IGP Mangu: Muda wowote tutamkamata Maalim Seif kwa uchochezi, anayetaka ya Lugumi akaliulize Bunge

Mangu:Zipo taratibu zinaendelea kufanyika kukabiliana na changamoto hii,tumeanza na mkoa wa kipolisi wa kinondoni kwa majaribio, pia kinondoni ni mkoa unaoongoza kiuhalifu.
 
Tiddo: Mmefikia wapi kukabiliana na matatizo yaliyotokea Tanga na mwanza?
 
Mangu: Baadhi ya watuhumiwa wameanza kukamatwa, na kufikishwa mahakamani
 
Tiddo: Kwanini matukio yasiyo ya kawaida yanatokea siku hizi hapa Tanzania
 
Mangu: Tanzania sio kisiwa, hata Kenya matukio ya namna hii yametokea, huu ni ujumbe kuwa tusibweteke, tunapanga mipango ya kukabiliana nayo.
 
Ha ha ha,jamaa yuko makini,majibu mafupi na ya kutosheleza kuogopa asije kusema ndivyo sivyo magazeti yakapata la kuandika
 
Mangu: Tanzania sio kisiwa, hata Kenya matukio ya namna hii yametokea, huu ni ujumbe kuwa tusibweteke, tunapanga mipango ya kukabiliana nayo.


Mkuu endelea kutupa update maana wengine tupo mbali na tv
 
Tiddo: Hivi viashiria vya hali ya uhalifu mnafanya nini kuhakikisha mnavidhibiti hali hiyo?
 
Mangu: Siwezi kusema uwezo wetu wa kukabiliana na adui yetu kwa uwazi, hii ni siri, ila tunabadilishana taarifa na wenzetu mbalimbali kwenye taifa na nje ya taifa. Watanzania wawe na amani sisi tupo imara dhidi ya wahalifu
 
Tiddo: Idara ya polisi imeelezwa kuwa ina vitendo vya rushwa kwa kiwango kikubwa, mmechukua hatua gani?
 
Mangu: Hali hii imepungua, sisi hatuvumilii vitendo vya rushwa, jamii inashawishi askari wetu kuchukua rushwa, hivyo jamii haitupi ushirikiano juu ya suala hili.Tunachukua hatua kali za kisheria kwa askari wetu wanaojihusisha na rushwa
 
Tiddo: huoni kuwa kuwa na maslahi mabaya, makazi mabaya ndio inapelekea polisi kujihusisha na rushwa?
 
Mangu: Polisi ambaye anamiliki mali kinyume na uwezo wake na isiyo na maelezo, tuletewe maelezo sisi tutachukua hatua. Polisi kumiliki mali si dhambi
 
Back
Top Bottom