KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Chagga pare ndio hao hao tu,sawa sawa na malindi na kikwajuni wote wazanzibariHawa wangekuwa wanaitwa:
Peter Tarimo na Alfonsi Tarimo jeshi la polisi lote lingeitwa la Wachaga.
Chagga pare ndio hao hao tu,sawa sawa na malindi na kikwajuni wote wazanzibariHawa wangekuwa wanaitwa:
Peter Tarimo na Alfonsi Tarimo jeshi la polisi lote lingeitwa la Wachaga.
Una rekodi za utendaji wao mkuu ili kukazia msimamo wako??!!!!
mkuu nia yangu ni kuchokoza mada ili tufike mahali tuache propaganda zisizo na maana tuache mambo ya udini ukabila na haya mambo ya rika yanayochipukia kwa kasi
Taarifa ya IGP ya uteuzi wa Makamanda wa Polisi wa Mwanza, Mbeya na Simiyu
08/12/20130 Comments
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amefanya uteuzi wa Makamanda wa Polisi kwa Mikoa mitatu Mwanza, Mbeya na Simiyu, ambapo amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Tarime Rorya amehamishiwa Tunduru kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Source: Taarifa ya IGP ya uteuzi wa Makamanda wa Polisi wa Mwanza, Mbeya na Simiyu - wavuti.com
Hulijui jeshi la polisi la Mwema,ni UPARE kwa kwenda mbele.
Huyu Mkumbo si ndiye yule aliyekuwa na figisu figisu na Mengi au?
Mwema, Msuya, Mlasani, Msangi Chagonja.hawa watu ni makini na wanastahili utumishi uliotukuka.
msangi mbeya ni pagumu sanaaaaaaa, sio dar kuna wanyia wana roho ngumu wanakata vichwa
Athuman diwani kimepanda ameamia makao makuu Dar
Huyo msangi mng'a meno na kucha huko mbeya tayari muandike maumivu na muwe mnatembea na ganzi.
Viva home boy mkumbo.
Mwema, Msuya, Mlasani, Msangi Chagonja.hawa watu ni makini na wanastahili utumishi uliotukuka.
sio huyo, huyu ni mwingine. Yule yuko udsm-education.