IGP Simon Sirro arejea toka Rwanda, ziara ya kikazi imegundua mengi kuhusu Tanzania

Yanaweza kuwapo japo si kwa kiwango husika. Pia, wingi wa raslimali unaweza kuchochea mataifa au makundi kutaka kuvuruga amani ili kupata uchochoro wa kupata mali kwa bei rahisi kama ambavyo imekuwa ikiendelea nchini DRC.
🚍
 
UGAIDI ni nini? gaidi au ugaidi ni mtu au kikundi cha watu waliodhulumiwa haki zao za msingi. na wanapotaka haki zao wazipate huwa hawazipati na bado wana zidi kuonewa. wanapo amuwa kudai haki zao kwa kujitetea ama kwa silaha ama njia nyingine yoyote hapo hupachikwa jina la gaidi
 
Mimi nilichoona hapa IGP wa TZ amekwenda kuelekezwa na IGP wa Rwanda namna ya kukabiliana na ugaidi wa Nchi jirani yake ya Msumbiji. Akili nyingi inamuongoza akili ndogo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kufuatia ugunduzi huo watawashirikisha viongozi wa Kidini kwa ajili ya kupitia mafunzo ya Dini wanayofundishwa watoto kuanzia Chekechea, Sunday schools, Madrasa, Shule za Sekondari hadi Vyuoni kuonana pia na maaskofu na masheikh ili Kudhibiti vichocheo vya Ugaidi. Vyombo hivyo vya usalama vitataka kujua Je mafunzo wanayotoa viongozi wa dini kwa watoto na vijana ni kwa ajili ya kujenga utaifa na uzalendo au ni kwa ajili ya kubomoa taifa.
Sirro aache kuchanganya Dini na Siasa😅😅
 
Elimu ya madrasa ipitiwe upya kuna raia wa yemen alikuwa anafundisha madrasa kumbe alikuwa na ajenda nyingine km sio serkali kustuka mapema ingekuwa balaa
 
Aibu kubwa sana kwamba tunaweza kufanya ziara ya kujifunza Rwanda juu ya usalama , amani , mshikamano na utengamano wa taifa letu. Lakini ndio hivyo imeshakua, Tafsirii moja tu kuwa kuna mahali tuliacha dira ya kuasisiwa kwa taifa letu.
 
Yapo kitambo tu mkuu,umesahau shambulio la kina Osama kwny ubalozi hapo daslam?
Ubalozi wa USA ( malekani ). Mwenye maana harisi ya ugaidi ni malekani wengine wadandiaji tu, kama ule ugaidi ambao wamalekani wanaa maana hiyo pasinge kalika hapa kona bar wala kidimbwi.. kuna kitu wanatengeza na huenda tutakipa magaidi wenyewe hawapendi dhihaka hata kidogo 😁😁😁
 
Ugaidi ni neno pana . Ugaidi si sawa na uasi .. Twende kwenye chimbuko la neno Ugaidi kwanza ndio ujue kuna kitu kinalengwa au wanakitaka
Kuchambua maneno ni kuficha uhalisia..yote hayo yanafanana hata kama hayafanani,ni ukorofi wa watu fulani au imani fulani dhidi ya wengine huku wakichanganya kubeba mali,au mamlaka ya nchi,au kuchota watu wengi ktk imani yao kwa manufaa ya sadaka au mamlaka ziongezeke za kidunia dhidi ya walioshinda, yako mambo mengi...hapa Mwanza tulikuaga tunaona msikiti fulani,vitoto vidogo baada ya darasa la madrasa vinatolewa nje pale vinajipanga kwenye safu vinafundishwa mapigano/karate....sasa mtoto ukimjenga kwa namna hiyo na umleavyo ndivyo akuavyo itatokea nini baadae?
 
Back
Top Bottom