IGP Mwema apangua jeshi la Polisi, ahamisha vigogo wa juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema apangua jeshi la Polisi, ahamisha vigogo wa juu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema ambaye amefanya mabadiliko ya uongozi wa jeshi hilo kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri wa kazi ya ulinzi wa amani na usalama nchini.

  *KIKOSI CHA USALAMA CHAPATA BOSI MPYA

  MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema amefanya tena mabadiliko ya uongozi kwenye jeshi hilo, lakini safari hii akitupia jicho zaidi kwenye Kikosi cha Usalama Barabarani na maofisa wa vitengo, kikiwemo cha habari...
  Mabadiliko hayo ya viongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani yamekuja siku chache baada ya Mwema kufanya mabadiliko makubwa ya makamanda wa mikoa katika kipindi ambacho wimbi la ujambazi linaonekana kuanza kurejea kwa kasi.

  Msemaji mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika alisema jana kuwa katika mabadiliko mapya, Mwema amemteua Kamishna Msaidizi Mohammed Mpinga kuwa kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani badala ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi James Kombe ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sheria.

  Kamanda Mssika alisema kuwa nafasi ya Kamanda Mpinga inachukuliwa na mkuu wa usalama barabarani mkoani Pwani, Mrakibu Mwandamizi Johansen Kahatano. Kabla ya uteuzi huo, Kamanda Mpinga alikuwa ni afisa mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

  Katika mabadiliko hayo, Mwema amemteua Mrakibu Msaidizi Advera Senso kuwa msemaji msaidizi wa polisi badala ya Mrakibu Suzan Kaganda, ambaye amehamishiwa Kanda ya Dar es Salaam kuwa msaidizi wa kitengo cha masuala ya operesheni.

  Wengine waliohamishwa ni ofisa mnadhimu wa mkoa wa Tanga, ACP Simon Mgawe ambaye anakwenda makao makuu ya Polisi, wakati mkuu wa usalama barabarani mkoani Kigoma, SSP Salehe Mbaga anakwenda kuwa mkuu mpya wa usalama barabarani mkoa wa Pwani.

  Kamanda Mssika alisema kuwa mkuu wa upelelezi wa Kikosi cha Reli, Mrakibu Adolphina Kapufi sasa anakuwa ofisa mnadhimu wa mkoa wa Tanga na nafasi yake inachukuliwa na SP Sebastian Mbutta kutoka upelelezi mkoani Singida.

  Alisema SP Robert Masanja, ambaye ni mkufunzi Chuo cha Polisi CCP Moshi, sasa anakuwa mkuu wa polisi wilayani Songea mkoani Ruvuma. Awali nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na ASP Marco Joshua ambaye sasa anahamishiwa ofisi ya kamanda wa mkoani Ruvuma.

  Kamanda Mssika aliwataja maafisa wengine waliohamishwa kuwa ni ASP Anthony Masonzu, anayetoka makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani kwenda makao makuu ya Polisi wakati mkuu wa kitengo hicho mkoani Kigoma, Mrakibu Msaidizi William Mkonda ameteuliwa kukaimu nafasi ya mkuu wa kitengo hicho mkoani Kigoma.

  Kamanda Mssika alisema kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga zaidi katika kuboresho ufanisi katika kutoa huduma za polisi kwa jamii.

  CHANZO: MWANANCHI
   
Loading...