IGP Simon Sirro nisaidie dhamana ya wadogo zangu Kituo cha Dakawa

nyakubonga

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
4,585
7,156
Sina hakika kama mkuu wa upelelezi wa kituo cha Dakawa ni binadamu wa kawaida

Leo nimefuatilia dhamana ya wadogo zangu ambao wameshikiliwa kituo cha Dakawa tangu jumatatu kwa kosa la kupigwa na vijana WA kimasai, naomba nieleweke vizuri 'kwa kosa la kupigwa na vijana wa kimasai'

Nimemkuta mkuu wa upelelezi nkamueleza lengo langu kwamba ni dhamana ya vijana hao, majibu aliyonipa ndio yamefanya niandike uzi huu

Anadai hawezi kuruhusu dhamana kwasababu mimi si mwenyeji wa hapa( ni kweli nimetoka moshi), ikabidi nitafute mtu anayeishi nyumba moja na hao vijana, akakubali kuwadhamini ila tumefika huyu mpelelezi akagoma tena, kwa utetezi wa kua huyu anayetaka kuwadhamini hajui wanakotoka hawa vijana (sijajua sheria ya dhamana inasemaje kuhusu hili)

Nilipojaribu kumfuata tena ili ikiwezekana nimuombe hata kwa machozi akanambia "usinisoglee utaniambukiza korona"

Amenisikitisha sana mpelelezi huyu, nimejihisi siko Tanzania kabisa na msaada wangu umebaki kwa afande Sirro tu

Najua IGP anaweza asione ujumbe huu ila Nina hakika vijana wake wapo humu, naombeni msaada kwani hawa vijana hawajafanya kosa lelote.
 
Wadogo zangu wana hali mbaya, angekua muwazi ningetoa chechote japo najua ni kosa kisheria
Huyo mpelelezi ana bei yake wamasai walishampatia (unaweza kuta wanamfugia ng’ombe kadhaa), na hiyo kitu hayo maeneo ni common.
 
Back
Top Bottom