IGP Wambura, Jeshi la Polisi lilihitaji taswira mpya ya kiuongozi na kiutendaji

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Emmanuel Kalule
20.07.2022

Leo mapema majira ya saa nane usiku, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi ya Polisi nchini kwa kumteua aliyekua Kamishna wa Polisi Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu mpya wa Jeshi la polisi nchini (IGP).

IGP Wambura akichukua nafasi ya Simon Sirro (Mstaafu)ana jukumu kubwa la kuigeuza taswira ya jeshi hilo na kuhakikisha Jeshi la Polisi nchini linabaki kuwa kiungo muhimu cha kuhakikisha linatetea haki za kila raia na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

IGP Wambura kitaaluma na kiutendaji ni mpelelezi aliyebobea, na weledi katika nyanja ya upelelezi ilionekana tangu enzi za Alfred Tibaigana akiwa Kamanda wa Polisi DSM ambapo kila alipoingia katika jukumu alifanikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu kwa asilimia 100%, ni mara chache sana kuikuta kasoro ndani ya kazi ya Kamishna Wambura.

Hii ilipelekea Rais Samia kumpandisha cheo na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya jinai nchini (DCI).

Kuunganisha utendaji kazi wa vyombo mbalimbali vya haki-jinai nchini ndio jukumu mojawapo la DCI, ambapo taswira ya upepelezi kukamilika kwa wakati, kupotea kwa kesi za kubambikiana, kupotea kwa kesi za wizi wa mtandao na kupungua kwa kesi za mitandao kukaonekana chini ya uongozi wa Wambura kama DCI.

Haya yakiwa ni malalamiko makubwa kwa muda mrefu kutoka katika makundi mbalimbali ya watu nchini, sasa muarobaini ukawa ni Wambura kuwa DCI, na hii leo anaposhika kijiti cha u-IGP, ni kwa imani kuwa taswira ya Jeshi la Polisi inaenda kubadilika na kuwa chombo chenye kusimamia haki za wananchi ipasavyo.
 
Kila la kheri kikubwa hakibitendeke ikizingatiwa pia moja ya tofauti zetu ni mavazi.
 
RC wa Mwanza alipukutwa usiku wa manane na huyu ameteuliwa usiku wa manane kweli serikali hailali.
 
polisi pale kunduchi mtongani wanakula rushwa hadharani.
akaanza na afande JOHN Wa mtongani kunduchi
 
IGP Wambura akichukua nafasi ya Simon Sirro (Mstaafu)ana jukumu kubwa la kuigeuza taswira ya jeshi hilo na kuhakikisha Jeshi la Polisi nchini linabaki kuwa kiungo muhimu cha kuhakikisha linatetea haki za kila raia na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Kwa kinywa chake amesema kuhakikisha viongozi hawasumbuliwi
 
Hapa IGP tumepata
Usiweke sana matarajio kwa mtu.Mifumo yetu ni mibovu sana kiasi ambacho kinawapa wakati mgumu watu wazuri kuperfom kwenye maeneo wanayopata kuhudumu.Kuna mambo ambayo ubora wa mtu mmoja mmoja hauwezi kuonekana kama system nzima iko vibaya.Jeshi la polisi ni mojawapo ya maeneo ambayo yanahitaji kufumuliwa nakusukwa upya.
 
Emmanuel Kalule
20.07.2022

Leo mapema majira ya saa nane usiku, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi ya Polisi nchini kwa kumteua aliyekua Kamishna wa Polisi Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu mpya wa Jeshi la polisi nchini (IGP).

IGP Wambura akichukua nafasi ya Simon Sirro (Mstaafu)ana jukumu kubwa la kuigeuza taswira ya jeshi hilo na kuhakikisha Jeshi la Polisi nchini linabaki kuwa kiungo muhimu cha kuhakikisha linatetea haki za kila raia na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

IGP Wambura kitaaluma na kiutendaji ni mpelelezi aliyebobea, na weledi katika nyanja ya upelelezi ilionekana tangu enzi za Alfred Tibaigana akiwa Kamanda wa Polisi Dsm ambapo kila alipoingia katika jukumu alifanikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu kwa asilimia 100%, ni mara chache sana kuikuta kasoro ndani ya kazi ya Kamishna Wambura.

Hii ilipelekea Rais Samia kumpandisha cheo na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya jinai nchini (DCI).

Kuunganisha utendaji kazi wa vyombo mbalimbali vya haki-jinai nchini ndio jukumu mojawapo la DCI, ambapo taswira ya upepelezi kukamilika kwa wakati, kupotea kwa kesi za kubambikiana, kupotea kwa kesi za wizi wa mtandao na kupungua kwa kesi za mitandao kukaonekana chini ya uongozi wa Wambura kama DCI.

Haya yakiwa ni malalamiko makubwa kwa muda mrefu kutoka katika makundi mbalimbali ya watu nchini, sasa muarobaini ukawa ni Wambura kuwa DCI, na hii leo anaposhika kijiti cha u-IGP, ni kwa imani kuwa taswira ya Jeshi la Polisi inaenda kubadilika na kuwa chombo chenye kusimamia haki za wananchi ipasavyo.
Polisi na mfumo mzima wa haki jinai Tanzania umeoza hata ateuliwe malaika hawezi fanya lolote. Kabla hayajakukuta huwezi jua ila siku yakikukuta ndio utajua mateso uonevu na adha iliyoko kule hakuna Cha IGP mpya Wala wa zamani mfumo mzima ni hopeless
 
Back
Top Bottom