IGP Simon Sirro afanya Mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Polisi nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya ndege, Naibu Kamishna(DCP) Matanga R. Mbushi anakwenda kuwa Mkuu wa vikosi Maalum vya Polisi, Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo Makao Makuu

Nafasi ya DCP Mbushi inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi(ACP) Jeremiah Shilla

Vilevile, aliyekuwa Kamanda wa Polisi kikosi cha Bandari, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, (SACP) Robert Mayala anakuwa Mkuu wa Mafunzo wa chuo cha Polisi Zanzibar

Nafasi ya SACP Mayala atakaimu aliyekuwa Afisa Mnadhimu Kikosi cha Bandari, Kamishna Msaidizi(ACP) Theresia Nyangasa

Aidha, taarifa ya Polisi iliyotoa habari hii imesema mabadiliko haya ni ya kawaida katika kuongeza ufanisi na utendaji kazi
IMG-20181010-WA0000.jpeg
 
Aya ya mwisho, mabadiliko ya kawaida hii kauli huwa sielewagi kwani mabadiliko mengine huwa yana lengo gani unaposema hayo ni ya kawaida?
 
Sirro anatakiwa sio kubadilisha hao wa juu tu bali hata wa chini;kuna ma OCS wamekaa kwenye vituo muda mrefu sana kiasi kwamba wahalifu wamekuwa marafiki zao. Mfano pale KAWE vijana wanavuta bangi mchana uwanjani ili hali kituo cha polisi kiko karibu hapo hapo!!!
 
Mimi huwa nashangaa Simba kuwaua chui na chita, kumbe angewaacha wao wawe wanaua mnyama anawasubiri wale washibe harafu na yeye anakula kiulaini bila kuvuja jasho, kumbe ndiyo huwa hivi
 
Back
Top Bottom