kiben10
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 616
- 789
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amwsema moja ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo ni unafiki miongoni mwa askari wake. Sirro ameongea hayo leo Jumanne September 24, mwaka 2019 katika kikao kazi cha maafisa waandamizi wa jeshi hilo ambapo ameonekana kuwajibu Maafisa wa polisi wanaosema hatoshi katika nafasi hiyo.
"Tatizo linalotusumbua sisi Jeshi la Polisi pia ni unafiki. There is no way tukawa na IGP zaidi ya mmoja. Mimi sikujichagua. Kamanda wa polisi Kinondoni (Mussa Taibu) unanisikia? Kubali yaishe. Mimi sikujiteua mwenyewe, kwahiyo siwezi kujiona kama sitoshi katika nafasi hii. Aliyeniteua ndiye anaweza kuona kama natosha au sitoshi” amesema IGP Sirro.
Akijibu tuhuma hizo, Kamanda wa polisi Kinondoni ACP Mussa Taibu amesema IGP Sirro amemtaja yeye kama mfano lakini ujumbe huo haumhusu yeye. "Hiyo nondo ya IGP imepigwa mahususi kwa baadhi ya watu. Mimi nimetajwa tu kufikisha ujumbe"
Na case study yetu ni matukio ya Akwilina na Mwangosi, changamoto kubwa ambayo hujitokeza ni command (amri) inapokuwa weak (dhaifu) haya hutokea. Kilichotokea Kinondoni siwezi kusema lakini mnaweza kuwa mashuhuda, kuna mahali kama Jeshi la Polisi hatukutimiza wajibu wetu"
Zaidi soma...
Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema kulingana na amri za jeshi hilo, askari atakayejihusisha na siasa lazima wenzake watamshangaa.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Septemba 24, 2019 katika ufunguzi wa kikao cha siku tatu cha maofisa waandamizi wa polisi kinachofanyika jijini Dar es Salaam ambako ameeleza masuala mbalimbali yanayolikabili jeshi hilo, likiwemo la kujihusisha na siasa.
“Changamoto nyingine ni baadhi yetu kujihusisha na siasa, katiba iko wazi na police general order (kanuni za polisi) iko very clear (wazi kabisa) wala sio sifa, sisi Polisi wenzako tunakushangaa hata umma utakushangaa.”
“Watu wanataka kusikia unasema nini, wewe sio mwanasiasa unajiaibisha mwenyewe, tujikite kwenye majukumu yetu hayo unayofanya umeyatoa wapi,” amehoji Sirro.
Ameongeza, “Halafu unafanya hivyo kwa sababu uko kwenye nafasi hiyo tukikutoa hapo utaweza kufanyia nyumbani kwako? Si Pahala pa kufurahisha watu, wengine wanafanya vitu kutafuta umaarufu wa kisiasa tu, unamfurahisha nani?”