Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Bado naendelea kushtushwa na kitendo cha IGP kusema kua wana mpango wa kukagua mafunzo yalotolewayo na na taasisi za kidini humu nchini, watuambie kua Polisi huo ujuzi wameutoa wapi na wanaruhusiwa na sheria ipi kuingilia imani za watu?
Afande Sirro mzee wangu unataka kufika mbali sana, staafu kwa amani achana na haya mambo. Kwa hisia ni kwamba inachukuliwa kua walengwa ni watu wa imani flani, na wao wanachukulia kama una chuki binafsi na imani hiyo. Achana na mambo ya imani za watu kwenye taifa, watu wanafia imani zao na imeleta matatizo makubwa sana haihitaji kutolewa mifano.
Chukueni hatua kali kwa wanaokiuka sheria za nchi kwa mujibu wa sheria na siyo kuijivika kilemba na taaluma za kukagua mafunzo ya imani za watu. Sheria za nchi zipo mnahangaiaka nini?
Muda si mrefu viongozi wa taasisi za kiislam nchini watatoa msimamo wao na inaonesha kua wamefedheheshwa na uamuzi wako IGP. Wakikataa uamuzi wako usilazimishe maana matokeo hayatakua mazuri kama ufikiriavyo, usituletee mambo ya Rwanda,sisi tupo na amani yetu tangu uhuru. Kenya wenyewe ambao maeneo ya mwambao wa bahari nchini mwao kumejaa matishio ya kiusalama lakini hawana utaratibu huu.
Ni hayo tu Afande uwe na majukumu mema.