IGP, Mauaji yaliyotokea Dar Free Market yachunguze kwani kuna utata mwingi

Namba7

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
763
1,000
Jana RPC wa Kinondoni alikiri kutokea kwa mauaji maeneo ya Mtaa wa Tunisia na Ali Hassani Mwinyi, karibu na Dar Free Market.

Mauaji haya kwa mujibu wa RPC yalitokea baada ya askari waliokuwa doria kusikia kelele za mwanamke akipiga kelele kuwa ameiniwa simu na majambazi yaliyokuwa na silaha.

Askari waliokuwa doria na walivaa kiraia waliposikia waliwakimbilia na wakati wakiwakimbilia wale majambazi walianza kurusha risasi ndipo askari nao wakajibu mashambulizi hatimaye walifanikiwa kuua jambazi mmoja.

Kamanda Sirro, habari hii ina ukakasi mwingi kama ifuatavyo;

1. Jambazi kutumia silaha kuiba simu wasiojua thamani yake kwa kutumia silaha...hii haiingii akilini.

2. Jambazi waibe tena wako na pikipiki halafu askari wapate wasaa kumdadisi mwanamke alichoibiwa then wawakimbilie jambazi wakiwa na pkpk tena usiku na wafanikiwe kuwashika...hapa labda walianza kuwafukuza baada ya kuua ndipo walimrudia mwana mke aelezee mkasa.

3. Inasemekana kuwa aliyeuwawa alipewa simu na askari mmoja kati ya hawa wanaotajwa kutekeleza mauji akamsaidie kuiflash lkn kijana haikuirudisha kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa amemtapeli asakari na ndipo akaamua kutengeneza sinema hii ya mauaji ya kisasi.

Japo inasemekana ana tabia ya udokozi laki sio jambazi.

Kwa muktadha huu nashauri uchunguzi ufanyike, ikiwa walipeana simu na aliyepewa hakuirudisha na anapatikana, badala ya kuua kulikuwa na nafasi ya kumchulia hatua ya kisheria na sio kuua.
 

Namba7

JF-Expert Member
Nov 12, 2020
763
1,000
Ni mwizi hakuna uchunguzi wala nini akaendelee kuiba huko kuzimu kwa ninihakutaka kuvuja jasho mwizi ni mwizi tu iwe mdokozi au vinginevo hakuna kumtetea hapa
Hivi kila mtu akiamua kujichukulia sheria mkonomni hivi hii nchi patatosha?
 

Rcrusso Jr

Member
Jul 26, 2020
82
150
Mdogo wangu ni mkazi wa Goba, juzi jmos tunamshukuru Mungu kwa nafasi nyingine ya uhai wake.. mana ni simu,pc na bag lake kibaka/mwizi hakujali thamani ya kijana huyu.. kifupi ni kwenye daladala ya makumbusho via Goba alikaa na mtu kumbe ni mwizi, alimpulizia kitu dogo akapoteza network (hakika ni kikali mana mpaka leo bado hayuko sawa).

inavyoonekana alijifanya kumjua dogo akashuka nae kama anamsaidia baada akamtelekeza (njia nne) na watu wakawa wanahisi ni mlevi..hakupata msaada mpaka saa moja asubuhi akaweza tamka tu neno moja mtaa wa nyumbani ndipo boda boda wakajishauri wamlete mtaa huo walipofika tu wakaelekezwa nyumbani..

Hivyo mwizi ni mwizi hajui thamani ya uhai wako na wala hana kipimo cha kukudhuru mradi apate atakacho .. na wafe tu hata ikawaje
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,598
2,000
Jana RPC wa Kinondoni alikiri kutokea kwa mauaji maeneo ya Mtaa wa Tunisia na Ali Hassani Mwinyi, karibu na Dar Free Market.

Mauaji haya kwa mujibu wa RPC yalitokea baada ya askari waliokuwa doria kusikia kelele za mwanamke akipiga kelele kuwa ameiniwa simu na majambazi yaliyokuwa na silaha...
Kwahiyo unatetea ujambazi sio?
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
12,112
2,000
mdogo wangu ni mkazi wa goba,juzi jmos tunamshukuru Mungu kwa nafasi nyingine ya uhai wake.. mana ni simu,pc na bag lake kibaka/mwizi hakujali thamani ya kijana huyu....
Daah kina jirani yangu nae kapigwa kama hivyo,anafanya mishe za Tigo pesa,jamaa kampulizia madawa,kakomba kila kitu.
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,836
2,000
Jana RPC wa Kinondoni alikiri kutokea kwa mauaji maeneo ya Mtaa wa Tunisia na Ali Hassani Mwinyi, karibu na Dar Free Market.

Mauaji haya kwa mujibu wa RPC yalitokea baada ya askari waliokuwa doria kusikia kelele za mwanamke akipiga kelele kuwa ameiniwa simu na majambazi yaliyokuwa na silaha...
Ubaya askari wetu shule hawana, kufanya mission hata ndogo kiasi gani hawawezi....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom