IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,582
Wanabodi,

Hii ni kama barua ya wazi kwa mkuu mpya wa jeshi letu la Polisi, IGP, Kamanda Simon Sirro, kutoka kwa raia mwema, anayemtakia mafanikio mema katika majukumu yake kama IGP mpya, nikimsisitiza karma ya shedding an innocent blood under any circumstances, haijawahi kumwacha mtu salama, hivyo asiruhusu jeshi letu safi lichafuliwe na damu isiyo na hatia, karma yake haitalichapa jeshi la polisi au serikali, karma ya uovu huu itawachapa wahusika, na mabosi wao individually, walio toa amri, au kuona uovu huu ukitendeka na and do nothing as if nothing happened!.

Declaration of Interest.
Mimi ni mtoto wa polisi, Mzee wangu Andrew Mayalla (RIP) ndiye aliyekuwa RSO wa Mwanza wakati wa ile Kesi ya Mauaji Mwanza, ya mwaka 1976, hivyo ninaelewa mbinu mbalimbali za kipolisi za interrogations za watuhumiwa wa mauji!, hivyo nalijua vizuri jeshi letu la polisi.

Jeshi Letu la Polisi Safi.
Baada ya utambulisho wa mtoto wa polisi, kwa kuzingatia taarifa za mahojiano ya polisi kwenye kesi ya Uhani ya 1984, then nikisema jeshi letu safi la polisi, naomba mnielewe!, ni Nyerere alilisafisha, labda kama limechafuka tena!. Kwa vile kauli huumba, kila siku ukimwita mtoto kuwa ni mtoto mbaya, kauli hiyo ya mtoto mbaya inaumba ubaya, hivyo huyo mtoto anakuja kuwa mtoto mbaya kweli!. Hivyo kuliita jeshi letu la polisi kuwa ni jeshi letu safi la polisi, ni kutumia nguvu ya kauli za affirmatives, kwa kutumia affirmations kuliumbia usafi jeshi letu la polisi ambalo kiukweli sasa, limechafuka tena!, ingekuwa ni enzi za Mwalimu Nyerere, siku nyingi Waziri wa Mambo ya ndani, na IGP, wangesha staafishwa kwa manufaa ya umma, na yule kamanda aliyetangaza uzembe huo saa hizi saa nyingi angekuwa, ana...debe!. Kwenye ile Kesi ya Mauaji Mwanza, walikufa mahabusu wawili Mwanza, kuanzia waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa, Director wa TISS, Emelio Mzena, IGP Salmwel Pundugu, RC wa Mwanza Peter Kisumo, wote hawa waliwajibika!. Kisha RPC, OCD, RSO na DSO ndio wakashitakiwa kwa mauaji. Siku hizi kila uchao watu wanakufa kwa uzembe wa polisi, sijui ni mpaka watu wa idadi gani wafe ndipo watu wawajibike!.

Pongezi Kwa IGP, Kamanda Simon Sirro.
Naomba kuanza kwa kutoa pongezi kwa Kamanda Simon Siro kuteuliwa kuwa IGP, na pia kutoa pongezi kwa jeshi letu la polisi kwa kazi nzuri inayofanya kulinda raia na mali zao. Mimi binafsi nina imani sana na Kamanda Siro kwa good track record yake ndani ya jeshi hilo, na sura ya kipolisi tofauti na mtangulizi wake aliyekuwa na sura laini laini, matokeo yake jeshi letu nalo lilifanana nae kwa kuwa ni jeshi nyoronyoro kwa polisi wetu kuchinjwa kama kuku mchana kweupe!.
Mauaji ya Polisi Wetu ni Ujambazi au Ugaidi au Retaliation?. Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?, - JamiiForums

Natoa wito kwa IGP, Kamanda Simon Siro, asiruhusu uzembe kama huu ulioelezewa hapa, kwa mtuhumiwa wa mauaji, kufa akiwa mikononi mwa polisi, kizembe zembe namna hii kama ilivyoelezwa hapa ambako kunachafua jeshi letu safi la polisi!.

Shuhudia Kamanda Polisi Akithibitisha Kifo cha Mtuhumiwa Kwa Uzembe Bila Hata Blink of an Eye, As if ni Jambo la Kawaida!.


Japo aliyeuliwa ni mtuhumiwa wa mauaji, kwa maelezo yaliyotolewa hapo, nakuomba sana, IGP Kamanda Sirro, kamwe usiukubali blanket statements za uzembe kama huu, unless kifo cha mahabusu huyu ni utekelezaji wa lile agizo la Amiri Jeshi Mkuu, Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...

Nijuavyo mimi, mtuhumiwa yoyote mikononi mwa polisi, anapopelekwa popote isipokuwa mahakamani, anasindikizwa na ulinzi madhubuti wa askari wenye silaha za moto, na wakati wote anakuwa na pingu mikononi, anawezaje kutoroka hadi kupelekea kuuwawa mikononi mwa polisi?!.

Mazingira ya Polisi Kutumia Silaha Za Moto Kwenye Arrest
Nakiri kuyafahamu mazingira ambayo jeshi letu la polisi wanaruhusiwa kutumia silaha za moto katika arrest na kuzuia mtuhumiwa kutoroka akiwa mikononi mwa polisi, mazingira hayo nimeyazungumza katika bandiko hili.
Hivi polisi wameruhusiwa kuua wakihisi fulani ni mhalifu ...
nimesema

Asante Teles kwa kuibua issue hii. Kwa mujibu wa sheria yetu, hakuna mtu yoyote anaruhusiwa kuua bila shera kufuata mkondo wake. Hata wanao hukumiwa kifo, ni mpaka rais asaini.
Kinachofanywa na polisi wetu, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu ambao hawa polisi wetu hawazijui.

Kwa mujibu wa sheria penal code na criminal procedure, polisi anatakiwa kutumia reasonable force wakati wa kufanya arrest. Akitumia nguvu zaidi ili liable for prosecution.

Ziko sheria makini sana zinazoelekeza ni wakati gani polisi atatumia silaha kwenye arrest atempt, only mtuhumiwa ni armed na ikiwa imeelekezewa kwa polisi or on the chase na hideout.

Polisi pia anaweza kutumia silaha kuzuia jaribio la kutoroka kwa mtuhumiwa asiye na silaha. Hapa polisi anatakiwa kumpiga risasi miguuni ili isiweze kukimbia.

Kwenye kesi ya Uhaini ya 1982, wakili Murtaza Lakha, aliichachafya sana serikali mahakamani kufuatia kuuwawa kwa
Mtuhumiwa Martin Tamimu, ambaye alikuwa ni comandoo, alipozingirwa ili akamatwe, aliruka ukuta, akadandia pick-up up iliyokuwa kwenye mwendo kasi lakini hakuwa na silaha yoyote.
Mwenye pick-up alipogundua, akasimamisha pembeni, polisi wakaizingira hiyo pick-up, wakamiminia risasi 7 toka umbali wa meta 3!. Lakha akauliza hii ni arrest atempt gani polisi kupiga risasi 7 umbali wa mita 3 wakati risasi moja tuu ilitosha!.
Huu ni unyama wa polisi na kuna matukio mengi sana ya kutisha na kusikitisha yanayofanywa na polisi kuua raia wasio na hatia. Haya yanaripotiwa ni machache kati ya mengi yasiyoripotiwa.
Hii kesi ya Zombe, japo atashinda, inafungua milango ya polisi kuwa makini zaidi na kazi yao, vinginevyo mkono wa sheria ambao ni mrefu, utawakuta.


Hoja Mbalimbali Katika Mauaji ya Mahabusu Huyu
  1. Ni kweli mtuhumiwa alijaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi kwa kukimbia huku akiwa na pingu mikononi.
  2. Baada ya kupigwa risasi moja ya mguu, lazima alianguka chini. Mahabusu mwenye pingu mikoni, amepigwa risasi moja ya mguu, ameanguka chini, je ni nini kilimfanya apigwe risasi nyingine ya miguu, yaani miguu yote?!.
  3. Jee alipigwa hizo risasi mbili tuu miguuni ndizo zilizopekekea kifo kweli, au alimiminiwa risasi kadhaa na kuachwa a bleed to death?. Risasi mbili za mguu zinawezaje kusabisha kifo?.
  4. Nakijua kinachowapata watuhumiwa wanaojaribu kuroka mikononi mwa polisi, jee ni kweli baada ya kupigwa hizo risasi mbili, mtuhumiwa huyo, jee alipatiwa huduma yoyote ya kwanza kumzua as bleed to death na kumuwahisha hospitali?, au baada ya kumiminiwa risasi za kutosha, mtuhumiwa huyo pia 'alishughulikiwa' ipasavyo kama walivyoshughulikiwa watuhumiwa hawa kwenye kisa hiki, na kilichopelekwa Mt. Meru Hospital ni mwili tuu kwa ajili ya kupata taarifa ya dakitari?!. Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
  5. Vifo vyote vya mahabusu wowote mikononi mwa polisi, lazima vifuatiwe na independent inquiry, ili kujiridhisha, kufuatia huko nyuma jeshi la polisi kuwahi kuhusishwa kwa utesaji na mauji ya mahabusu kama ilivyotokea hapa katika kisa hiki, TISS ni Watekaji, Watesaji na Wauaji!. Wasijadiliwe na Bunge bali ...
  6. Huu nauita ni uzembe, kwa sababu nguvu iliyotumika kumdhibiti mahabusu huyo ni kubwa kuliko, mtu ana pingu mikononi, amepigwa risasi mguu moja, ameanguka chini, kwa nini afie mikononi mwa polisi badala ya kulinda maisha yake, apone awaonyeshe polisi washirika wake?!
  7. IGP, Kamanda Siro, wewe ni mtu wa kuaminika sana, kwa uadilifu na ushupavu usiotia shaka, nakuomba usikubali kirahisi rahisi taarifa za watendaji wako zenye makando kando kama haya, yanayoweza kupelekea karma repercussions za damu za watu zinazomwagika chini yako, zikaja kuwa juu yako!.
Hitimisho.
Lengo la bandiko hili, sio kulitaka jeshi la polisi kujibu chochote katika hoja hizi, bali ni angalizo tuu kutoka kwa raia mwema, anayekutakia mafanikio mema katika kazi yako, na weledi wa hali ya juu kwa jeshi letu la polisi haswa katika kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto nyingi za uhalifu wa kutumia silaha za moto, na silaha za kivita, na mauaji ya kisiasa kama kifo cha kamanda Mawazo, au mashambulio ya wanasiasa kama shambulio la Lissu, japo matukio mengine yana possibilities za friendly fires lakini polisi ndio mkanyooshewa vidole, hivyo jeshi lako la polisi ni lazima liwe na undendaji makini kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa usio tia shaka, na haswa katika kuwabaini watu wasiojulikana, kama wale waliomtishia Mhe. Nape bastola, ambao nao walikuja pale St. Peters kwa kutumia gari aina ya Nissan Patrol nyeupe, hadi picha zao zilitapakaa kwenye magazeti yote na video kwenye TV zote na mitandao ya kijamii, lakini jeshi letu la polisi bila aibu, linatangaza eti ni watu wasiojulikana!, lakini mko bize kufuatilia mitandao ya kijamii nani kasema nini, huku watu wanaojulikana, wakifanya uzembe wa wazi kabisa, mchana kweupe, lakini hakuna lolote linalofanyika!.

Wasalaam

Paskali.

Rejea

IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu ...
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
Unyama wa polisi Tanzania- walazimisha mtu kukubali video kwa ...
 
Nasikia alikuwa kasha mtaja askari mmoja wa FF kuwa alikuwa anashirikiana naye. Sasa kwa kifo cha kijana huyo basi hakuna kesi tena kwa huyo askari. Paskali nini maoni yako kuhusu hili?
 
Nasikia alikuwa kasha mtaja askari mmoja wa FF kuwa alikuwa anashirikiana naye. Sasa kwa kifo cha kijana huyo basi hakuna kesi tena kwa huyo askari. Paskali nini maoni yako kuhusu hili?
Ana maoni maana jeshi la polisi kwake ni safi kweli isiyokuwasha ujairamba hv unajua kuna watu wapo central mwenzi wa 4 huu hkn cha mahakamani wala nn hakika jeshi la polisi ili lipo kwa Ajiri kulinda serikali na viongozi wake sio raia paskali kaka yngu kwako lazima jeshi liwe safi maana jina na heshima ya baba yko kwa jeshi letu ndio inakulinda na familia yko...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli jeshi la polisi lina jukumu kubwa kulinda raia na mali zake.

Na niseme wazi tu, wapo askari waadilifu wanaotimiza majukumu yao kwa weledi. Hongera kwao.

Lakini nikiangalia upande mwingine naona jeshi lililojaa wauaji, watesaji na mambumbumbu.

Kuwa askari inapaswa iwe kielelezo cha wema na utii. Sio utii kwa wanasiasa bali sheria za nchi tulizojitungia ili kutuongoza.

Yanini askari unajaa kiburi na kugandamiza raia hata kwa mambo yakutumia akili tu?

Ukiona askari hayupo upande wa wananchi na anaona sana tu kuua, kujeruhi na kudhalilisha hapo maana yake huyo askari ni mbumbumbu na viongozi wake pia ni mbumbumbu
 
Nimemsikia mkuu leo kasema hukumu za kunyonga wasimpelekee.. Sasa huyu kijana binafsi nadhani anatahiki kunyongwa mpaka kufa... Kwa kua hatuwezi kutekeleza hukumu kama hizo nadhani Polisi wako sawa tu! Shida yangu na Polisi siku hizi ni jinsi wanavyotumika kisiasa kutekeleza agenda za mtukufu za kuua upinzani!
 
Nasikia alikuwa kasha mtaja askari mmoja wa FF kuwa alikuwa anashirikiana naye. Sasa kwa kifo cha kijana huyo basi hakuna kesi tena kwa huyo askari. Paskali nini maoni yako kuhusu hili?

Inawezekana maana Mzazi mmoja alitoa fungu akaambiwa umeshatoa taarifa polisi utamkuta mtoto shimoni.Ni nani aliyempelekea information mtuhumiwa??

Polisi haijawahi kuwa SAFI hata siku moja.Wanapenda sana kubambika kesi.
 
Back
Top Bottom