IGP Mwema: Jaribu Uzalendo, Madaraka ni Ya Muda tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema: Jaribu Uzalendo, Madaraka ni Ya Muda tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jul 16, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  IGP Mwema, wananchi hawana imani na jeshi unaloliongoza. Vituko vya jeshi la polisi ungekuwa mzalendo na sio mchumia tumbo, kusema kweli mzee wangu ungejiuzulu. Wananchi badala ya kulindwa wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kuuwawa na jeshi la polisi ambalo limegeuka kuwa jeshi la majambazi waliopewa silaha kuwalinda wananchi. Hauna tofauti na fisi anayepewa kazi ya kulinda nyama

  Shutuma dhidi ya ACP Ahmed Msangi kusema kweli usingeyanyamaziaa na kumtoa Suleiman KOVA kafara kwa kumpa mbuzi ndani ya gunia hasa baada ya ushahidi wa kutisha kutolewa kuonyesha ughaidi na ujambazi sugu wa mtuhumiwa ACP Msangi

  Unafahamu fika kwamba polisi wako pamoja na TISS wamechemsha kwa kutuletea ushahidi wa kijinga, kipumbavu na kitoto kuhusiana na mkenya kuwa ndiye mtekaji wa dr. ulimboka. Mungu ameanza kuwaadhibu ndio maana mnayoyafanya ni kama watu waliochnganyikiwa. Tangu mwanzo tulijua kwamba mtu angebambikiziwa uchafu wa TISS na Polisi waliotumwa na Kikwete kumuua Ulimboka. Kwa heshima na taadhima pamoja na uzalendo, tafadhali fikiria nchi yake ya baadae. Jiuzulu. Hata kama unamlinda kikwete na serikali yake dhaifu, kujiuzulu sasa hivi kutakupa maisha maisha mazuri kuliko kusibiria kufukuzwa hapo baadae na wananchi waliowapeni madaraka.

  Jeshi lako linashindwa hata
  1. Kumhoji ACP Msangi kwa sababu ametajwa kama mtuhumiwa?
  2. Yule aliyepigwa hospitalini akisema bado yuko hai?
  3. Obedi wa Ikulu?
  4. Mawasiliano ya simu ya Ulimboka na watekaji?
  5. Gari lililotumika ndani ya hii tanzania isipatikane hadi wa leo?
  6. Hata kuwahoji mashuhuda pale leaders club?
  7. DNA testing nguo au vitu vngine vya ulimboka?

  Alafu unatuletea ujinga wa mkenya, tena kutumia kanisa, sehemu takatifu ya Mungu? Shame on you. Nyie mnaojiita viongozi serikalini si nmna watoto? Msidhanie nyie na watoto wenu mtaishi kwa amani kwa mazingira mnayowatengenezea ya chuki. watoto wenu Wataishi kujuta maisha yao yote. Damu zinazomwagika bila hatia zitawaandama maisha yenu yote. Unyanganyi na hujuma mnaowafanyia wananchi wasio na hatia daima itawanyima amani. Majumbani mwenu amani itatoweka. Mtakufa kama kuku. Mtapata na magonjwa ya ajabu. Watoto wenu, watashinda wakitumia madawaya ya kulevya, wengine watakuwa makahaba, na majambazi kama mlivyo. Mungu aliyejuu mbinguni atawapa maisha marefu myashuhudie haya yote ambayo yatakuwa ni malipo ya ukatili wenu

  Magari ya kifahari mliyonayo yatageuka kuwa silaha za kuwakata miguu. Majumba makubwa mliyokuwa nayo yatageuka kuwa mapango ya na ugomvi majonzi. kamwe hamtaweza kuiona amani wala kuisikia. hela mlizoiba hazitawanululia hata tabasamu. Mungu na asikie vilio vya watanzania. Nyumba ya Kikwete, Pinda, Mwema, Othman, Jambazi msangi na wengine wote wanaofanya uhalifu waishi wakitambua kuwa siku ya kusaga meno inakuja. Tunawaombea maisha marefu ili muone matunda aya uovu wenu wa kuwang'oa watu masikini wanaodai haki za msingi meno na kucha kiunyama
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na mleta mada maana kadri siku zinavyoenda ndivyo wananchi wanavyozidi kupoteza imani na jeshi la polisi na chuki inazidi kuongezeka dhidi ya polisi.Hao walioambiwa wamejazwa upofu hilo wala hawalioni na wamejisahau kabisa na kuzidi kufanya madudu.Ila iko siku!
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  anastaafu mwaka kesho, mkuu wake kamwambia alambe mkataba, kasema inatosha
   
 4. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  mwema na kundi lako hizi chuki mnazozijenga kwa wananchi dhidi ya jeshi la polisi mtakujazijutia...hakuna kitu kibaya kama kujenga chuki miongoni mwa wananchi ili kulifurahisha kwa muda kundi fulani. Wakati na historia vitawahukumu
   
 5. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Hawa watu hawamuogopi mungu kabisa, wana damu za watu wengi mikononi mwao,
  na mungu anazidi kuwaumbua, jana mchungaji gwajima kawaumbua kwa kuwakana, pili hata timing ya matukio ya uyo mtekaji wao, tukio la kutekwa na maneno ya kova vimetofautiana,
  ina maana ata walopewa jukumu la kuwasafisa hasa watu wa tiss yawezekana iq zao ni ndogo sana
   
 6. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante mtoa mada , naona umeamua kumwambia ukweli. kwani wajue wewe umetoa ujembe wawatanzania
   
 7. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  IGP naye c anafukuzia kua mwenyekiti wa bodi baada ya kuustaafu.
   
 8. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Kwa hiyo atarudi Interpol au..?
   
 9. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hv huyo mzee kumbe alikuwa huko!?
  Duu kwa mfumo yetu hata aje kiongozi gani hatuwezi kuendelea!
   
 10. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 769
  Trophy Points: 280
  Kama intelijensia ya kitanzania ndo iko hivi inayoshindwa hata kupanga operations zake hahaha basi Tanzania ipo uchi mbele ya mataifa mengine na hata wakitaka kutuvamia bhasi muda wowote uwezo huo wanao. Najua Mungu ameshaanza kuwaadhibu na bado itafikia kipindi hata mtaani hamtakua mkipita kwa aibu yenu na jinsi mnavyoendelea kujijengea maadui.
   
 11. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  inamsubiri
  hata akirudi wapi, jehanamu
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Lakini yana mwishi haya
   
 13. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Mwema kiazi tu mwingine na tumbo ka mfuko wa nya...
   
Loading...