Igp mwema na rpc arusha wajiuzulu haraka-kupisha uchunguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igp mwema na rpc arusha wajiuzulu haraka-kupisha uchunguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkombozi, Jan 7, 2011.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana Jamii, nilikua na waza kidogo ni nani wa kuwajibika hususani mauaji yaliyofanyika Arusha. Nimegundua IGP mwema ndio mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya Arusha pamoja na majeruhi. Hii ni kutokana na kuawaagiza polisi kuchukua sheria mkononi na kupiga risasi watu wasio na hatia yeyote. Nguvu aliyotumia ni kubwa sana hasa pale police inapoamua kutumia risasi za moto kumpiga raiya ambaye hana silaha yeyote. Ni wakati muafaka sasa wa kumwomba IGP ajiuzulu kutokana na kashifa ya mauaji na kujeruhi watu wasio na hatia. Wao wameishitaki CHADEMA kwa kuandamana tu, je aliyeua si zaidi ya kuandamana? Kutoa uhai wa mtu?Je wategemezi ya waliokufa au waliopata majeraha na vilema vilivyotokana na fujo? Tunaomba tuungane wote kwa pamoja kufanya haya yafuatayo

  1.Kumtaka IGP ajiuzulu wadhifa wake kutokana na kashifa ya mauaji na kujeruhi Arusha na afikishwe mahakamani.
  2.Iundwe tume huru ya kuchunguza ili wote wanaohusika wafikishwe mahakamani
  3.Kamanda wa Police Arusha nae ajiuzulu na kufikishwa mahakamani pia

  Tushirikiane wananchi wote, asasi za kiraiya, tume ya haki za binadamu, NGOs, jumuiya ya kimataifa na vyama vya siasa (CHADEMA, CUF,DP,TLP,NSSR,UDP,PPT n.k) ili wahanga wa majeruhi na mauaji ya Arusha wapate haki zao. Bila hivi ndigu zetu watakua wanauwawa bila sababu na sisi tunanyamaza tu
   
 2. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Muone na huyu mnafiki mwingie (nukuu kutoka Global publishers)
  'WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ATOA TAMKO
  serikali leo mchana imependekeza pande zinazosigana katika siasia mkoani Arusha zikae meza moja na kutafuta suluhu kwa mazungumzo na sio kwa vurugu. Hayo yamesemwa mchana huu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Shamsi Vuai Nahodha alipoongea na wanahabari ofisini kwake jijini Dar, akiwa na Inspketa Jenerali wa Polisi, Afande Saidi Mwema, ikiwa ni siku moja baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa CHADEMA baada ya kufanya maandamano yanayodaiwa kuwa si halali. Inasemekana watu wawili wamepoteza maisha na sita wamejeruhiwa vibaya katika vurumai ya jana.
  Mh. Nahodha, ambaye amekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibra kwa muda mrefu na mwenye uzoefu wa mambo hayo, amesema serikali imeamua kuingilia kati mgogoro huo kwa kuziweka meza moja pande mbili zinazokinzana ili kuleta amani mpya na kuidumisha jijini Arusha.
  Pia Mh. Nahodha amesema askari polisi yeyote ambaye itathibitika alikwenda nje ya mipaka yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria"

  Hivi hekima hiyo anaiona sasa baada ya mauaji? Halafu hapo kwenye red, mtu wa kwanza kuchukuliwa hatua za mauaji si yupo karibu naye hapo- huyo shemeji yake mkwere?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  nafikiri watz hawana hiyo hulka bado
   
Loading...