G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Leo IGP Simon Sirro katika taarifa yake kwenye kikao chake na NEC ameeleza umma kuwa kipo Chama cha Siasa kilichopanga kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020 kwa kupanga kuchoma vituo vya kuuza mafuta aina ya diesel na petrol nchini.
Kwa kuzingatia cheo alicho nacho kwa nchi, hizi mi tuhuma nzito na hazihitaji kuelezwa juu juu bali lazima kuwe na taarifa na ushahidi wa kueleweka.
Kuchoma vituo vya mafuta ni sawa na kutangaza vita, siyo jambo dogo hivyo taarifa isiyo ya juu juu inapaswa kutolewa na hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa. Chama cha Siasa kujihusisha na vitu vya aina hii ni sawa na ugaidi. Tunahitaji taarifa ila isiwe na mawaa.