IGP akerwa na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP akerwa na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 21, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkuu wa Jeshi hilo, Inpekta wa Polisi (IGP), Said Mwema

  Jeshi la polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya kuibuka kwa vitendo vya baadhi ya watu kutumia vibaya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kutoa habari za uchochezi zilizolenga kuvuruga Uchaguzi Mkuu.

  Mkuu wa Jeshi hilo, Inpekta wa Polisi (IGP), Said Mwema, alitoa tahadhari hiyo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya utafiti, Teknolojia ya habari na Mawasiliano (Teknohama) na huduma za kijamii kati ya jeshi hilo na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Katika hotuba yake, Mwema alitolea mfano taarifa alizoziita za uzushi zilizozagaa za kukamatwa kwa kontena lenye karatasi feki za kura katika mji waTunduma, mkoani Mbeya ambapo alisema kuwa sio za kweli.

  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia, Profesa John Kondoro, alisema kuwa, makubaliano hayo yamelenga maeneo ambayo ni mafunzo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu kwa jeshi hilo kulingana na mahitaji na makubaliamo maalum.

  Pia alisema tafiti za Teknohama na nyanja ambazo zitasaida kuimarisha na kuboresha jeshi, kutoa huduma za kitaalamu katika jamii na uandishi wa makala mbalimbali.

  Aidha, Kondoro alitaja majukumu ya taasisi hiyo katika ushirikiano huo kuwa ni pamoja na kuezesha jeshi kutumia miundombinu yake pamoja na rasilimali mbalimbali chini ya makubaliano maalum.

  Kadhalika, alisema majukumu mengine ni kutoa mafunzo ya taaluma ya muda mfupi na mafunzo ya kozi za kawaida kwa watumishi wa jeshi.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyumzee atupishe hapa na uzezeta wake..kama yeye hajui maana ya technolojia basi akae pembeni afanye mambo yake ya polisi jamii
   
 3. C

  CAIN Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine humu ni wanafiki wakubwa. Polisi ikikaa kimya bila hata ya kutoa tahadhari ya mambo inaonekana imelala, ikitahadharisha inaonekana zezeta. Sasa hivi watu wanataka ifanyeje??? yaani unajua mimi huwa sipati majibu kabisa ya hawa watu ni wa aina gani!!!

  Sielewi pia kwa watu wa namna hii wanatoka katika jamii ya watu gani???

  Kwa kweli sipati majibu zaidi ya kufikiri huenda wakawa na matatizo ya kiakili..
   
Loading...