IGP Mwema apongezwa kwa kusimamia haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema apongezwa kwa kusimamia haki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Feb 7, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  VIONGOZI 105 wa madhehebu mbalimbali ya dini kutoka nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na Kusini mwa Afrika wamemtaja Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jeneralali Saidi Mwema kuwa anashika nafasi ya kwanza katika kusimamia haki za raia na demokrasia.
  Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na viongozi hao wenye taaluma za utafiti, elimu, mazingira, haki za binadamu na maendeleo kutoka nchi za Burundi, Malawi, Uganda, Tanzania, Kenya, Kongo, DRC, Zambia na Rwanda wakati wa mkutano wao wa siku mbili wa kubadilishana utaalamu na uzoefu katika kutatua migogoro na kuchochea maendeleo kwa jamii.
  Mwenyekiti wa mkutano huo kutoka Uganda, Paulo Gabriel, aliwashambulia viongozi wa kisiasa katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu kwa kutengeneza migogoro, migomo, maandamano pamoja na kung’ang’ania madaraka.
  Gabriel aliwatahadharisha wanasiasa wa nchi za Maziwa Makuu na Afrika kumcha Mungu na kuacha kukodolea macho yanayotokea katika nchi za Misri na Tunisia, kwani hayo si mfano wa kuigwa badala yake waachane na kiburi cha kupenda madaraka yasiyoleta tija kwa wananchi.
  Naye Mchungaji Alex Alexander, Mchungaji Philip Kamau na Sheikh Akbar Mohamed kutoka Human Rights DR Congo, wamesema utafiti wao wa miaka minne katika nchi zote za maziwa makuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, chini ya Saidi Mwema, limeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa sehemu ya wananchi tofauti na wakuu wa majeshi ya polisi kwenye nchi hizo ambako polisi ni sehemu ya wanasiasa. “IGP Mwema ni mfano wa kuigwa, kwa umakini wake, kwani tumejifunza pia wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hapa Tanzania, ambapo wananchi walikuwa huru kupiga kura kwa utulivu mkubwa ingawa utulivu huo uliharibiwa na wanasiasa wenyewe wakati wa kuhesabu kura, tofauti na nchi nyingi ambako polisi hutumiwa na wanasiasa kuwalazimisha wapiga kura kuwapigia, jambo ambalo huleta machafuko ya kisiasa. SOSI: TANZANIA DAIMA
   
 2. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Yaani hawa jamaa HIZI TAARIFA ZA VURUGU ZA ARUSHA ZILIZOPELEKEA VIFO VYA WATU 3 AU ZAIDI KWA KUPIGWA RISASI ZA MOTO NA POLISI WA IGP MWEMA HAWAJAZISIKIA????????????

  Mambo mengine yanakera hata kuyasikia!! Huyu IGP Mwema kawapa hongo gani mpaka wamwone kuwa anastahili sifa hizo? Naona wote ni majuha tu!! Pambaf kabisa>
   
Loading...