Igp saidi mwema jeshi la polisi alijatenda haki kwa familia ya mzee ally khatibu wa arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igp saidi mwema jeshi la polisi alijatenda haki kwa familia ya mzee ally khatibu wa arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by zamlock, Aug 24, 2012.

 1. z

  zamlock JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mimi kama mpenda haki na asiye penda kuona wanyonge wana nyanyaswa nimeamua kuwaletea kisa hichi hapa jf wadau na wapenda haki kwa kila mtu waweze kusoma na kuchukua hatua kwa yeyeto ambaye anaweza kuwa na msaada kwenye familia hii ya mzee ally khatibu ambaye saizi ni marehemu.


  Huyu mzee alikuwa nafamilia ya watoto watano ambao amewazaa na kuwalea katika jiji la arusha kwenye mtaa wa bondeni barabara ya ndovu na alikuwa ana miliki nyumba mbili ambazo alizijenga moja aliijenga pangani na ingine alijenga kwenye huu mtaa wa bondeni barabara ya ndovu.
  Sababu kubwa ya kuandika haya nikuonyesha umma jinsi gani jeshi la polisi linavyo shirikiana na matajiri wa nchii hii na watu wajanja ambao wanatumia nafasi zao kuwanyanyasa watanzania wenzao ambao hawana hatia.

  Kilichotokea kwenye familia hii ni msimamizi wa wa mirathi kuchukua jukumu la kufanya biashara ya nyumba alikuwa ameachiwa na baba yake ilikuwa pangani ambayo alichukua jukumu la kuiuza nyumba hii kwa sababu alikuwa na mamlaka nayo kwa mujibu wa maelezo ya familia ni kwamba alipewa nyumba hiyo kuwa ni yake kabisa na alipochukua jukumu la kuuza familia aikuwa na malalamiko kwa sababu ilikuwa ni yake. Baada ya kuuza nyumba yake na kujipatia pesa na kutumia ikaisha ndipo alipochukua jukumu la kwenda kwenye nyumba ya pili ambaye baba yao aliwaachia watoto wote na kesema kuwa nyumba hii isiuzwe

  alicho kifanya bwana huyu ambaye ni mtoto wa familia ya mzee ally ambaye kwa jina ni selemani ally alimtafuta mteja kwa jina anaitwa deo ambaye ni mfanya biashara ya mazao hapa mjini arusha na kufanya ujanja wao pasipo kuwashirikisha wanafamilia wakauziana nyumba hiyo ya familia ambayo iko mtaa wa bondeni aliyoitolea usia na mzee ally kuwa isiuzwe kilichofanyika huyu bwana akafanikiwa kumshawishi kati mmoja kwenye familia ambaye anaitwa fatuma ally khatibu aliyekuwa anatunza hati ya nyumba yao na kumpa hiyo hati na kwenda kumkabidhi deo ambaye aliyenunua hiyo nyumba kwa njia za kiujanja pasipo familia kujua na siku ilipo wadia deo na bwana selemani ally na huyu fatuma walikwenda kwa mtendaji na kutaka kufanya makubaliano ya mauziano ya nyumba hiyo na ndipo mtendaji alipo wauliza hii nyumba ni ya familia kwa nini mje nyie tu msije wote mkakubaliana?

  Hapo ndipo ukweli ukabainika kuwa nyumba inatakiwa kuuzwa kwa njia za magamu pasipo familia kujua yote na ndipo mtendaji alipochukua jukumu la kuiita familia yote na kupewa taarifa na kilichotokea ni familia nyingine kukataa na kusema hii nyumba tumeachiwa urithi na baba yetu na maagizo ni kuwa isije kuuzwa na ndipo bwana selemani akatoa kauli na kusema yeye ndiye msimamizi wa mirathi kwa hiyo atauza tu watake wasitake na ndipo mtendaji alipoona hii ni hatari akawaambia warudi kesho yake wakiwa wameelewana na kilichofuata kesho yake bwana selemani alikwenda kwa mkuu wa wilaya na kumueleza kuwa mtendaji amekaata kutuuzia nyumba yetu na ndipo mkuu wa wilaya alipo toa maagizo kuwa mtendaji aende ofisini kwake na makaenda na kumkuta bwana deo na selemani na alichokisema mtendaji ni kwamba hawa walikuja ili nyumba iuzwe pasipo familia ingine kujua na ndipo nilipo chukua jukumu la kukata mpaka watakapo kubaliana na kuongeza kuwa nikubali kufanya mauziano ya nyumba hiyo watanipa silingi laki mbili lakini nilikataa

  mdipo mkuu wa wilaya alipo chukua jukumu la kumueleza bwana seleman upuuzi wako huo siutaki hapa tena naweza kukuitia polisi sasa hivi wakuweke ndani na ndipo mkuu wa wilaya akaagiza hiyo nyumba isiuzwe kwa sababu ni nyumba ya usia wakaondoka na walivyo ondoka wakaenda wakatumia njia ingine ya kukabidhiana fedha kw mawakili na kilichofuata ile familia ilipigiwa simu na kuambiwa njooni mchukue cheq zenu hapa kwenye ofisi zetu na ndipo ile familia ikataa nakusema sisi atujauza nyumba na atuwezi kuja kuchukua pesa hizo na amri ya kuuza hiyo nyumba ilitolewa na mahakama ya mwanzo na hakimu anajulikana kwa jina la kasimu na baada ya hii familia kupeleleza nakujua aliyetoa amri hiyo ni mahakama ya mwanzo ndipo walipokwenda kwa jaji na kumueleza haya yote na yule hakimu akaitwa na jaji na kuulizwa kwa nn umefanya haya akajibu kuwa amepewa amri na mkuu wa wilaya na ndipo jaji alipo mpigia simu mkuu wa wilaya na kumuuliza na ndipo mkuu wa wilaya akamjibu kuwa nimeletewa hiyo kesi kwangu na mimi nimeisimamia na kuwaeleza wasiuze hiyo nyumba

  hakika pesa ni kitu kingine katika maisha ya mwanadamu ndipo ujanja ulipofanyika yule bwana deo na seleman walienda na kumuona mkuu wa polisi [ocd] wakati huo alikuwa ni bwana zuberi ambaye saizi ni staf officer kwenye jeshi la polisi hapa arusha,na kupewa pesa ambayo ilipelekea akajichukulia mamlaka ya kupeleka askari wake na wakati huo huo bwana deo ambaye alinunua nyumba kutoka kwa bwana seleman alichukua kundi la watu ambao aikujulikana wametoka wapi walikuwa wengi sana zaidi ya hamsin wakiwa kwenye roli na ulinzi wa jeshi la polisi ukiwepo na kuwasimamia kuvunja nyumba hiyo usiku wa manane pasipokuwepo na kibali kutoka mahakama ya kuwaruhusu kuvunja nyumba usiku wa manane hakika kilikuwa ni kitendo cha kiunyama sana kwenye familia hii wakapoteza vitu na mali zao na kuvunjiwa nyumba usiku wa manane haki yao ikapotea kwa sababu ni wajane pia hawana mtu wa kuwatetea na kaka yao ambaye ni huyo mkubwa akawageuka kwa sababu ya tamaa ya pesa,

  ila tuna mshukuru jaji kiongozi kulichukulia swala hili umuhimu na kuwashauri waende mahakamini ili wakaweze kupata haki yao kwa sababu wana copy ya hati ya nyumba yao na mpaka tunavyo ongea hvi aijulikani nyumba hiyo imeuzwa kiasi gani cha fedha imekuwa ni kilio na majozi makubwa sana na saizi wamepanga kwenye nyumba wanalipa kodi wana miezi mitatu sasa toka wamebomolewa nyumba yao na wanalia sana na aliyekuwa ocd wa wilaya bwana zuberi kwa sababu yeye ndiye aliyeleta ulinzi na akiwa amesimamia zoezi hilo na bwana daudi mpaka nyumba ikavunjwa usiku wa manane

  na kibaya zaidi kabla ya sikukuu ya idi huyu dada ambaye ni mkubwa kwenye familia yao kwa upande wa madada anajulikana kwa jina la zubeda alikwenda kwenye nyumba yao hiyo iliyo bomolewa na kwa bahati nzuri wakakutana na anaye daiw akununua nyumba hiyo bwan deo ambaye ni mfanya biashara maarufu hapa mjini kilichotokea ni mvutano wa hapa na pale na ndipo deo alipo mtolea bastola na kutaka kumpiga risasi na wananchi wenye hasira kali walipotokea na kutaka kumpiga deo kwa kitendo alicho kifanya hakika mama huyu alilia sana kuona haki yao inaondoka bila vyombo husika kuingilia kati na kwa maelezo yake wameshapelekwa polisi na huyo deo kwa amri ya bwa zuberi zaidi ya mara kumi nakuwekwa ndani huku aliyekuwa ocd akimweleza uwezi pambana na wenye pesa utaumia
  na baada ya huyu mama kwenda kuripoti polisi ndipo deo alipo mfuata na kumtishia kuwa atamlomesha tu na atapambana naye .
  Mambo ni mengi siwezi elezea hapa ila mama huyu ameomaba msaada kwa yeyote atakae ingiwa na huruma juu ya swala hili basi ampe msaada wa kisheria kwa sababu kesi ndo iko mahakamani itatajwa tarehe kumi na tisa na ana hitaji pia msaada wa advocate kwa kumsaidia na simu ya mama ambaye nimsimamizi wa swala hili ni
  0752890102 kwa mawasiliano juu ya mtu yeyote anayetaka kumpa msaada wa kisheria na mawazo juu ya nn afanye
   
 2. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Mh! ebu pia peleka copy kule jukwaa la sheria..unaweza saidika
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  du umenikumbusha mbali kweli,Nasisi tulifanyiwa unyama huohuo,aliyeuza nyumba yetu ya vyumba 12 ni mama yetu mdogo toka nitoke na mama yangu na aliyenunua nyumba yetu ni ndugu yetu kbs MSOFFE alikua anafanya kazi manispaa Moshi na yule aliyepigwa risasi eneo la kia.....nawashauri hao wana ndugu wapambane nyumba yao itarudi na waweke maombi mbele kwani Mungu yu Mwema,Hata sisi ilikua ngumu kuirudisha lkn Mama yt alipambana mbaya wakaturudishia
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu haya nimachache, ni mengi wamefanyiwa ukiona saizi wanapoishi utasema kwel haki iko kwa wenye pesa tu, sasa ukienda pale kwenye nyumba kila unaye mgusia swala la nyumba hiyo ni kusikitika sana kwa unyama waliofanyiwa watu hawa.. Ndugu yao kawageuka tumbo moja ndo anafanya unyama huu.
   
 5. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Poleni sana, umoja wenu ndio silaha itakayowasaidia, msikubali kurubuniwa kwa fedha mkasalitiana. Nenda kwa RPC au RCO kumjulisha jinsi huyo Deo anatumia silaha yake vibaya na pia kuhusu Bw. Zuberi. Jaribuni kuwasiliana na jamaa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wanaweza kusaidia.
   
 6. z

  zamlock JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndugu ubungo huyu mama ana hitaji msaada wa mawazo na ushauri afanye nini uzuri nimeweka simu yake hapo chini ni vyema ukampigia ukampa ushauri nini afanye hakika atafarijika sana hata kwa mawazo tu
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeshampigia ndugu yangu. Thankx
   
 8. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  poleni sana na Mungu awape ujasiri mfuatilie mahakamani ili mpate haki yenu .ndo hali halisi ya jeshi la polisi tz na si

  wakuamini asilimia zote kwenye kulinda raia na mali zake
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hii ndo tanzania.....

  Ukiwa na hela hata serengeti utauziwa.....
   
Loading...