IGP Mwema atangaza DEATH PENALTY | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema atangaza DEATH PENALTY

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hume, Oct 23, 2007.

 1. H

  Hume JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Jana, wakati akiongea na vyombo vya habari IGP alitangaza adhabu ya kifo kwa wale wenye mikakati kama iliyotokea CHATO, LINDI, na Singida.

  Atakayeandamana kwenda polisi kwa lengo la kumtoa mharifu, basi ajiandae kukabiliana na risasi za moto kichwani kwake.

  Hukumu hii aliyotoa tusijeona wanaitumia ndivyosivyo!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Niliuliza "mko tayari"... ?
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wacha spinnning, alizungumza kwa uwazi na kuonesha ni wakati gani hiyo death penalty itumike. umeyaacha yote yalioongelewa ukaona udaku huu ulete hapa
   
 4. H

  Hume JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45

  Wakati kama uliotumika kwa KOMBE siyo?
  Kuna haja gani ya kumuua mtu asiyekuwa na silaha?
  Kwa nini usimjeruhi? Ndo mafunzo yao yalivyo?

  Mpaka uamue kwa makusudi mazima kumpiga mtu risasi ya kichwa wakati ungeweza kumpiga ya mguu ili akaadhibiwe na mahakama ni sawa kweli?
  Au na wao hawana imani na mahakama, angelisema hilo pia!
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Niliogopa sana kumsikia huyu Mwema akitangaza mabaya. Hii ni hatari, unasimama unatangaza kupiga watu risasi za moto. TUNAELEKEA WAPI?

  Suala ni kwamba wajiulize ni kwa nini wananchi wamefikia hatua hiyo ya kuvamia vituo vya polisi. Je, hawana Imani na Police au hata Serikali yao na Mahakama au hata na bunge? Pengine ni ndiyo. Kitendo cha Kuzomewa mawaziri kinaashiria nini?

  Risasi za moto sio suluhisho kwa watu wanaohisi kuonewa na kukatishwa tamaa, angalia mfano wa Afrika kusini ya makaburu na Palestine.

  Mjiangalie nyie Police na serikali kwa ujumla mmekwenda kombo wapi hadi wananchi wanakuwa wao ndio Wapelelezi, askari wa kukamata waharifu na mahakimu, Japo Muungwana kawakataza wapinzani wake juzijuzi tu kufanya hizo kazi, sasa wananchi mkiendelea nazi vichwa vyenu vitakumbana na risasi za Moto.

  Kabla ya kuliangalia tatizo kutokea nje, Mwema anatakiwa aliangalia kuanzia ndani ya Jeshi lake na kujiuliza ni kipi kimeenda kombo. Kwa hakika wananchi wanapoteza imani na vyombo vya utawala. Hebu tujichunguza kwanza tusijeanza kutishiana maisha katika nchi yenye misingi ya Udugu na Umoja.

  Kauli kama hiyo ya matumizi ya risasi za moto siiungi mkono hata kidogo na pia nalaani tabia ya wananchi kuchukua sheria mkononi kuua watuhumiwa.

  Lakini chanzo cha haya yote ni Rushwa na Ufisadi.
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwema ang`aka

  2007-10-23 10:23:02
  Na Mwandishi Wetu


  Jeshi la polisi limeruhusiwa kisheria kutumia nguvu, hata kuua ikibidi, pale inapotokea raia kuvamia vituo vyao, kuvichoma moto, kuua au kutaka kutorosha watuhumiwa. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Bw. Said Mwema, alisema jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari juu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi, kuvamia vituo, kujeruhi polisi na kuua watuhumiwa.

  Aliwataka raia kufahamu kuwa wanahatarisha maisha yao wanaposhiriki kwenye matukio kama hayo kwani Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Ibara ya 16 vifungu vya 18, 18b na 18c vinaruhusu matumzi ya nguvu katika kulinda maisha na mali.
  Alitaja kifungu cha 29 cha Sheria ya Polisi kinaruhusu kutumia silaha ili kuzuia kutoroshwa kwa nguvu, watuhumiwa walio chini ya ulinzi na pia kuzuia polisi kukamata mtuhumiwa.
  ``Kuvamia vituo vya polisi, kuchoma moto, kutorosha watuhumiwa na hata kuwaua ni mazingira ambayo kisheria polisi wanaruhusiwa kutumia nguvu na silaha na hata ikibidi kuua,`` alisema IGP Mwema.

  Katika mkutano huo, Bw. Mwema alionya juu ya tabia ya kuwaua, kuwachoma moto na kuwatesa watuhumiwa mbalimbali mitaani na kusema vitendo hivi vinaendelea kujijenga kwenye jamii na vinahalalishwa kwa kisingizio cha `kupambana na wahalifu.`

  ``Vikiachiwa viendeelee vitazaa ukatili na kutengeneza mazingira yasiyoheshimu utawala wa sheria, watu kutoheshimiana na kuhatarisha amani na utulivu.`` Aliongeza kuwa huwezi kupambana na uhalifu kwa kufanya uhalifu mwingine na kwamba hiyo ni dhana inayohatarisha amani kwa jamii.

  Bw. Mwema aliyekuwa na makanda wa jeshi hilo akiwemo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Bw. Mohamed Simba, alikemea tabia ya kupambana na vyombo vya dola kama, polisi, mahakama na ofisi za serikali pale raia wanapodhani hawakutendewa haki na wanaowatuhumu.

  Bw. Mwema aliwaona hata wale wanaovamia majengo ya ibada, ofisi za vyama, za serikali na za kazi.

  ``Kwa maoni yetu, hii siyo njia halali ya kushughulikia migogoro iliyoko katika jamii. Iwe ya kidini, wafugaji, wakulima, kisiasa na kadhalika,`` alisema.
  Alisema uvunjifu huo wa amani hautaruhusiwa kuendelea na kwamba polisi itawaadhibu kisheria wanaoshawishi, kushiriki, kusaidia na kuchochea vitendo hivyo.

  Aliwataka viongozi wote na kwa kila ngazi kupambana na uhalifu kwa kuwaelimisha wananchi kuacha uhalifu, mfano mauaji ya imani za kichawi, ubakaji, ulawiti na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  Pia aliwataka wakemee uuaji wa vibaka kwa kisingizio cha `watu wenye hasira kali`, uvamizi wa taasisi za dola na pia kuelimisha jamii kuwa dawa ya uhalifu si kufanya uhalifu.

  Mwezi huu matukio ya kujichukulia sheria mkononi yamejiri huko Singida ambapo wavamizi walivunja kituo cha polisi na kumua mtuhumiwa wa mauaji.

  Wilayani Chato, Kagera wanavijiji walichoma makao makuu ya polisi ili kumuua mtuhumiwa anayedaiwa kukutwa akiwa na ngozi ya binadamu.

  Huko Tanga raia walivunja ofisi ya kijiji kumuua mtuhumiwa wa mauaji aliyekuwa amefungiwa humo.

  Wakati huo huo, Jumbe Ismailly anaripoti kutoka Singida kwamba Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilongero na watu wengine watano wanashikiliwa na polisi Mkoani Singida kwa tuhuma za kuvamia kituo kidogo cha polisi, kumshambulia askari na kumuua mtuhumiwa wa tukio la vifo vya watoto wawili wa familia moja.

  Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bi. Celina Kaluba, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 20, usiku kwenye kituo kidogo cha polisi cha Ilongero, wilaya ya Singida Vijijini.

  Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanaoshikiliwa kufuatia tuhuma hizo ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Issah Swedi, Hamisi Ally (Tall) (40), Yusufu Jumanne (19), Victor Soteli (30), Zena Yusufu (45), na Josephine George (Mwinda) (45), wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Ilongero.

  Hata hivyo, Kamishna huyo alisema pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, polisi bado wanaendelea kuwatafuta watu wengine ambao tayari wametambuliwa kuwa ndiyo walioongoza katika mashambulizi hayo na kusababisha mauaji ya mtuhumiwa huyo.

  Bi. Celina alisema siku ya tukio, kulikuwepo na zaidi ya wananchi 200 wenye hasira kali, waliovamia kituo kidogo cha polisi Ilongero na hatimaye kumtoa nje kwa nguvu mtuhumiwa Khalfani Mohamedi maarufu kama Nkindwa Mile (28),ambaye alikuwa mkazi wa Kijiji cha Mrama, katika Halmashauri hiyo na kisha wakamuua kwa kumpiga mawe.

  Aidha, Kamanda huyo alifafanua kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye sasa ni marehemu alikuwa amekamatwa Oktoba 20, 2007 usiku na kufikishwa kituoni hapo kwa kosa la mauaji ya watoto wawili, Twahiba Athumani (13), na Zulfa Athumani (7), Oktoba 14, mwaka huu.

  Kamanda huyo alisema kwamba, wananchi hao waliokuwa na jazba walivunja mlango wa chumba cha mashtaka na hatimaye mlango wa chumba cha mahabusu, kwa kutumia mawe makubwa na kumtoa ndani hadi nje ya kituo mtuhumiwa, ndipo walipoanza kumpiga kwa kutumia mawe hadi kufa.

  Baada ya kumuua, walimsogeza nje ya uzio wa kituo cha polisi na kumfunika kwa majani kwa lengo la kutaka kumchoma moto.

  Lengo hilo halikutimizwa kutokana na kuwasili kwa askari kutoka Singida mjini na kuanza kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani.

  Kadhalika, Bi. Celina alisema kuwa kitendo hicho cha kufika askari kiliwazidishia hasira wananchi hao na kuanza kuwarushia mawe polisi.

  Alisema kwamba gari la polisi lenye namba za usajili PT 0704, Landrover pick up, lilipigwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele.

  Bi. Celina alisema amesikitishwa na kitendo cha wananchi hao cha kujichukulia sheria mkononi, hasa ikizingatiwa kwamba mtuhumiwa alikuwa tayari mikononi mwa polisi.

  SOURCE: Nipashe
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kiasi fulani tunaweza kuangalia ni kwa nn akasema kuwa kuuwa halali ni mazingira yepi, mmh kwa spinning nyinyi mwisho na kuna watu liandikwalo basi sawa wanaanza kusupport usiwe ndondocha
   
 8. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hata waliouwawa pemba na mwembe chai kulitolewa sababu za kutetea mauaji yao!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Oct 23, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa vile polisi wetu wana license to kill kwa kutumia vipengele hivyo vya sheria itakuwa ni jambo la kuchekesha kuhoji polisi wanapoua wakitimiza wajibu wao wa kisheria.
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mazingira yatahukumu, na sio utashi pekee mkjj, walivamiwa kituo wakamtoa mtuhumiwa na kisha kumuua sasa mazingira haya yaachwe yameee eeeh?

  hata siku moja serikali na vyombo vya usalama kwa hapa hamna budi kukemea
   
 11. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi hualiwaita wanahabari ktk mkutano wa ilikuwautubia tu na kisha kuingia mitini,hakuna swali wala hoja imepita hiyo.mimi habari za bongo huwazinanipa tabu sana kuzisoma zinakuwa kama hadithi za juma na rose.
  kweli waandishi wetu msikubali mikutano ya namna hiyo inawadhalilisha sana kwa wasomaji wenu,mnakuwa kama maduwanzi kila kitu nyie ndio mzee
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  4256.jpg

  naam pengine masuala yaliulizwa na ndio ikapatikana stori nzima hata hivyo, saa zengine maelezo yanakuwa wazi kiasi cha kujitosheleza
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...huyu ng'ombe inabidi ajiuzuru ,hawezi kutishia wananchi kiasi hicho na waache waanze mchezo wa kuua raia kwa visingizio vya kipumbavu hivyo,wakumbuke wananchi nao wana uwezo wa kupata hizo bunduki...wakiua watauliwa tuu nao bora wasianze!
   
 14. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kila siku nasema hapa watu ni wepesi wa kusahau,huyu mwema sidiye waliwafungia mahabusu kule mbeya na kusababisha mauti ya maabusu,hana jipya na mikono yake ilaaniwa na damu ya mwanadamu.kama ingekuwa ni kuangalia record ya mtu basi huyu asingefaa kuwa igp.kalini bongo ushikaji kwanza kazi baadaye.
   
 15. Bi. Senti 50

  Bi. Senti 50 JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 291
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mtu kawaambia ukweli mnasema kawatishia. Itawezekana vipi raia wachukue sheria mikononi kwenda kituo cha polisi na kumkwapua mtuhumiwa na kumuua kana kwamba Tanzania haina sheria? Je siku mmoja na ukichaa wa baadhi ya watu wakiamua kuingia ofisi ya Wizara au hata Ikulu na kumfanyizia "mbaya" wao si tutapiga kelele sana.
   
 16. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi waungwana mnataka watu waanze kuvamia vituo vya polisi na kuchoma watu moto?

  Lazima utawala wa sheria ulindwe kwa nguvu zote na hiyo ipo kila sehemu hapa duniani.

  Hata kama polisi wameshindwa kazi yao lakini hata siku moja siwezi kutetea raia kujichukulia madaraka mikononi mwao. Madhara
  ya hatua kama hiyo yanaweza kuwa makubwa mno.

  Niliwahi kushuhudia sehemu, vijana wakamkamata jamaa na kuanza kupiga kelele za mwizi, watu wakaja na kumponda mawe mpaka kufa, kumbe jamaa alifumaniwa tu na mke wa mtu.

  Tunapotetea utawala bora basi ni kwa kila mtu kuanzia raia mpaka rais wetu
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....hakuna mtu ana support huo upuuzi wa wananchi just kwa sababu wana hasira,walichofanya hao wananchi ni sawa sawa na MWEMA anachotaka kufanya
   
 18. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Bi senti tatizo ni kuwa wananchi wamepoteza imani na vyombo vinavyowaongoza. Kuanzia bunge, serikali na mahakama. Inawezekana mwenzetu unafanya kazi ikulu na unaishi oysterbay ndio maana haya mambo huyaoni na unazungumza hivyo.

  Nitakupa mfano mmoja. Fikiria mwanaume rijali (Mr.X) mwenye umri wa miaka 57 kambaka mwanao wa kike (kiume), mwenye umri wa miaka 4. Ushahidi wa daktari unaonyesha Mr.X kambaka mwanao. Mr.X kapelekwa kituo cha polisi ili sheria ichukue mkondo wake. Baada ya masaa mawili unamuona aliyetenda ukatili kwa mwanao yupo mtaani, ni lipi utakalofikira haraka kichwani mwako.

  Kwanza napoteza muda wa bure ku-type hapa. Hebu angalia kesi ya kaka dito. Sasa hivi anaruhusiwa mpaka kuhutubia wananchi kwenye majukwaa kwamba wananchi wanao hoji viongozi wa serikali wakalale na wake zao.

  Hakuna raia ambaye angependa kuingilia kazi za polisi. Tatizo linakuja pale polisi inaposhirikiana na wahalifu kupindisha sheria. Na hili tatizo la kuficha maradhi, mauti itatufichua siku moja. Hata kama si wewe, basi mjukuu wako.

  Naomba kuwasilisha.

   
 19. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  !!!Mtanzania nadhani hapa unaongea kwa ushabiki. Polisi ya leo haina cha mtuhumiwa wala anayetuhumu. Vituo vya polisi ni sehemu za biashara sasa hivi. Kama unabisha nenda kashitaki polisi kwamba umeibiwa "asset" yako, na una una ushahidi kuwa Mr.X ameshiriki katika huo wizi. Mpaka kesi inakwenda mahakamani, mtuhumiwa na mshitaki mtakuwa mmetolewa upepo sawa sawa. Hivi nyie mnadhani mapolisi wana mudu vipi ugumu wa maisha kwa mishahara hii ya bongo. Mapolisi ni kaka zetu, ni dada zetu, ni wadogo zetu, ni baba zetu. Wengi tunajua ujanja wanaotumia kumudu maisha yao.

  Hapa tunaongea unafiki. Kama huna kitu ndio watafungua vitabu kusoma hizo sheria. Hivi nyie mnaishi dunia ipi???Mimi naunga mkono wananchi wenye hasira ambao wanaona sheria hazifuatwi wafanye kweli.

  Naomba kuwasilisha.

   
 20. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  hawa wazee wote ni mafisadi. Hapo wanawaza, sijui koplo chacha ataleta shs ngapi leo jioni.
   
Loading...