IGP Sirro achana na ukaguzi wa mafunzo ya kidini, staafu kwa fahari

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Bado naendelea kushtushwa na kitendo cha IGP kusema kua wana mpango wa kukagua mafunzo yalotolewayo na na taasisi za kidini humu nchini, watuambie kua Polisi huo ujuzi wameutoa wapi na wanaruhusiwa na sheria ipi kuingilia imani za watu?

Afande Sirro mzee wangu unataka kufika mbali sana, staafu kwa amani achana na haya mambo. Kwa hisia ni kwamba inachukuliwa kua walengwa ni watu wa imani flani, na wao wanachukulia kama una chuki binafsi na imani hiyo. Achana na mambo ya imani za watu kwenye taifa, watu wanafia imani zao na imeleta matatizo makubwa sana haihitaji kutolewa mifano.

Chukueni hatua kali kwa wanaokiuka sheria za nchi kwa mujibu wa sheria na siyo kuijivika kilemba na taaluma za kukagua mafunzo ya imani za watu. Sheria za nchi zipo mnahangaiaka nini?

Muda si mrefu viongozi wa taasisi za kiislam nchini watatoa msimamo wao na inaonesha kua wamefedheheshwa na uamuzi wako IGP. Wakikataa uamuzi wako usilazimishe maana matokeo hayatakua mazuri kama ufikiriavyo, usituletee mambo ya Rwanda,sisi tupo na amani yetu tangu uhuru. Kenya wenyewe ambao maeneo ya mwambao wa bahari nchini mwao kumejaa matishio ya kiusalama lakini hawana utaratibu huu.

Ni hayo tu Afande uwe na majukumu mema.
 
Si alienda kujifunza kwa kagame jamani ama! bado sheria ya wachungaji na mashehe kuwa na digrii inakuja , hatutaki kabisa ujinga sisi, lazima watu wasomeshwe tena chini ya uangalizi wa polisi
 
mnaohangaika na hii isue achaneni nayomtu wala hamtajuwa kuwa tayari mmeshaanza kuchunguzwa hawatakuja na magwanda humo watakuwa kama wenzenu tu
 
Anafuatilia mafunzo ya taasisi nyingine, huku yeye na askari wake hawafahamu hata PGO yao ikoje!?
kwani kuna shda gan ka akichunguza?? au kuna madudu gani huko mbona mmekuwa wakali sana kuchunguzwa?
 
kwa ufahari upi wakati vijana wake pamoja na yeye mwenyewe wanafanya kazi kiholela bila kufuata order zao za kipolice kitu ambacho ni finyu mno kwa upatikanaji wa HAKI wa mtuhumiwa aliyeko mikononi mwa jeshi hili kabla ya kufikishwa mahakamani.

Haki ya mtuhumiwa inaanzia pale anapokamatwa hadi pale anapofikishwa mahakamani - kama hufuati hapa aisee mfumo wa Haki wa mtuhumiwa ndani ya jeshi ni mdogo ama haupo kabisa.

Kesi hii ya Mbowe itatusaidia kujua mengi yanayofanyika gizani. Mungu ni mwema wakati wote.
 
Unachunguzwa na mtu asiyejua muongozo wa kazi yake? Mla rushwa atachunguza nini? Kwa huu udhaifu unaofanywa na polisi, wao watachunguzwa na nani? Au tuteue viongozi wa dini nao wakawachunguze polisi?
Un
wani kuna shda gan ka akichunguza?? au kuna madudu gani huko mbona mmekuwa wakali sana kuchunguzwa?
 
Mimi ni Mkristo, lakini huu mchezo wa kuanza kuingiliana kwenye mambo ya imani za watu yatatuweka pabaya sana. To be honest hata akijifanya kuwa ukaguzi huo ni kwa dini zote, lakini targets hapa ni Islamic faith. Sioni kama hili jambo ni afya kwa umoja na usalama wa nchi
 
Mafunzo yafanyike kwa askari wote kuzijua na kuzitekeleza PGOs. Nimezisoma kidogo mwanzoni, zikitumiwa na polisi kweli jeshi letu litakuwa POLICE SERVICE na si POLICE FORCE
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom