IGP Mwema apangua wabaya wa MENGI

mwanadaresalaam

New Member
Nov 10, 2010
3
0
Wamo Nzowa na Mkumbo ambao siku za karibuni walitajwa na Mengi kutaka kumbambikia mwanae madawa ya kulevya...

karibuni...

MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, amefanya mabadiliko makubwa kwa makamanda wa Polisi wa mikoa na maofisa waandamizi ndani ya jeshi hilo.

Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana, zinasema IGP Mwema amefanya mabadiliko hayo ikiwa ni sehemu ya uboreshaji na utendaji kazi wa kila siku wa jeshi hilo.

“Ni kweli IGP Mwema amefanya mabadiliko makubwa yakianzia makao makuu ya jeshi hadi kwa makamanda wa polisi wa mikoa, nadhani nia ni kuboresha utendaji wa chombo hiki,” kilisema chanzo chetu.

Katika mabadiliko hayo, IGP Mwema amemhamisha Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), pia amemhamisha Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo, ambaye sasa anakwenda makao makuu.

Wengine waliokumbwa na uhamisho huo ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ambaye anahamishiwa makao makuu, wakati nafasi yake inachukuliwa na Charles Kenyela anayetoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Pia IGP Mwema amemhamisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, kwenda mkoani Arusha, wakati aliyekuwa kamanda wa mkoa huo, Basilio Matei, amehamishiwa makao makuu.

Taarifa zinasema, nafasi ya Kamanda Andengenye imechukuliwa na ofisa mmoja kutoka makao makuu aliyetajwa kwa jina la Mama Charo.

Rungu hilo limemwangukia pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, ambaye amehamishiwa makao makuu, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani.

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi (RCO) wa Mkoa wa Morogoro, Ahmed Msangi, amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo. Hadi tunakwenda mitamboni taarifa zinasema uhamisho huo umegusa zaidi ya maofisa 40.

Kaimu Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alipoulizwa kuhusiana na mabadiliko hayo, alikiri kuwapo na kusisitiza kuwa ni mabadiliko ya ndani.

“Mwandishi nakwambia mabadiliko haya yamefanyika, lakini ni ya ndani, yangekuwa ‘public’ (wazi) tungewaambia tu jamani… mbona hunielewi, tutawapa taarifa,” alisema Senso huku akitaka apigiwe simu baadaye.

Alipofuatwa ofisini kwake, kuelezea kuhusu mabadiliko hayo, aliendelea kushikilia msimamo wake huo huo.

Mabadiliko haya yamekuja mwezi mmoja tu baada ya Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kutoa madai mazito yaliyowahusisha maofisa wa juu wa jeshi hilo na njama chafu za kutaka kumbambikia mwanaye dawa za kulevya.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mengi aliwataja wahusika wa mpango huo uliotikisa nchi kuwa ni pamoja na mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya Kiasia, ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya EPA mahakamani.

Mengi alisema mfanyabiashara huyo ambaye hakumtaja jina, amefadhili mkakati huo kwa kuwahusisha baadhi ya maofisa wa polisi wa ngazi ya juu nchini na Polisi wa Kimataifa (Interpol), ambao kila mmoja angelipwa dola za Marekani 40,000, sawa na sh milioni 47. Aliwataja aliodai kuhusika katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kamishna wa Polisi Msaidizi wa kitengo cha kukabiliana na dawa za kulevya, Godfrey Nzowa, aliyeahidiwa dola za Marekani 40,000, sawa na sh mil. 47 na kulipwa dola za Marekani 20,000, sawa na sh mil. 23.5 kama malipo ya awali.

Mwingine ni ofisa wa polisi, Charles Mkumbo na polisi wa Interpol, aliyemtaja kwa jina moja la Henry. Wote waliahidiwa kiasi kama hicho cha Nzowa na kupata malipo ya awali yanayofanana.

Watuhumiwa wengine katika mpango huo ni maofisa wawili wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na ofisa kutoka kampuni moja ya simu za mkononi ambao hata hivyo hakuwataja kwa majina. Hao wanadaiwa kuahidiwa kulipwa sh mil. 15 na wote walilipwa malipo ya awali ya sh mil. saba kila mmoja.

Akijibu tuhuma hizo, Nzowa, kwanza alishangaa kusikia taarifa hizo na kuongeza kuwa katika kipindi alichotaja Mengi alikuwa nje ya nchi kikazi.

“Kwanza mimi katika kipindi anachotaja Mengi sikuwepo nchini. Lakini pia sijui kama Mengi au huyo mwanae wananijua. Binafsi huyo mwanae wala simjui, sasa sijui nimehusikaje hapa,” alisema Nzowa.

Alisema kauli ya Mengi ina lengo la kumchafulia jina lake, kwani kiasi anachokitaja ili kumhujumu mwanae ni kidogo sana ikilinganishwa na ahadi alizowahi kupewa na wahalifu, lakini alizikataa na kusimamia misingi ya sheria.

Kwa upande wake, Kamanda Mkumbo, naye aliruka ‘kimanga’ kwamba hajawahi wala hawezi kuthubutu kumbambikia dawa za kulevya mtu, kwa sababu ya kulipwa pesa.

“Mimi kwanza huyo mtoto wa Mengi simjui na hata sasa sijui tuhuma hizi zinatokea wapi. Hata mbele ya Mwenyezi Mungu niko tayari kukana kuhusika na mpango huo,” alisema.

Kamanda huyo alisema anashangazwa zaidi kuhusishwa na Nzowa kwenye mpango huo, kwani vitengo vyao havihusiani kikazi.

Chanzo:Mwananchi
 
Last edited by a moderator:
Dawa ni kuwapiga chini, na kuwafungulia kesi. Kwani ile tume ya Mwema kuchunguza sakata la Mengi matokeo ni lini? na kuwahamisha watuhumiwa sio kuvuruga hali ya hewa?
 

mi mzee mengi namwamini haongeagi bila evidence.
Sasa hapo ndo utajua serikali ya kitu kidogo...NO ACTION zaidi ya uhamisho.
Sasa huko makao makuu wanapelekwa wakafanye nini? mwema anaogopa kikundi cha watu wadogo kama hao?? Fukuza kazi mazima wakileta mgawanyiko tunawapiga detention wakakae vijijini kwao milele.
Hao bado ni watu wadogo sana katika usalama wa taifa letu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom