IGP, huyu RPC Shana analifedhehesha Jeshi pamoja na kumuonya

Mshangai

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
468
1,086
Jeshi huwa na nidhamu yake, lakini kumuona kamanda ana simama hadharani anakatakatà mauno hovyo ni fedheha kubwa.

Tunakumbuka ulipoongea na ma RPC wote miezi michache iliyopita tunakumbuka ulitoa onyo kwa tabia za namna hii kwa makamanda.

Sasa jee Shana anakudharau kuwa humuwezi? Huyu si ndiye alisindikiza zile dhahabu kule Mwanza kilicho muokoa ni ukada wa chama tawala?

Je, haya anafanya kwa vile ni kada?

 
Acha kukariri mambo. Polisi ni jeshi la wananchi, ni lazima waonyeshe ukaribu na wananchi. Kama kamanda wa Police ana jukumu la kutengeneza uhusiano mwema na Raia. Kupitia hafla kama hizi ni lazima ajichanganye na watu
Uniform za Jeshi zina heshima na masharti yake tofauti na sare za CCM au CDM. Kamanda kukatika hadharani ndani ya sare ni kinyume cha taratibu acheni kutetea upuuzi.
 
Uniform za Jeshi zina heshima na masharti yake tofauti na sare za CCM au CDM. Kamanda kukatika hadharani ndani ya sare ni kinyume cha taratibu acheni kutetea upuuzi.
Wakati mwingine hupaswi kujiuliza jeshi letu la polisi liitwapo polisisiemu!!! Aidha baadhi ya makamanda wake hawajui kwamba wanaitumikia nchi ama si hivyo basi wanakuwa wameteuliwa toka yuuviisisiemu ili wakatumikie jeshi kwa maslahi ya chama chao na "ukatuni" badala ya kufuata weledi na misingi ya kazi...
Ogopa sana ukikuta jeshi la polisi linashiriki siasa...
 
Samahani,kama ni kosa askari kufurahi,band ya jeshi nayo ipo ki makosa?
Wewe nyumbani kwako kama ni baba basi kwa vile umenunua radio huwezi kuonyesha tofauti na watoto kwenye kunengua kisa umenunua?
Tunamzungumzia kamanda boss!
 
Back
Top Bottom