IGP Simon Sirro azungumzia kuhusu Kibiti, kutekwa watoto na shambulio la Lissu na ofisi za IMMMA

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
IGP Simon Sirro amezungumza na waandishi wa habari juu ya usalama wa nchi na kusema hali ni shwari kiujumla.



Amezungumza juu ya mauaji ya Kibiti na kusema hali sasa ni tulivu na asilimia 90 ya wahalifu wameshakamatwa
Pia amezungumzia juu ya kauli ya Rais jana ya kuwakamata watu waliotajwa kwenye kashfa ya madini na kusema kuna watu wamekamatwa Manyara tayari
Pia amezungumzia suala la watoto kutekwa na kusema kwa sasa watoto wa watanzania wapo shwari

Amezungumzia suala la Tundu Lissu kupigwa risasi na kusema wametuma wapelelezi wao wazuri kwenda Dodoma na lazima watawakamata,ila itawezekana kama wananchi watawapa taarifa

Sirro amesema ameona video fulani Tundu Lissu akimtaja Sirro na Kipilimba lakini yafaa kujiuliza je aliripoti taarifa hii vyombo vya usalama? na kuongezea kwa sasa hivi sio bora kunyoosheana vidole na kusema Mbowe amefanya vyema kwa kusema hawezi kutuhumu taasisi yoyote kwa muda huu
Amesema wananchi wasidanganywe kwenye suala sima la siasa na kama hakuna amani siasa wala dini haiwezi kufanyika na mtu asitumie nafasi hii kusema polisi wanatumika vibaya

IGP pia amezungumzia tukio la ofisi za IMMA kupigwa bomu na kusema upelelezi unaendelea vizuri na mwishowa siku watakuja na mafanikio mazuri na matokeowatayaweka wazi

IGP anajibu maswali

kutumika kwa silaha nzito kama SMG kumshambulia Tundu Lissu kunaleta tasira gani?
Na eneo tukio lilipotokea ni eneo wanaloishi viongozi wa serikali, usalama ukoje?

Majibu: Silaha iliyotumika tundu Lissu ni SMG au SR,matukio mengi ya uhalalifu silaha hizi hutumika, zinaingizwa nchini na kutoka nchi jirani zenye vurugu, inatumika maeneo mengi nchini

Swali: Kwa nini kupigwa risasi Tundu Lissu kumetokea eneo ambalo viongozi wa serikali wanakaa, hii inaleta taswira gani?

Jibu: Matokeohaya hayatokei porini, hutokea sehemu ambayo sehemu watu wanakaa, mfano mhalifu akitaka kuiba gari ataenda sehemu ambayo magari yanahifadhiwa.
Tanzania sio kisiwa, haya matukiowanayaona nchi nyingine wanaiga na kuja kuyafanya huku pia.
Upelelezi juu ya kushambuliwa tundu Lissu hatuwezi kusema umefikia wapi kwa sababu ni mapema sana. Nimelizungumzia kwa kifupi sana ili lisitoe mwanya kwa wahusika kujua tunachofanya

Swali: Watuhumiwa waliotajwa jana kwenye ripoti ya madini kwa nini hawajaitwa kwa majina waje mmoja mmoja kwa DCI kama inavyofanyika wanaitwa kiujumla?

Jibu: Upelelezi una namna nyingi, iwe kwa jina moja moja au kwa ujumla haijalishi kikubwa ni wote waliotajwa wanaripoti, hata ambao hawajatwa kwenye ripoti ikigundulika wanahusika wataitwa pia

Swali: Kumekuwa na msuguano wa mara kwa mara katiya polisi na Tundu Lissu na kuna wahalifu walivaa nguo zinazoendana na sare za polisi walitakakulichafua jeshi hili mnalizungumziaje?

Jibu: Kinachofanya uhalifu sio uniform, kinachofanya uhalifu ni mtu, mara nyingi tumekamata watu wanaovaa nguo zinazofanana na polisi, cha msingi ni tumkamate yule aliyefanya tukio.

Tunamkamata kamata Tundu Lissu kutokana na matendo yake, kutokana na sheria ilivyo na akikamatwa anapelekwa mahakamani, hapo kuna tatizo gani?
Polisi tunatenda haki kwa raia yoyote na hatupo kwa ajili ya kumuonea mtu

Swali: Kuna umesema umewakamata huko Arusha kuhusiana na suala la madini, wangapi wamekamatwa na majina yao ni yepi?

Jibu: Kwa leo sitataja ni wangapi na haitanipendeza kutaja majina

Swali: Kuna watu waliojitokeza kwenye mitandao ya kijamii wakionyesha kufurahishwa na Tundu Lissu kushambuliwa na kijana mmoja anajulikana kwa jina la Suleiman na DC wa Kilombero kuna ujumbe wao unasambazwa kwenye mitandao, je mmechunguza hili na mmekamata hao watu?

Jibu: Jeshi la polisi linafuatilia, mambo mengine hatutarajii kabisa, mwenzako amejeruhiwa halafu wewe uka comment kuonyesha furaha, hata polisi walipouawa 8 kuna watu walikuwa wanafurahia, wapelelezi wetu wanafuatilia kuonyesha kilicho nyuma ya furaha yao

Swali: Tundu Lissu madai yake aliyosema kuna watu wanamfuatilia na kumtisha mliyafuatilia?

Jibu: Tundu Lissu akija mmuulize swali kuwa aliripoti kwa polisi? mtu ukitishiwa unatakiwa kuripoti kituo cha polisi sio kwa wanahabari. Tundu Lissu ni mwanasheria anajua haki zake

WhatsApp Image 2017-09-08 at 12.55.19.jpeg
WhatsApp Image 2017-09-08 at 12.55.20.jpeg
 
IGP Simon Sirro amezungumza na waandishi wa habari juu ya usalama wa nchi na kusema hali ni shwari kiujumla

Amezungumza juu ya mauaji ya Kibiti na kusema hali sasa ni tulivu na asilimia 90 ya wahalifu wameshakamatwa
Pia amezungumzia juu ya kauli ya Rais jana ya kuwakamata watu waliotajwa kwenye kashfa ya madini na kusema kuna watu wamekamatwa Manyara tayari
Pia amezungumzia suala la watoto kutekwa na kusema kwa sasa watoto wa watanzania wapo shwari
Amezungumzia suala la Tundu Lissu kupigwa risasi na kusema watahakikisha wanawakamata waliofanya huo na kuwataka watanzania kuacha kushtumiana kwa hisia wasubiri upelelezi ukamilike

Ni lini waliwahi kupeleleza wakaja na Genuine findings?
 
Read Full Transcript

IGP Sirro:Tuko serious sana na hili tukio, baadhi ya wapelelezi tumeshawatuma, na lazima tutawakamata waliohusika.

IGP Sirro: Waliohusika ni wahalifu kama wahalifu wengine, la msingi tushirikiane tuhakikishe tunawapata hao waliofanya hivyo.

IGP Sirro: Suala lililotokea kwa Mh. Tundu Lissu wote tunaona ni chalenge kwa nchi yetu.

IGP Sirro: Nakanusha kwamba jeshi la polisi linatumika vibaya hilo sio sahihi.

IGP Sirro: Suala la Lissu ni mapema mno kulizungumzia tumefikia wapi na tunaelekea wapi, tuvute subira.

IGP Sirro: Tusitoe mianya kwa hawa ambao tunawatafuta wakaweza kutukimbia au wakajua tunawatafuta.

IGP Sirro: Tunamkamata kamata Bw. Lissu kutokana na matendo yake, bahati nzuri anapokamatwa anapelekwa mahakamani.

IGP Sirro: Kimsingi sisi kama jeshi jukumu letu ni kutenda haki kwa raia wote na hatupo kumuonea mtu.
 
Swali: Kwa nini kupigwa risasi Tundu Lissu kumetokea kwenye eneo la viongozi wa serikali wanakaa?

Jibu: Uhalifu unatokea sehemu ambayo watu wanakaa, mfano mhalifu akitaka kuiba gari ataenda sehemu ambayo magari yanahifadhiwa
 
Hajataja kabisa kundi la watu wasiojulikana kwenye maneno yake?
 
Back
Top Bottom