IGP Sirro aagizwa kuchunguza wahitimu wa polisi wanaotaka kupangiwa utrafiki na bandarini

Hili hata mtoto wangu aliyefaulu Mtihani wa Chekekechea kiingia Grade One anaweza toa jibu bila uchunguzi!
 
Mbona Majibu yako wazi kwamba ni rushwa, posho na magendo, sasa unataka sirro afanye uchunguzi gani wakati kila kitu kiko wazi kila palipo na ulaji ndo watu wengi huwa wanapenda kufanyia kazi hilo eneo, hizo ela za kufanyia uchunguzi bora zifanye kazi nyingine, bandarin na traffic ndo kuna hela kila siku mtu anaondoka na around 20000 hadi 30000 kwa mwezi ni laki 6 hadi 9 nje ya mshahara wake then unategemea asiombe huko ????
 
Ukitafakari kwa kina hoja ilikuwa kuhamasiaha wananchi kutumia barabara kwa usalama na kujali watumiaji wengine wa barabara.

Sasa hii ya Askari wa usalama barabarani wanapatikanaje inafikirisha kidogo au Hawa Askari wamekuwa chanzo Cha matumizi mabaya ya barabara? Naamini wapo baadhi wanaomba rushwa Katika utendaji wao wa kazi za kila siku kama ilivyo Katika sekta nyingi za Serikali na Kuna wakati watumishi wa umma walipunguza kadhia hii ya rushwa swali hapa ni je,mtu mmoja aliweza kutamka au kuchimba mkwala nchi nzima wakaogopa?

Naungana na wanaotaka badala ya uchunguzi tufanye mambo mengine yenye manufaa kwa nchi maana sababu za Askari kupenda sehemu zenye unafuu wa kazi ni hulka ya kila binadamu Jambo muhimu ni kuweka wasimamizi wenye kutenda haki ambao kimsingi ni wachache sana.

Lakini kama kunadhamira ya kweli Katika uchunguzi basi waanzie juu kabisa wanaweza kubaini ugonjwa huu wa Kansa usio na tiba ulianzia wapi.

Niliwahi kusoma Mahali Askari wakilalamika kutokupangiwa KAZI kulingana na professional zao mfano muhasibu fani ya daktari na daktari anafanya uhasibu kama ni kweli hali itakuwa mbaya sana ndani ya jeshi Hilo na siyo tu kwenye eneo la usalama barabarani.

Ushauri tukitaka Askari watende haki tuanze kuwatendea haki kwanza wao na tusiwatumie kuvunja haki za wengine iwe ni kwenye uchaguzi au kwenye kazi zao za kila siku.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro pamoja na wakuu waandamizi wa polisi kuchunguza sababu za wahitimu wengi wa mafunzo ya polisi kuomba kupangiwa idara ya usalama barabarani na bandarini kama maeneo yao ya kazi na si maeneo mengine https://t.co/pksnTrZ9bqView attachment 2021292
Mwendazake aliwahalalishia trafiki rushwa kwa nini mtu asikimbilie huko?

Afu trafiki Kazi yao ni rahisi Sana ..Polisi itoe kozi ya jumla kwa askari polisi wote afu huko trafiki iwe ni rotational tuu.
 
Back
Top Bottom