IGP angalia huu uonevu wa Askari wa Usalama Barabarani

Nairobian

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
873
2,281
Nilikuwa natokea Mlimani City, kufika mataa ya mwenge, kukawa na magari matatu mbele yangu. Taa ziliporuhusu Polisi pale wakatupiga mkono ilikuwa kati ya 5 seconds. Wa mbele yangu na mimi, Ina maana kwamba, aliyetoa mbele yangu na mimi tulikamatwa na kuchajiwa 60,000 kila mmoja. Yaani ni Gari mbili tu ziliruhusiwa.

Ninachishindwa kuelewa, ni Kwa nini hawa watu wa program traffic lights Kwa sekunde 5? Hii ni kuwakomoa wananchi au kuongeza mapato? IGP Tafadhali Angalia hii swala. Wananchi wananyanyaswa mno barabarani
 
Kumbe wewe ni mlalahai? nilifikiri mlalahoi kama watanzania.IGP zidi kukamua tulikondeshe daraja la walionacho na wasionacho.
Apana mkuu. hoja ya nduguyetu yawezakuwa ya msingi. walalahai nao wanahaki sawasawa na sie walalahoi.

Whatever is gonna be, itifaki izingatiwe. na kila class litendewe haki.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Wanaoprogram Taa ni Halmashauri ya Manispaa husika sio Trafiki.
Kama ulipita wakati taa hazikuruhusu ni Kosa Kisheria.
 
We unalalamika taa?halafu jamaa wanajua kabisa hapa makosa yatafanyika wanakaa na max malipo zao
Kuna mtu hakupiga msuaki alichajiwa !!makusanyo yao 75% ni dhuluma kabisa watu wanatoa kwa kinyongo
 
Kumbe wewe ni mlalahai? nilifikiri mlalahoi kama watanzania.IGP zidi kukamua tulikondeshe daraja la walionacho na wasionacho.

Mawazo ya kimasikini, typical poor human being. Badala ya kutaka watu wengi watoke kwenye umasikini waingie kwenye utajiri unashabikia wenye pesa wakifilisiwa, mzunguko wa pesa bongo mdogo kutokana na market kubwa kua ya watu masikini, linganisha na nchi kama UK ambayo middle class ni wengi pesa inazunguka sana in the end millionaires kibao, na ajira pia kibao. Yaani watanzania mnajiroga wenyewe, mnapenda sana kuona tajiri anapigwa doro, mkiwa level moja mnafurahi sana, sasa kesho yake atakayekupa ajira nani? au ukifungua biashara utakayemuuzia nani kama wote wamekua masikini?
 
Traffic police kwa sasa ni tatizo. Juzi nimelipishwa 30,000 kwa vile nilibeba tank tupu jipya la maji kwenye landcruzer pickup kwa vile tank lilitokeza kama cm 8 hivi juu ya cabin, wakadai mzigo umebebwa kwa njia hatarishi. Nilipomwuliza ni hatari gani, hakuweza kusema badala yake akasema itabidi anipeleke kituo cha polisi kwa vile nabishana naye. Nilitoa kuondoa usumbufu. Maana hata ukienda kituoni, ni nadra sana waliopo ofisini kufanya tofauti na matakwa ya waliopo barabarani.

Iliniuma sana, kwa kufikiria kuwa ni polisi hawa hawa, mara mbili, kwa wakati tofauti, nilinunua mafuta kujaza kwenye gari zao ili wasafirishe miili ya wenzao waliokuwa wamefariki lakini ofisi yao haikuwa na fedha za kununua mafuta ya gari. Wakati sisi tunathamini ubinadamu wao, traffic wanafanya kazi kwa kutukomoa!
 
Nilikuwa natokea Mlimani City, kufika mataa ya mwenge, kukawa na magari matatu mbele yangu. Taa ziliporuhusu Polisi pale wakatupiga mkono ilikuwa kati ya 5 seconds. Wa mbele yangu na mimi, Ina maana kwamba, aliyetoa mbele yangu na mimi tulikamatwa na kuchajiwa 60,000 kila mmoja. Yaani ni Gari mbili tu ziliruhusiwa.

Ninachishindwa kuelewa, ni Kwa nini hawa watu wa program traffic lights Kwa sekunde 5? Hii ni kuwakomoa wananchi au kuongeza mapato? IGP Tafadhali Angalia hii swala. Wananchi wananyanyaswa mno barabarani

Hawezi kukusikia mkuu. Hiki kikombe yeye hakimkuti. Yeye hatokaa akamatwe na kosa la usalama barabarani. Kwako yeye ni kama dua la kuku.

Kero za askari wa usalama barabarani ni ajenda muhimu kujipatia ushindi katika chaguzi katika nchi hii.

Vyama vya siasa pamoja na kudai katiba mpya ahadi ya kuwapiga chini hawa jamaa waliowekeza katika manyanyaso, rushwa, dhuluma, ufedhuli n.k barabarani, kwaweza kuwa ni mtaji wa maana kabisa katika kujipatia kura za kutosha.
 
Nilikuwa natokea Mlimani City, kufika mataa ya mwenge, kukawa na magari matatu mbele yangu. Taa ziliporuhusu Polisi pale wakatupiga mkono ilikuwa kati ya 5 seconds. Wa mbele yangu na mimi, Ina maana kwamba, aliyetoa mbele yangu na mimi tulikamatwa na kuchajiwa 60,000 kila mmoja. Yaani ni Gari mbili tu ziliruhusiwa.

Ninachishindwa kuelewa, ni Kwa nini hawa watu wa program traffic lights Kwa sekunde 5? Hii ni kuwakomoa wananchi au kuongeza mapato? IGP Tafadhali Angalia hii swala. Wananchi wananyanyaswa mno barabarani
Hakuna namna ni kulipa mkuu
 
Mkuu ulikua unatokea upande gani taa zikaruhusu kwa sekunde 5, maana ile yellow light ndio hukaa kama sekunde 10.
 
Traffic police kwa sasa ni tatizo. Juzi nimelipishwa 30,000 kwa vile nilibeba tank tupu jipya la maji kwenye landcruzer pickup kwa vile tank lilitokeza kama cm 8 hivi juu ya cabin, wakadai mzigo umebebwa kwa njia hatarishi. Nilipomwuliza ni hatari gani, hakuweza kusema badala yake akasema itabidi anipeleke kituo cha polisi kwa vile nabishana naye. Nilitoa kuondoa usumbufu. Maana hata ukienda kituoni, ni nadra sana waliopo ofisini kufanya tofauti na matakwa ya waliopo barabarani.

Iliniuma sana, kwa kufikiria kuwa ni polisi hawa hawa, mara mbili, kwa wakati tofauti, nilinunua mafuta kujaza kwenye gari zao ili wasafirishe miili ya wenzao waliokuwa wamefariki lakini ofisi yao haikuwa na fedha za kununua mafuta ya gari. Wakati sisi tunathamini ubinadamu wao, traffic wanafanya kazi kwa kutukomoa!
Tenda wema nenda zako, hayo ndiyo madhara ya kusubiri shukrani! Elfu 30 unapiga mayowe hivi, kweli unaweza kujaza mafuta kwenye gari la msiba wewe?
 
Nilikuwa natokea Mlimani City, kufika mataa ya mwenge, kukawa na magari matatu mbele yangu. Taa ziliporuhusu Polisi pale wakatupiga mkono ilikuwa kati ya 5 seconds. Wa mbele yangu na mimi, Ina maana kwamba, aliyetoa mbele yangu na mimi tulikamatwa na kuchajiwa 60,000 kila mmoja. Yaani ni Gari mbili tu ziliruhusiwa.

Ninachishindwa kuelewa, ni Kwa nini hawa watu wa program traffic lights Kwa sekunde 5? Hii ni kuwakomoa wananchi au kuongeza mapato? IGP Tafadhali Angalia hii swala. Wananchi wananyanyaswa mno barabarani
Kalipe faini, acha kulalamika, sekunde tano hata huyo wa kwanza asingetoka, IGP ana akili timamu, anajua maana ya sekunde tano.
 
Nilikuwa natokea Mlimani City, kufika mataa ya mwenge, kukawa na magari matatu mbele yangu. Taa ziliporuhusu Polisi pale wakatupiga mkono ilikuwa kati ya 5 seconds. Wa mbele yangu na mimi, Ina maana kwamba, aliyetoa mbele yangu na mimi tulikamatwa na kuchajiwa 60,000 kila mmoja. Yaani ni Gari mbili tu ziliruhusiwa.

Ninachishindwa kuelewa, ni Kwa nini hawa watu wa program traffic lights Kwa sekunde 5? Hii ni kuwakomoa wananchi au kuongeza mapato? IGP Tafadhali Angalia hii swala. Wananchi wananyanyaswa mno barabarani
Na pale Agha Khan mjini kuwa makini ,style hiyo hiyo
 
Apana mkuu. hoja ya nduguyetu yawezakuwa ya msingi. walalahai nao wanahaki sawasawa na sie walalahoi.

Whatever is gonna be, itifaki izingatiwe. na kila class litendewe haki.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mkuu Wa nchi akiagiza ni amri. Lazima muishi kama mashetani. Au hujui ?
 
Back
Top Bottom