kata ya Muriet Credo Kifupe.

Licha ya IGP Sirro kukerwa na mauaji hayo alimpongeza kamanda Shanna kwa umahiri wake katika kushughulikia masuala ya uhalifu na wahalifu jambo lililopelekea mkoa wa Arusha kupungua kwa kiasi kikubwa matukio ya uhalifu.

Katika hatua nyingine Sirro amekipandisha hadhi kituo kidogo cha polisi cha Muriet kuwa kituo cha wilaya kitakachokuwa na askari wengi zaidi na kuhudumia eneo hilo na maeneo jirani ya kata ya Muriet.

IMG_20200304_161902.jpeg
IMG_20200304_153638.jpeg
IMG_20200304_162031.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom