IGP amwaga vyeo polisi, Askari zaidi ya 500 wanufaika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP amwaga vyeo polisi, Askari zaidi ya 500 wanufaika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, May 6, 2010.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,006
  Trophy Points: 280
  IGP amwaga vyeo polisi, Askari zaidi ya 500 wanufaika Wednesday, 05 May 2010 22:41 0diggsdigg

  Boniface Meena
  JESHI la Polisi limepandisha vyeo maafisa wa kati na juu zaidi ya 200 na kuwapangia kati ya hayo majukumu mapya.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ya kuaminika kutoka ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi zinasema kwamba zaidi ya mainspekta wasaidizi 200 wamepandishwa vyeo na kuwa mainspekta kamili, wakati askari wengine 347 wamepelekwa kusomea nyota katika Chuo Kikuu cha Polisi tokea wiki iliyopita.

  Vilevile, chanzo cha habari hii kimeeleza Mwananchi kwamba zaidi ya Waratibu Waandamizi zaidi ya 20 wamepandishwa vyeo kuwa makamishina wasaidizi wa jeshi hilo.

  Katika mabadiliko hayo, askari waliopandishwa vyeo wamepangiwa kuwa makamanda wa polisi wa wilaya na wengine wakuu wa upelelezi wa mikoa.

  Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa, Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP), Said Mwema alikuwa atangaze mabadiliko hayo jana mbele ya vyombo vya habari, lakini kutokana na Mkutano wa Uchumi wa Dunia(WEF), ulioanza jana alisimamisha zoezi hilo.

  Pia askari 347 wamepelekwa chuoni kusomea nyota kuanzia Aprili 30 mwaka huu na wanaendelea na masomo.

  Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Abdallah Mssika alipotafutwa na kuzungumzia taarifa hizi hakupatikana katika namba zake zote mbili ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi.

  Lakini wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, Mssika alipatikana na alipoanza kuulizwa kuhusu mabadiliko hayo simu ilikata na alipopigiwa tena simu haikupatikana.

  Baadaye Mwananchi iliwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ambaye alisema ni jambo la kawaida askari kupandishwa vyeo na kwamba angemwagiza Msemaji wa Polisi aweze kuutangazia umma.

  "Kwa sasa nipo nje ya ofisi na kesho nitamwagiza msemaji awape taarifa," alisema Mwema.

  Mabadiliko hayo yamekuja siku chache baada ya IGP Mwema hivi karibuni kufanya tena mabadiliko ya uongozi kwenye jeshi hilo, lakini safari hiyo akitupia jicho zaidi kwenye Kikosi cha Usalama Barabarani na maofisa wa vitengo, kikiwemo cha habari.

  Mabadiliko hayo ya viongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani yalikuja siku chache baada ya Mwema kufanya mabadiliko makubwa ya makamanda wa mikoa katika kipindi ambacho wimbi la ujambazi linaonekana kuanza kurejea kwa kasi.
  http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/1369-igp-amwaga-vyeo-polisi-askari-zaidi-ya-500-wanufaika.html

  MY TAKE
  Nina wasi na kuongezwa cheo kwa polisi tu? Jamani tujiulize kulikoni? ndo kuhongwa maafande ili wawashukie vilivyo waandamanji hapo baadae? wawe na umoja? mtapata laana polisi kama hamtaona hiyo ni danganya toto kwenu!
   
 2. M

  MJM JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  This is good news kwa askari wetu wanaofanya kazi katika mazingira magumu na waliosahaulika kwa muda mrefu. Usiishie hapo tu bali pia boresha maisha na mazingira ya kazi ya hawa askari wetu na kutimua wale wasio na maadili ya kazi hiyo. Mungu akutangulie na kukupa hekima katika kazi zako
   
 3. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Itakuwa na maana zaidi kama mayanki watakuwa wamefikiriwa isije kuwa ni wao madingi wamejiandalia EXIT STRATEGY ya kustaafu!!
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wafanye kazi sasa. Makamanda wengi wanafanyakazi na kamera za TV zikiwa migongoni kwao. Uhalifu hautapungua kwa kutuonyesha sura zilezile na silaha zilezile.
   
Loading...